Thursday, July 29, 2021

SERIKALI YATOA SH.173 MILIONI KWA AJILI YA MAFUNZO YA UFUNDI KWA VIJANA SINGIDA.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima, akionesha umahiri kwa kushona nguo wakati alipotembelea chuo cha  ufundi na marekebisho kwa watu  wenye ulemavu cha Sabasaba (VTC) kilichopo Kata ya Utemini mjini hapa..

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima, akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho.
Mkuu wa chuo hicho, Fatuma Malenga akizungumzia juu ya utekelezaji wa program ya kukuza ujuzi kwa vijana inayofadhiliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima, akimsalimia kwa unyenyekevu mkubwa mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho.
 


Na Dotto Mwaibale, Singida.


SERIKALI imetoa Sh.173.7 kwa ajili ya gharama ya mafunzo ya ufundi kwa vijana mkoani hapa.

Hayo yamesemwa jana na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima wakati alipotembelea   chuo cha  ufundi na marekebisho kwa watu  wenye ulemavu cha Sabasaba (VTC) kilichopo Kata ya Utemini mjini hapa.

Akiwa chuoni hapo Sima aliweza kuzungumza na vijana 70 wanaopata elimu ya ufundi kwa miezi sita kwa ufadhili wa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu. 

Akizungumza na vijana hao Sima alisema akiwa bungeni alitoa hoja kuiomba Serikali kugharamia elimu ya ufundi ili kupata vijana wengi wenye ujuzi ambao wataweza kujitegemea hoja ambayo ilikubaliwa na matokeo yake ndio hayo mafunzo yanayotolewa kwa vijana hao kwa ufadhili wa Serikali. 

Mbali ya chuo hicho vijana wanaonufaika na masomo hayo ni wa Chuo cha VETA chenye wanafunzi 246 na FDC chenye wanafunzi 60.

Sima alitumia ziara hiyo katika vyuo hivyo kuwaomba vijana hao kuzingatia masomo yao hayo ya ufundi ambayo yatawasaidia kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa.

"Jambo kubwa ambalo napenda kuwahimiza someni kwa bidii kwani ufundi mnaojifunza utawasaidia kujiajiri na kuondoa dhana ya kutaka kuajiriwa," alisema Sima.

Mkuu wa chuo hicho, Fatma Malenga alisema hivi sasa wanafanya utekelezaji wa program ya kukuza ujuzi kwa vijana inayofadhiliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo vijana hao wapatao 70 wanajifunza fani za umeme, ushonaji nguo,mapambo,useremala,ujenzi na kupaka rangi. 

Wanafunzi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti walimshukuru mbunge huyo na kumpongeza Rais Samia Saluhu Hassan kwa kutoa fedha zinazowawezesha kupata mafunzo hayo.

MAFIA WASHAURIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA PASS KUKUZA BIASHARA ZAO.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PASS Trust, Anna Shanalingigwa akizungumza Wadau wa kilimo, uvuvi na ufugaji wilayani Mafia katika warsha ya siku mja iliyofanyika jana.

Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Martin Mtemo ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika warsha hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Mafia,Martin Mtemo (katikati) akiwa na timu ya Wafanyakazi wa PASS walipotembelea Kiwanda cha Usamabazaji Samaki cha Mkaire General Supplies kinacho milikiwa na  Ismail Kamugisha Mkazi wa Mafia ambaye amekiboresha baada ya kuwezeshwa na PASS.



Na Mwandishi Wetu, Mafia


WADAU wa kilimo, uvuvi na ufugaji wilayani Mafia wameaswa kutumia fursa ya Upatikanaji wa mikopo ya fedha na zana za kisasa za kutendea kazi zao kupitia huduma zinazowezeshwa na Taasisi ya PASS TRUST ikishirikiana na Kampuni tanzu yake ya PASS LEASING.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Martin Mtemo alipokuwa akizungumza na wadau hao walipokutana katika warsha maalumu ya wiki ya PASS iliyoandaliwa na Kampuni hiyo wilyani humo ambapo pamoja na mambo mengine, Mtemo amewaasa wakulima, wafugaji na wavuvi hao kuunda vikundi ili waweze kunufaika na fursa zinazotolewa na Kampuni hizo pacha.

