Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Ahmed Abbas Ahmed (kushoto) akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji wa Bohari ya Dawa (MSD), Victor Sungusia wakati wa mkutano mkuu wa MSD na wadau wake wa Mkoa wa Ruvuma uliofanyika Aprili 8, 2024, Na Mwandishi Wetu, Ruvuma MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Ahmed Abbas Ahmed, amewataka watumishi wa sekta ya afya Mkoani Ruvuma, kuzingatia weledi na kutoa huduma bora kwa wananchi, ili kuakisi maboresho na uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye sekta ya afya, chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita. Kanali Ahmed amesisitiza kuwa, serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi kwa ajili ya maboresho na ujenzi wa miundombinu ya afya mathalani majengo, ununuzi wa bidhaa za afya na kuwezesha ajira za kutosha, lengo likiwa kuinua hadhi ya huduma zinazotolewa nchini, hasa zinazomgusa mtanzania wa kawaida. Kanali Ahmed ametoa rai hiyo hii leo, wakati wa akifungua kikao kazi baina ya MSD Kanda ya Iringa na ...