Thursday, June 30, 2022

RC SINGIDA ATAHADHARISHA WANANCHI KUTOUZA CHAKULA OVYO, HALI NI MBAYA

 Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akizungumza na Wananchi wa Ikungi  mkoani humo katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi uliofanyika viwanja vya Stendi ya Mabasi leo Juni 30, 2022.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi wakipokea kero kutoka kwa mwananchi aliyefika kwenye mkutano huo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali katika mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi (ACP) Lukas Mwakatundu akizungumza kwenye mkutano huo. 
 Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi (ACP) Phaustine  Ngunge akizungumza kwenye mkutano huo. 
Mkutano ukiendelea.
Mkuu Mpya  wa Polisi Wilaya ya Ikungi (OCD) Susan akijitambulisha rasmi katika mkutano huo.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.

Mhandisi Fred Nkosya kutoka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Singda akizungumzia mikakati ya ujenzi wa barabara wilaya ya Ikungi.

 Mhandisi wa TANESCO Mkoa wa Singida, Onesy  Mbembe akizungumzia ukamilikaji wa usambazi wa umeme mkoani hapa ambapo alisema hadi kufikia Juni mwakani vijiji vyote vya Mkoa wa Singida vitakuwa vimepata umeme.

Afisa Mfawidhi wa Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) Mkoa wa Singida Layla Daffa akielezea umuhimu wa kudai lisiti kwa abiria jambo litaaaaaakalosaidia kuwabaini wamiliki wa mabasi wanaotoza nauli kinyume na  ile iliyopangwa na Serikali.

Wednesday, June 29, 2022

DC SOPHIA KIZIGO AWAALIKA WAWEKEZAJI KWENDA KUWEKEZA KILIMO CHA KOROSHO MKALAMA

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Sophia Kizigo akiwaonesha Wananchi wa Kata ya Iguguno korosho ambazo kwa mara ya kwanza zimeanza kuzalishwa wilayani humo wakati wa mkutano wa kupokea kero ulioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge uliofanyika jana.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Sophia Kizigo akifurahi waakti akipeana mkono na  Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge baada ya kumkabidhi korosho ambazo kwa mara ya kwanza zimeanza kuzalishwa wilayani humo wakati wa mkutano wa kupokea kero za wananchi uliofanyika jana Kata ya Iguguno.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge. akizungumza na wananchi wa Kata ya Iguguno wakati wa mkutano huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama wakiserebuka wakati wa uzinduzi wa wimbo maalum wa kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi pamoja na mapokezi ya Mwenge Uhuru ambao utalala katika kata hiyo mara utakapo wasili wilayani humo, uliotungwa na vijana wa kata hiyo na ndani yake kuchombwezwa maneno na DC Kizigo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi (ACP) Lucas Mwakatundu akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mkoa wa Singida, Agustino Mwakyembe akizungumza kwenye mkutano huo.
Wananchi wa Kata ya Iguguno wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wa Kata ya Iguguno wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wa Kata ya Iguguno wakiwa kwenye mkutano huo.
Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Singida, Phaustine Ngunge akizungumza kwenye mkutano huo ambapo aliwaomba wananchi kutoa taarifa pale wanapowaona watu wanaowahisi ni wageni ambao wanaingia wilayani humo bila ya kufuata taratibu hasa wakati huu wa msimu wa mafuno ya mazao ambayo wanakuja kuyanunua kutoka nchi jirani.
Afisa Mtendaji Kata ya Iguguno Josia Pangani akitoa taarifa ya maendeleo ya kata hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Mesos akizungumzia utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo ambapo Serikali imetoa zaidi ya Sh.5 Bilioni kuitekeleza.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania      (TANROADS) Mkoa wa Singida, Msama K. Msama akizungumzia utekelezaji wa miradi ya barabara ambapo Serikali imetoa zaidi ya Sh.19 Biilioni kwa ajili ya kazi hiyo.
Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu (LATRA) Mkoa wa Singida, Layla Daffa akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu viwango mbalimbali vya nauli.
Mganga  Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick akizungumza kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mhandisi wa TANESCO Mkoa wa Singida, Onesy Mbembe  akizungumzia mikakati ya usambaji umeme mkoani humo.
Kaimu Meneja wa TANESCO Wilaya ya Mkalama, Kasim Juma akielezea mipango wa kuwafungia umemewateja wapya wa Kata ya Iguguno.
Madiwani wa Kata ya Iguguno wakitambulishwa kwenye mkutano huo. Kulia ni Barnaba Mang'ola na Diwani wa Viti Malumu wa kata hiyo, Mariam Kahola.
Wakazi wa Kata ya Iguguno wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kueleza kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge (hayupo pichani)