“Wilaya yetu ya Mafia imebarikiwa kwa kuwa na fursa nyingi katika uvuvi na kilimo, na kama mnavyojua changamoto kubwa ambayo imekuwa ikifanya shughuli hizi ziwe za kusuasua ni ukosefu wa mitaji, Sasa kwa kushirikiana na PASS nawaasa wakulima na wavuvi chukieni hizo pesa muwekeze katika uvuvi na kilimo” alisema mkuu huyo wa wilaya huku akiwatoa hofu wadau hao kuhusu dhana potofu inayopelekea hofu miongoni mwa watanzania katika kuchukua mikopo benki kwa ajili ya kukuza biashara zao.

“Serikali inatambua mchango wa PASS katika kuendeleza shughuli za kilimo nchini, hapo mwanzo wakulima wengi walikuwa hawakopesheki kwa kukosa 

dhamana lakini PASS ni Taasisi ambayo imeanzishwa hapa nchini mahsusi kwa ajili ya kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi kukopesheka katika benki zetu, kwahakika hii ni fursa muhimu sana kwetu na niombe wanamafia msiogope serikali ipo na tunafanya kazi kwa ushirikiano na PASS, kopeni mfanye kazi ili tupate maendeleo” alisema Mtemo.

Kufuatia ufafanuzi wa kina juu ya huduma za kampuni hizo ambapo Meneja wa Kanda ya Mashariki, Hadijali Seif aliwaeleza wadau wa mkutano huo kuwa PASS Trust inawezesha udhamini wa mikopo ya fedha kwa wajasiriamali wa kilimo biashara kuanzia 20% hadi 60% kwa kinababa na 20% hadi 80% kwa vijana na kinamama na baadaye Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa PASS, Hamis Mmomi akafafanua kuwa Kampuni tanzu ya PASS Leasing yenyewe inajikita na ukodishaji wa zana za kutendea kazi katika mnyororo mzima wa kilimo, uvuvi na ufugaji bila dhamana yoyote, wadau hao walieleza kufurahia huduma hiyo na kuomba PASS kuongeza uwekesaji katika wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kuwatembelea mara kwa mara ili wakulima wengi waweze kufikiwa na huduma hiyo.

Miongoni mwa wadau waliotoa maoni yao juu ya huduma za PASS Trust na Kampuni tanzu yake ya PASS Leasing ni Afisa Uvuvi wa wilaya hiyo ya Mafia Anthony Mbega ambaye alidokeza kuwa PASS imekuja kuwa suluhisho kwa wakulima wa wilaya hiyo kwa kujaza nafasi ambayo inaachwa wazi kutokana na bajeti ya halmashauri kutotosheleza mahitaji ya mikopo kwa wajasiriamali.

“Kwa niaba ya wavuvi nashukuru Sana taasisi ya PASS kwa kutuletea fursa hii adimu kwani hapo awali wavuvi wetu wamekuwa wakikosa mikopo kutokana na ufinyu wa bajeti ya halmashauri yetu. Sasa kwakuwa samaki tunao, wavuvi wapo na Sasa PASS wekuja naomba wavuvi na wakula wote na wavuvi undeni vikundi vya ushirika ili kuweza kunufaika zaidi na fursa hii ambayo wawezeshaji hawa wametuletea hapa” aliwaasa Mbega na kuongeza kuwa serikali wilayani humo itahakikisha inafanya kazi kwa karibu na wajasiriamali wote watakaohitaji mikopo ya fedha na zana za kilimo ili kuwawezeha kupata huduma hiyo kiurahisi.

Wakitoa shuhuda jinsi walivyoongeza thamani katika biashara zao, baadhi ya wanufaika wa huduma za PASS walibainisha kuwa udhamini wa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi unaofanywa na Kampuni hiyo umewasaidia kukuza uwekesaji wao na kuzalisha ajira katika Biashara zao za uvuvi na kilimo.

