Posts

Showing posts from September, 2020

UN yamuunga mkono Magufuli kutokomeza ukatili wa mwanamke Ikungi

Image
     Picha ya pamoja ya Mkuu wa mkoa wa Singida  Dk. Rehema Nchimbi(mwenye kilemba) na       wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo mara baada ya uzinduzi wa mradi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi(kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania, Zlatan Milisic baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi    Na John Mapepele, Ikungi  MKUU wa  Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi  leo amezindua  miongoni mwa miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa nchini, mradi wa  pamoja  baina ya Mashirika ya Kimataifa ya UN Women na UNFPA kupitia ufadhiri  wa  Shirika la KOICA wa Tuufikie usawa  wa jinsia kupitia kuwawezesha wanawake na wasichana utakaogharimu takribani bilioni 11.5 za kitanzania  ambao utatekelezwa  katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida na Msalala mkoani  Shinyanga katika kipindi cha  miaka mitatu k...

BENKI YA I&M TANZANIA YAZINDUA KLABU YA MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WAKE

Image
  Timu ya wafanyakazi wa I&M Benki walipozindua klabu yao ya michezo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, Maktaba Square jijini Dar es salaam Timu ya wafanyakazi wa I&M Benki walipozindua klabu yao ya michezo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, Maktaba Square jijini Dar es salaam Timu ya wafanyakazi wa I&M Benki walipozindua klabu yao ya michezo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, Maktaba Square jijini Dar es salaam  Timu ya wafanyakazi wa I&M Benki walipozindua klabu yao ya michezo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, Maktaba Square jijini Dar es salaam                                           ............................................................................... Siku ya ijumaa tarehe 11 Septemba 2020, benki ya I&M Tanzania ilizindua klabu ya michezo kwaajili ya wafanyakazi wake kupitia kamati yake ya mabadiliko ...

I&M BANK YAKUTANA NA WATEJA KWENYE CHAI YA ASUBUHI

Image
  Timu ya wafanyakazi wa I&M Bank ikiongozwa na mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Baseer Mohammed, wakuu wa idara mbalimbali, meneja wa matawi ya Dar es salaam pamoja na wateja katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam. Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M, Bw. Baseer Mohammed akiongea na wateja wakati wa kikao kifupi na wateja Golden Tulip siku ya Ijumaa 11 Septemba. Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja wa Benki ya I&M,  Lilian Mtali akifafanua jambo wakati wa kikao cha wateja kilichofanyika ijumaa 11 septemba Hoteli ya Golden Tulip Masaki ....................................................................... Benki ya I&M Tanzania leo 11 septemba 2020 imekutana na wateja wake katika Hotel ya Golden Tulip kama ilivyo ada ya Benki ya I&M Tanzania kukutana na wateja wake kwaajili ya kujadiliana mada mbalimbali zinazohusiana na huduma za kibenki, changamoto na njia za kuwapatia wateja wake suluhisho ili wafurahie hudu...

WORLD VISION YAWANOA WANAHABARI KUHUSU LISHE NA AFYA YA UZAZI

Image
  Meneja wa Mradi wa ENRICH, Bi Mwivano Malimbwi (aliyesimama) akitoa mafunzo maalum ya malengo ya mradi huo ya utoaji wa elimu ya lishe na kuboresha afya ya uzazi kwa vijana balehe kwenye  mikoa ya Singida na Shinyanga kwa waandishi wa habari ya Mkoa wa Singida (hawapo pichani) leo, aliyekaa  ni mtaalam wa Jinsia na Utetezi wa Mradi Huo Tumaini Fred Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akiangalia mazao ya asali na mashine ya kukamulia asali  ya kikundi cha ufugaji wa nyuki mkoani Singida kinachofadhiliwa wa World Vision hivi karibuni Na. John Mapepele ,Singida Shirika la World Vision nchini  limewataka waandishi wa habari kama wadau wakuu wa Shirika  hilo  kutoa taarifa sahihi za kazi za  shirika hilo  kwenye mradi wake wa ENRICH  ambao unatekelezwa  katika  mikoa ya Singida na Shinyanga. Mradi huo unalengo la kupeleka elimu ya lishe na afya ya uzazi kwa vijana balehe vijiji...

SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AWAFUNDA TAKUKURU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Image
Spika wa Bunge Job Ndugai (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida jana. Kutoka kulia ni Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Manyoni,  Jarome Mpanda, Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa, Sabina Seja, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kepteni Mstaafu George Mkuchika, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Magwisa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi, Yahaya Masere. Spika wa Bunge Job Ndugai (katikati) akipiga makofi baada ya kuweka jiwe la msibgi la  jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida. Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kepteni Mstaafu George Mkuchika, akizungumza kwenye hafla hiyo. Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa, Sabina Seja,   akizungumza kwenye hafla hiyo.  Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Magwisa,...

SERIKALI YATUMIA SH.BILIONI 470.4 KUTEKELEZA MIRADI MKOANI SINGIDA

Image
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya Wananchi (hawapo pichani) katika  mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Bombadia mjini Singida jana. Umati wa Wananchi wa Mkoa wa Singida wakisikiliza hutuba ya mgombea huyo wa Urais Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu akijinadi kwa Wananchi mbele ya  Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Francis Isack akijinadi kwa Wananchi mbele ya  Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo,  akijinadi kwa Wananchi mbele ya  Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Yahaya Masere akijinadi kwa Wananchi mbele ya  Mg...