TARI YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI WA KILIMO LA KUMPELEKA MTAALAM WA ZAO LA KOROSHO MANYONI

Mratibu wa Utafiti wa zao la Korosho Kitaifa kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele, Dk. Geradina Mzena akizunguza katika hafla fupi ya kumpokea Mtaalam wa Kilimo Bora cha zao la Korosho iliyofanyika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ikiwa ni utekelezaji wa  agizo la Waziri wa Kilimo la kuitaka TARI kumpeleka mtaalam huyo wilayani humo ili kwenda kuwasaidia wakulima wa zao hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Melkzedeki Humbe akiishukuru Serikali na TARI kwa hatua ya kumpeleka mtaalam huyo ambaye walikuwa wakimuhitaji kwa siku nyingi kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wa zao hilo wilayani humo.

Tuesday, June 28, 2022

RC SINGIDA AAGIZA WAKURUGENZI KUSHIRIKI ZIARA ZAKE BILA KUTUMA WAWAKILISHI

Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Misigiri kilichopo Kata ya Ulemo wilayani  Iramba mkoani humo kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

 


Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumza na wananchi katika mnada wa Kitukutu ambapo pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge alipata fursa ya kuzungumza nao na kupokea kero zao.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba, Pius Sangoma akizungumza kwenye ziara hiyo.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi (ACP) Lukas Mwakatundu akizungumza na wananchi hao ambapo aliwaomba wafanye shughuli za ujasiriamali kama za kufungua migahawa na hoteli za kulala wageni na vijana kutojiingiza katika vitendo vya wizi katika malori ya mizigo yanayoegeshwa katika eneo la Misingiri jambo litakalo wafanya madereva wa magari hayo kupata muda wa kupumzika na hivyo kupunguza ajali zinazotokea Mlima wa Sekenke kutokana ka kuwa na usingizi.
Mkazi wa Kijiji cha Misigiri  akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Mkazi wa Misigiri Evalyene Lyanga akizungumzia kero ya maji inayohusu bili kubwa na malipo ya fidia za nyumba zao zinazotakiwa kupisha ujenzi wa stendi ya mabasi.
Mkazi wa Kata ya Ulemo Elinipendo akiuliza swali kuhusu bima ya afya.
Mkuu wa Mkoa ya Singida Dk. Mahenge akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
Mkazi wa Kijiji cha Misigiri, Rhoda Philipo akizungumzia mama yake mzazi kupotea katika mazingira ya kutatanisha tangu mwaka jana ambapo hadi leo hii hajulikani alipo.
Wananchi wa Kijiji cha Misigiri wakiwa wamejipanga foleni tayari kwa kutoa kero zao kwa mkuu wa mkoa.
Maswali kuhusu Bima ya Afya yakijibiwa.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Bi. Elizabeth Shalua akitoa kero yake.
Mkazi wa Kijiji cha Misigiri, Shelua Gelema akielezea jinsi walivyopata eneo la mnada wa Kitukutu ambapo kuna mkazi mmoja wa eneo hilo amewatishia waondoke kwa kutumia silaha aina ya bastora.
Mhandisi wa TANESCO Mkoa wa Singida, Onesy  Mbembe akijibu maswali ya wananchi.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida, Msama K. Msama akielezea mikakati ya ujenzi wa barabara katika wilaya hiyo.