“Sehenmu kubwa ya uwezekaji wangu ambao naufanya katika uvuvi wa meli nimeupata kutokana na udhamini wa PASS ambao walinidhamini nikapata mkopo wa milioni 75 kutoka benki, nikawekeza na ndiyo imenifanya nifikie hatua hii kama mnavyoniona, kwakweli nawashukuru PASS” alisema, Said Issa Kombo mkazi wa Kisiwani Mafia.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya usindikaji na usamabazaji samaki, Mkaire General Supplies, Ismail Kamugisha aliweka wazi kuwa mafanikio yake hadi kuimarisha kampuni hiyo yametokana na mkopo aliowezeshwa na PASS kutoka benki ambapo bila udhamini wa PASS asingekopesheka kutokana na taratibu za kibenki.

“Kwakweli Kampuni ya PASS imenisaidia sana kukuza uwekezaji katika biashara yangu kwani hapo awali nilikuwa nasindika tani 5 kwa siku lakini tangu miaka miwili iliyopita baada ya PASS kuniwezesha kupata mkopo ninasindika hadi tani 800 kwa masaa 22. PASS walinidhamini 75% ya mtaji ambapo nilitumia 25% tu.

ya gharama za kuweza kumiliki mitambo hii ya usindikaji wa samaki” alieleza Mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa kwasasa biashara yake ni kubwa kiasi kwamba pamoja na kuwa msambazaji mashuhuri wa samaki Wilaya ya Mafia pia anasafirisha samaki wa kutosha kwenda katika masoko ya Dar es Salaam.

Maadhimisho ya wiki ya PASS Trust pamoja na PASS Leasing yenye kauli mbiu ya Pamoja tuwezeshe Upatikanaji wa fedha kwa kilimo endelevu yamefanyika wilayani Mafia ikiwa ni Mwendelezo wa maonesho hayo tangu yalipoanza mwanzao Julai 19 mwaka huu mkoani Singida na baadaye Dodoma huku baada ya Mafia kilele chake kikiwa katika Visiwa vya Zanzibar ambapo lengo kuu la Maadhimisho hayo kama ilivyoelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni  ya PASS Anna Shanalingigwa ni kuweza kupata mrejesho kutoka kwa wanufaika wa huduma zake, kuwakutanisha wadau wa sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji ili kujadili changamoto zilizopo na jinsi ya kuzitatua kwa na kutoa elimu na taarifa juu ya huduma za kampuni hiyo ya PASS Trust pamoja na Kampuni tanzu yake mpya ya PASS Leasing ili kuweza kuwapata na kuwasaidia wateja wapya wenye uhitaji wa huduma hizo.

KANISA KATOLIKI JIMBO LA SINGIDA LAPATA PIGO VILIO MAJONZI VYATAWALA KANISANI


Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Ibrahimu Hussein ambaye alikuwa mfanyakazi wa Jimbo Katoliki Singida aliyefariki dunia mwanzoni mwa wiki wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Misheni ya Makiungu mkoani Singida.

Marehemu Ibrahimu Enzi za Uhai wake.

Askofu wa Jimbo Katoliki Singida Mhashamu Edward Mapunda (katikati) akiongoza ibada ya Misa Takatifu ya kuaga mwili wa marehemu Ibrahimu Hussein.Kulia ni Paroko Msaidizi wa Parokia ya  Moyo Mtakatifu wa Yesu, Father Kinanda.
Ibada hiyo ikiendelea.
Askofu wa Jimbo Katoliki Singida Mhashamu Edward Mapunda akinyunyuzia mafuta ya baraka kwenye jeneza la marehemu.
Ibada hiyo ikiendelea.
Huzuni katika ibada hiyo.
Vilio vikitawala katika ibada hiyo.
Vilio vikitawala katika ibada hiyo.
Ni vilio vitupu vikitawala katika ibada hiyo.
Askofu wa Jimbo Katoliki Singida Mhashamu Edward Mapunda akiongoza msafara wakati wa kuingiza jeneza la marehemu kwenye gari tayari kwenda kijijini kwao kwa mazishi.
Watawa wa Jimbo Katoliki Singida wakiwa kwenye ibada hiyo ya kuaga mwili wa marehemu.



Watawa wa Jimbo Katoliki Singida wakiaga mwili wa marehemu.

Ibada hiyo ikiendelea.
Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu.
Wafanyakazi wenzake na marehemu wakiwa kwenye ibada ya kumuaga mwenzao.
 


Na Dotto Mwaibale, Singida


JUMUIYA ya Waumini na Wafanyakazi wa Jimbo Katoliki Singida imepata pigo na kusababisha vilio na majonzi baada ya kumpoteza mmoja wa Wafanyakazi wake mahiri Ibrahimu Hussein ambaye amefariki dunia mwanzoni mwa wiki wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Misheni ya Makiungu mkoani Singida.

Akiongoza ibada ya Misa Takatifu ya kuaga mwili wa marehemu Askofu wa Jimbo Katoliki Singida Mhashamu Edward Mapunda alisema Jumuiya ya Wakatoliki Singida itamkumbuka na kuendelea kumuombea kwa namna alivyojitoa  kutekeleza matendo mema katika kipindi cha uhai wake.

"Tuendelee kumuombea.Kifo cha kimwili sawa...lakini kifo cha kiroho ni kibaya zaidi sababu ni chukizo mbele ya Mungu. Kifo cha kijana huyu ni cha baraka, neema na ni mlango wa kuingia mbinguni.. kumuona Mungu," alisema Askofu Mapunda.

Baadhi ya walioguswa na msiba huo walisema Ibrahimu alikuwa ni kijana wa aina yake kwani hata alipokuwa akitumwa hakuonesha kukataa wakati wote alikuwa akitabasamu.

Mazishi ya marehemu  Ibrahimu Hussein yalifanyika jana nyumbani kwao Mang'onyi wilayani Ikungi mkoani hapa.

Wednesday, July 28, 2021

TAKUKURU SINGIDA YACHUNGUZA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI.1

p>

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida, Mzalendo Widege , akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo katika kipindi cha robo ya nne ya mwakawa fedha 2020/2021. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Adamu Kilongozi.

Maafisa wa Takukuru wakiwa katika kikao hicho cha utoaji wa taarifa kwa waandishi wa habari. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Samson Julius, Mkuu wa Taasisi hiyo Wilaya ya Iramba, Ahmed Sungura na Mkuu wa Taasisi hiyo Wilaya ya Mlalama, Yasini Mohamed. 

Maafisa wa Takukuru wakiwa katika kikao hicho. Kutoka kushoto  ni Paul Kaheshi na  Theopister  Tembo. 
Maafisa wa Takukuru wakiwa katika kikao hicho. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Taasisi hiyo Wilaya ya Ikungi, Erick Nyoni na Hamisi Kilulani.
Afisa Takukuru Mkoa wa Singida, Shemu Mgaya akiwa kwenye kikao hicho.
Maafisa wa Takukuru wakiwa katika kikao hicho cha utoaji wa taarifa kwa waandishi wa habari.


Na Dotto Mwaibale, Singida


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imechunguza miradi ya maendeleo yenye thamani ya  zaidi ya Sh. 1. Bilioni ili kuona utekelezaji wake kama hauna viashiria vya ubadhilifu.

Hayo yalisemwa  na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida, Mzalendo Widege wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za taasisi katika kipindi cha robo ya nne ya mwakawa fedha 2020/2021.

Alitaja miradi ilichunguzwa kuwa ni Afya jumla ya miradi  Saba yenye thamani ya Sh. 820,000,000,  Elimu miradi miwili yenye thamani ya Sh. 70,000,000, Ujenzi wa Majengo ya Halmashauri mradi mmoja wenye thamani ya Sh. 600,000,000 na mradi wa Ujenzi wa Barabara mmoja wenye thamani ya Sh.160,530,000. 

Alisema thamani ya miradi hiyo ni Sh. 1,650,530,000 ambayo ni  kwa mujibu wa fedha zilizoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi husika ya maendeleo.

" Kwa ujumla yaliyobainika wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo ni ukiukwaji wa taratibu za manunuzi kwenye baadhi ya miradi, kukosa ushirikiano wa nguvu za wananchi, ucheleweshaji wa fedha kwenye vituo kutoka Halmashauri na changamoto wakati wa utekelezaji wa sheria mpya inayoelekeza manunuzi ya vifaa kwa wazabuni waliosajiliwa  na GPSA ambao wengi wao gharama zao zipo juu na hivyo kusababisha miradi kutokamilika," allisema Widege.