 

Na Dotto Mwaibale,Singida


WAKURUGENZI wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Singida wametakiwa kuhudhuria ziara zote za mkuu wa mkoa  huo za kusikiliza kero za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi  bila ya kuwatuma wawakilishi wao.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge leo Juni 28, 2022 baada ya kupata taarifa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba,Mhandisi Michael Matomora hayupo kwenye mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Misigiri kilichopo Kata ya Ulemo wilayani  Iramba kwa ajili ya kusikiliza kero zao.

"Mkurugenzi yuko wapi, hawa wananchi wakitoa kero nani atazitatua, namwelekeza RAS (Katibu Tawala wa Mkoa) RC (Mkuu wa Mkoa) ninapofanya ziara wakurugenzi wawepo na kama kuna ruhsa nijulishwe nafasi yake itawakilishwa na mtumishi mwingine," alisema na kuongeza.

"Hapa nina Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania ( TANROADS) ana kazi nyingi sana, nina Meneja Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA),nina watu wa maji Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wapo hapa ni kwasababu tunataka kero zao wazisikilize moja kwa moja kutoka kwa wananchi," alisema.

Dk.Mahenge alisema yeye ni mwakilishi wa rais hivyo kero za wananchi rais atazipata moja kwa moja kwasababu wananchi wana haki ya kumweleza kero zao.

Alisema kulikuwa na ulazima gani kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ua Iramba kwenda kuhudhuria mkutano wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kwanini asingetuma mwakilishi kwenda huko ili yeye (DED) ashiriki ziara.

"Marufuku DC (Mkuu wa Wilaya) na nipate maelezo kama hakukuwa na mtu mwingine wa kwenda huko mpaka aende yeye tu, hata aliyemwita alipaswa anieleze mimi Mkuu wa Mkoa kwamba tunajua una ziara lakini tunamwitaji DED tuone kama ni yeye tu ndo anatakiwa aende maana halmashauri ni taasisi," alisema.

Akizungumzia kero ya maji iliyotokewa na wananchi aliigiza Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira  (RUWASA) mkoani hapa kwamba wiki ijayo wananchi wa kijiji cha Misigiri waanze kupata mara baada ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukamilisha kufunga transifoma ili mota za kusukumia maji zianze kufanya kazi.

Kuhusu elimu aliwapongeza wananchi wa Wilaya ya Iramba kwa kuchangia fedha za chakula kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 76 na za sekondari 25 hatua ambayo imesaidia wilaya hiyo kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la Saba na kidato cha nne.

"Msingi wa mwanafunzi kufanya vizuri ni pale tu anapokuwa hana njaa akiwa darasani, nawashukru wananchi wa Iramba kwa kuendelea kuchangia fedha za chakula," alisema.

Aidha,Mkuu wa Mkoa aliwahidi wananchi hao kuwa kero zote walizoziwasilisha serikali itazifanyia kazi. Katika ziara yake RC anaongoza na watalaam wa idara zote za serikali ambao hueleza kazi zilizofanywa na serikali na zinazoendelea kufanyika na kujibu kero za wananchi zinazo husu maeneo yao.

Katika hatua nyingine Dk.Mahenge aliagiza kufanyike uchunguzi baada ya mama mmoja Maria Isaya kudai wajawazito wilayani humo wanatozwa fedha wanapoenda kujifungua ambapo kwa mtoto wa kiume ni  Sh.60,000 na mtotowa kike Sh.50,000 na mjamzito anapotakiwa kufanyiwa upasuaji anatakiwa atoe kuanzia Sh. 200,000 hadi 300,000 na huku madai mengine yakiwa ni kujinunulia vifaa vya kujifungulia kwa kutozwa Sh.60,000 ili hali huduma hiyo inatolewa bure na Serikali.