Katika hatua nyingine taasisi hiyoimetangaza kuwachukulia hatua kali  wote watakao bainika wanatumia nembo nembo ya taasisi kwa vitendo idegevya uhalifu.

" Takukuru inazidi kutoa rai kwa wanan wote kuwa kumekuwepo na wimbi la matapeli ambao wanajifanya ni maafisa wetu, wamekuwa wakipiga simu kwa wananchi na kuwatisha kuwa wanaitwa kwenye ofisi zetu na kuwa wanatuhuma za rushwa jambo ambalo sio la kweli," alisema.

Hata hivyo Widege alitoa onyo kali kwa watu hao aliowaita matapeli kuacha mara moja vitendo hivyo na endapo watakaidi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.


Sunday, July 25, 2021

SERIKALI MKOA WA SINGIDA YAMKABIDHI MWENGE WA UHURU MKUU WA MKOA WA DODOMA

 Mkuu wa Mkoa Singida, Dk.Binilith Mahenge (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru 2021 Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka katika Kijiji cha Naguru wilayani Bai baada ya kuhitimisha mbio zake mkoani humo leo. Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Singida ulitembelea miradi mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh.8 Bilioni.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge (katikati), akisoma taarifa ya mkoa wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa wa Dodoma. Wengine kushoto kwa Dk. Mahenge ni Viongozi mbalimbali wa mkoa huo na kulia ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Singida..


Na Dotto Mwaibale, Singida


SERIKALI  Mkoa wa Singida chini ya Mkuu wa Mkoa huo Dk.Binilith Mahenge  leo asubuhi wamemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Anthony Mtaka baada ya kumaliza mbio zake mkoani humo.

Akisoma hotuba ya makabidhiano Dk. Mahenge alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Singida ulikibimbizwa umbali wa Kilometa 642.3 na jumla ya miradi 55 yenye  gharama ya zaidi ya Sh. 8 Bilioni iliwekewa mawe ya msingi, kuzinduliwa, kufunguliwa na kutembelewa katika sekta za maji, Elimu, Afya, Utawala Bora, Barabara, uwezeshwaji wa Wananchi Kiuchumi na program za mapambano ya UKIMWI, Maralia, Rushwa , mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya, Umuhimu wa Lishe na Matumizi sahihi ya Tehema, ambapo miradi yote ilikubaliwa na Mwenge huo wa Uhuru.

Mahenge aliwapongeza Vijana Sita Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa   kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiongozwa na  Luteni Josephine Mwambashi  na wenzake   Luteni Ramadhani  Msham, Luteni Geofrey  Aron, Luteni Mussa Mussa ,Coplo Rehema Haji na PTE  Dismas Mvula kwa kazi nzuri na kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kazi hiyo muhimu ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru na Ukaguzi wa Miradi kwa kina.

Aidha Mwenge wa Uhuru ulitoa ujumbe kwa Wananchi unaohusiana na Tehema chini ya kauli mbiu TEHEMA ni Msingi wa Taifa endelevu; Itumie kwa usahihi na Uwajibikaji pamoja na mapambano dhidi ya UKIMWI ,Maralia, Rushwa  , Mapambano dhidi Dawa za Kulevya  na umuhimu wa Lishe Bora na vijana sita walifafanua ujumbe wote.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa  LT Josephine Mwambashi akiwaaga wananchi wa Mkoa wa Singida wamempongeza  Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Singida Frederick Ndahani na Timu yake kwa Uratibu  mzuri  wa   mbio za Mwenge na kuwa ulikuwa mzuri na umesaidia kufanikisha mbio hizo mkoani humo.

Pia Mwambashi amewapongeza Wakuu wa Wilaya zote kwa usimamizi wa miradi uliosababisha miradi yote kukubaliwa. 

Mratibu wa Mwenge wa uhuru Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani ambaye pia ni Afisa Vijana wa Mkoa, amewashukuru wananchi, viongozi wa Serikali na Taasisi , Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama  vya Siasa wakiongozwa na Chama Tawala CCM  , Wakurugenzi, Makatibu Tawala, Timu ya Uratibu Mkoa,Waratibu wa Mwenge Wilaya na Wakuu wa Wilaya kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika Mbio za Mwenge wa uhuru  mkoani Singida.

Saturday, July 24, 2021

VIJANA WA VYUO VIKUU SINGIDA WASEMA HUU SIO WAKATI WA KUHITAJI KATIBA MPYA

 

Mwenyekiti wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa  Singida,  Michael Madirisha akizungumza  katika  kikao cha mkutano mkuu wa vyuo hivyo ulioketi mjini hapa leo. Kulia ni Katibu wa Seneti, Paul Dotto na kushoto ni Katibu Hamasa wa Seneti hiyo , Amina  Mussa.


Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Mkutano ukiendelea.
Katibu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa  Singida, Paul Dotto, akizungumza kwenye kikao hicho.
Spika wa Bunge la Serikali ya Wanafunzi ( TIASO) Taasisi ya Uhasibu Tanzania ( TIA) Kampasi ya Singida, Salim Salim akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania ( TIA) Kampasi ya Singida, Masele Richard, akizungumza kwenye kikao hicho.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi ( TIASO) Taasisi ya Uhasibu Tanzania ( TIA) Kampasi ya Singida , Hamisi Ibrahim, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Singida, Vedastus Nkonya, akizungumza kwenye kikao hicho.



Na Dotto Mwaibale, Singida


VIJANA wa Vyuo na Vyuo Vikuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Singida wamesema kwamba wakati huu si wakutafuta katiba mpya bali ni kufanya kazi za kuiletea nchi maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu mkoani hapa Michael Madirisha wakati akizungumza katika  kikao cha mkutano mkuu wa vyuo hivyo ulioketi mjini hapa leo.

" Suala la katiba ya nchi ni  matakwa ya wananchi na sio kundi dogo itakapofika mahali ambapo wananchi tunaihitaji na Serikali itakapoliona hilo italifanyia kazi,". alisema Madirisha.

Alisema kama vijana wa Vyuo na Vyuo Vikuu wa CCM kwa sasa ajenda yao ni maendeleo hivyo wanawaomba vijana wenzao wa Baraza Kuu la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo  (BAVICHA) popote pale walipo waende kuungana nao ili wapaze sauti ya pamoja ya maendeleo.

Alisema vijana wanao wajibu wa kulitumikia Taifa na Taifa lolote lina imani na vijana hivyo wanakazi kubwa kuhakikisha linapata maendeleo.

Alisema vijana wanapaswa kuwa wazalendo wa nchi  na kufanya kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni wakipiga kelele na kutumiwa vibaya na wanasiasa.

 Madirisha alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya  ndani ya nchi yetu.

Alisema katika kipindi cha uongozi wake ndani ya siku 100 Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kukutana na makundi mbalimbali kama wazee, vijana, wanawake kwa lengo la kujua changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi.

Madirisha pia alimpongeza Rais kwa kuondoa asilimia sita kwenye mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na kuendelea kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya awali hadi kidato cha nne.

"Nimpongeze tena Rais wetu kwa kuendelea kuwaamini vijana  ambapo tumeona akilienzi jambo hilo kwa kuwateua na kuwapa nafasi mbalimbali za kiutumishi ndani ya Serikali na kuweka bajeti bora ambayo imelenga kuwanufaisha watanzania wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo katika suala la mikopo imetenga Sh.570 Bilioni kwa ajili ya wanufaika wa vyuo Vikuu kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Alisema mambo haya yanayofanywa na Serikali ndiyo yanayotakiwa kusifiwa na vijana.

Alisema anaipongeza Serikali kwa kusikiliza  malalamiko ya wananchi kuhusu tozo za mihamala ya simu suala ambalo limewagusa watanzania wengiwa hali ya chini ambalo linafanyiwa kazi hivyo kuja na majibu.

Akichangia kwenye kikao hicho Rais wa Serikali ya Wanafunzi ( TIASO) Taasisi ya Uhasibu Tanzania ( TIA) Kampasi ya Singida , Hamisi Ibrahim  alisema kuhusu katiba mpya hadhani kama ni ya muhimu kwa sasa kwani katiba iliyopo imetutoa mbali na haina changamoto yoyote akitolea mfano  tukio la nchi yetu kufiwa na Rais aliyekuwepo madarakani kwa mara ya kwanza ambapo tukiangalia nchi za wenzetu Rais anapokufa au hata kujiuzulu matatizo hutokea  tofauti na hapa kwetu na ni katiba hiyo tulionayo ndiyo imetuvusha katika vipindi mbalimbali.

Alisema ni wajibu wa vijana kujitambua na kutumia akili zao kwa sababu wanaoshawishiwa kushiriki kwenye makongamano hayo ya kudai katiba ni vijana hivyo wana kazi kubwa ya kuelimishana.

Akizungumzia suala la uzalendo alisema ni changamoto kubwa kwani ndio chanzo cha rushwa, kuisemea nchi vibaya hivyo alitoa mapendekezo kwa seneti hiyo kuanzisha madarasa ya kufundisha watu kuhusu uzalendo.

WANASAYANSI CHIPUKIZI WATAKIWA KUPELEKA UJUZI WAO KWA JAMII

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifunga Mashindano ya Wanafunzi  Wanasayansi Chipukizi kutoka Sekondari mbalimbali yaliyofanyika mkoani hapa jana ambayo yaliandandaliwa na Taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST) akizungumza na wanafunzi hao.


Wanafunzi  Wanasayansi Chipukizi kutoka Sekondari mbalimbali, wakionesha kazi zao kwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko alipotembelea mabanda kwenye mashindano hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye mashindano hayo.
Walimu wakiwa kwenye mashindano hayo.
Washindi wa mashindano hayo wakiwa na vyeti vyao baada ya kukabidhiwa.
Wanafunzi wakiwa kwenye mashindano hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye mashindano hayo.



Na Dotto Mwaibale, Singida


WANA SAYANSI Chipukizi wametakiwa kupeleka kwa jamii ujuzi walioupata wakiwa shuleni badala ya kuufungia kwenye makabati.

Wito huo unetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifunga mashindano ya Wanafunzi  Wanasayansi Chipukizi kutoka Sekondari mbalimbali yaliyofanyika mkoani hapa jana ambayo yaliandandaliwa na Taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST)

"Mambo yote mliyojifunza myaboreshe na muende mkayaoneshe huko mbele ya safari kwamba ninyi mtatatua changamoto za wanasingida na nchi yote kwa ujumla na si vinginevyo," alisema Mwaluko.

Alisema kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ni kuwasomesha hivyo walicho kisoma wanatakiwa wakitafsiri na kuacha dhana ya kutaka kuajiriwa hivyo wajiajiri katika kilimo cha alizeti, vitunguu, korosho na fursa nyingine ambazo wanafunzi hao walizionesha katika mabanda yao.

Alisema kupitia mafunzo hayo wataanza kuonesha ubunifu wao wa kilimo kwa kutumia maji kidogo na kupata mazao badala ya kutumia maji mengi.

" Nakuja kutembelea mashuleni ili nione mambo haya mliyojifunza kama yanafanyika na waomba sana mjitahidi changamoto za mkoa wetu wa Singida ziweze kutatuliwa na ninyi kwa kutumia nafasi nzuri mnazo zipata mkiwa masomoni.

Mwaluko aliwaomba waratibu wa mashindano hao kuongeza shule nyingi zaidi kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo na kuwa ataanzisha mkakati wa Siku ya Sayansi katika kila shule na watakuwa wakishindanishwa baina ya shule mbalimbali mkoani hapa.

Alisema mkakati huo utaanzia ngazi ya mtaa, kata, wilaya hadi mkoa na atakaye fuzu atapatiwa zawadi na kupelekwa kushiriki mashindano  ngazi taifa.

Mwaluko aliwata wanafunzi hao wakiwa darasa kujenga tabia ya kuuliza maswali jambo litakalo waongezea uelewa zaidi badala ya kukaa kimya.

Mratibu wa mashindano hayo Mwalimu Nadhiru Bwikizo alisema awali yalikuwa yakifanyika ngazi ya taifa lakini sasa hivi yanafanyika mikoani na wanaofanya vizuri wanapata nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi pamoja na kupatiwa zawaidi.

Alisema mkoa wa Singida kwa mwaka 2012 na 2013 kuna wanafunzi kutoka Shule za Ilongero,.Mughanga, Dkt.Salmin Amour na Kijota walifanikiwa kupata nafasi za masomo nje ya nchi baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo ngazi ya Kitaifa.

Wanafunzi Stephen Tesha na Qessar Marsha ambao walipata vyeti baada ya kufanya vizuri katika mashindano hayo walitoa wito kwa wenzao kusoma zaidi masomo ya sayansi kwani yana fursa nyingi  katika maisha hasa wakati huu wa dunia ya sayansi na teknolojia.

Friday, July 23, 2021

MIRADI YA SH.2.9 BILIONI YAZINDULIWA MBIO ZA MWENGE WILAYANI IKUNGI

Mkuu wa Wilaya ya Singida Paskas Mulagiri akimkabidhi Mwenge wa Uhuru 2021 Mkuu wa wilaya Ikungi, Jerry Muro katika Kijiji cha Utaho baada ya kuhitimisha mbio zake wilayani humo leo. Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Ikungi unatarajiwa kupitia miradi mbalimbali yenye thamani ya Sh..2.9  Bilioni.

Mwenge wa Uhuru 2021 ukikimbizwa kabla ya kukabidhiwa Wilaya ya Ikungi.

Waratibu wa mbio za Mwenge Mkoa wa Singida wakiwa kwenye makabidhiano ya Mwenge huo.
Kurukaruka kwa furaha kukiendea wakati wa makabidhiano ya Mwenge huo.
Furaha tupu kwenye makabidhiano ya Mwenge huo
Mwenge wa Uhuru ukipokelewa.
Wanafunzi wakiwa kwenye mapokezi hayo.
Kurukaruka kwa furaha kukiendea wakati wa makabidhiano ya Mwenge huo, hawa ni wapambanaji kutoka Wilaya ya Singida.
Wananchi wakiwa kwenye makabidhiano ya Mwenge huo.
Wananchi wakiwa kwenye makabidhiano ya Mwenge huo.
Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yakiendelea. 
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye makabidhiano ya Mwenge huo.
Wananchi na Vijana wa Skauti wakiwa kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
Wanafunzi wakiwa kwenye mapokezi hayo.
Vijana wa Skauti wakimvika Skafu mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Mkuu wa wilaya Ikungi, Jerry Muro akimkabidhi zawadi Mkimbiza Mwenye wa Uhuru Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi.
Furaha tupu eneo la makabidhiano.
 


Na Dotto Mwaibale, Ikungi.


SERIKALI Wilayani Ikungi Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na wananchi mapema leo asubuhi wameupokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Manispaa ya Singida ambapo utazindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye  thamani ya Sh. 2.9 Bilioni 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Mwenge huo na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri katika Kijiji cha Utaho, Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro alisema  Mwenge huo utakimbizwa  kilometa 92.5 na kukagua miradi ya maendeleo.

Alisema Mwenge huo utaanza mbio zake kwa kutembelea Shule ya Msingi Semamba kukagua madarasa na mindombinu iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na kuzindua klabu ya rushwa na kupanda miti.

Alitaja baadhi ya miradi mingine itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru kuwa ni Mradi wa ufyatuaji wa Matofali wa Kikundi cha Jitume Vijana, Mradi wa TEHAMA Sekondari ya Ikungi, Kuweka jiwe la msingi la Kituo cha Mafuta cha JMC, kukagua mifumo ya huduma ya afya Kituo cha afya Ikungi na kuzindua vyumba vya maabara za Sayansi Shule ya Sekondari ya Unyahati.

Muro alitumia nafasi hiyo kuwatambulisha viongozi mbalimbali waliokuwepo kuupokea Mwenge wa Uhuru akiwepo Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Winfrida Funto ambaye alikuwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM), Wajumbe wa Kamati ya Siasa na Sekretarieti, Wabunge, Wananchi, Viongozi wa dini, Watumishi wa Halmashauri hiyo Madiwani na wanafunzi.