Wednesday, September 30, 2020
UN yamuunga mkono Magufuli kutokomeza ukatili wa mwanamke Ikungi
Thursday, September 17, 2020
BENKI YA I&M TANZANIA YAZINDUA KLABU YA MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WAKE
Timu ya wafanyakazi wa I&M Benki walipozindua klabu yao ya michezo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, Maktaba Square jijini Dar es salaam
Timu ya wafanyakazi wa I&M Benki walipozindua klabu yao ya michezo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, Maktaba Square jijini Dar es salaam
Timu ya wafanyakazi wa I&M Benki walipozindua klabu yao ya michezo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, Maktaba Square jijini Dar es salaam
...............................................................................
Siku ya ijumaa tarehe 11 Septemba 2020, benki ya I&M Tanzania ilizindua klabu ya michezo kwaajili ya wafanyakazi wake kupitia kamati yake ya mabadiliko ya kitamaduni ambapo wamedhamiria kuongeza ari kwa wafanyakazi wake kwa njia ya michezo mbalimbali ikiwemo mbio fupi za riadha ambazo hufanyika kila wiki pamoja na michezo mingine kama vile gofu, mpira wa miguu, mpira wa kikapu na mpira wa mikono.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja alisema, “Tumeamua kuanzisha klabu hii ili kuhamasisha wafanyakazi wetu kuwa na afya bora, kuchangamka kiakili na kuongeza mapato kwenye benki yetu kwani wafanyakazi watakua na uwezo maradufu wa kufikiria mbinu mbalimbali za kuongeza biashara.”
Viongozi wa klabu hiyo ambao ndio walisimama kidete kuhakikisha timu ya wafanyakazi imeweza kushiriki kikamilifu katika riadha ambayo ndio ilifungua dimba la klabu hiyo, Bi Anitha Pallangyo, Meneja wa masoko na mawasiliano wa Benki ya I&M na Bi. Juliana Mtei Meneja wa kitengo cha fedha walifurahia uzinduzi huo na kuongeza kuwa wana mipango mingi kupitia klabu hiyo kuhakikisha jina la Benki ya I&M linang’ara hasa kwa upande wa michezo.
Timu ya wafanyakazi wa Benki ya I&M wakiongozwa na Mkurugenzi wa benki hiyo Baseer Mohammed walifanya riadha fupi kutoka makao makuu ya benki hiyo kwenda viwanja vya coco beach pamoja na kurudi wakiwa wamevailia jezi za michezo za klabu hiyo ikiwa ni moja ya michezo ambayo imedhamiria kuimarisha afya za wafanyakazi.
Bw. Baseer Mohammed akiongea na mwandishi wetu alisema, “Najivunia sana kuwa na timu shupavu iliojaa vijana wenye nguvu na maarifa, pia wenye uthubutu wa kuipeleka benki kwenye levo nyingine kwa kuitangaza kupitia sekta ya michezo. Faida ya michezo kwa wafanyakazi ni pamoja na kuamsha ari ya kufanya kazi, kupunguza mawazo, kuongeza ufanisi wa akili, kuamsha timu pamoja na kuongeza mahusiano mazuri kazini.
Benki ya I&M pia imetajwa kuwa ni benki bora yenye nguvu nchini Kenya ambapo imeonekana ikiwa na fursa kubwa za ukuaji pamoja na kutengeneza faida zaidi. Benki ya I&M kwa sasa ipo Tanzania, Kenya (makao makuu), Rwanda, Mauritious (Bank One) na hivi karibuni Uganda
Saturday, September 12, 2020
I&M BANK YAKUTANA NA WATEJA KWENYE CHAI YA ASUBUHI
Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja wa Benki ya I&M, Lilian Mtali akifafanua jambo wakati wa kikao cha wateja kilichofanyika ijumaa 11 septemba Hoteli ya Golden Tulip Masaki
.......................................................................
Benki ya I&M Tanzania leo 11 septemba 2020 imekutana na wateja wake katika Hotel ya Golden Tulip kama ilivyo ada ya Benki ya I&M Tanzania kukutana na wateja wake kwaajili ya kujadiliana mada mbalimbali zinazohusiana na huduma za kibenki, changamoto na njia za kuwapatia wateja wake suluhisho ili wafurahie huduma za benki yao.
Akiongea kwenye kikao hicho, Baseer Mohammed Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo alisema, “Kwaniaba ya wafanyakazi wote wa Benki ya I&M napenda kuwashukuru wateja wetu wote mlioweza kuitikia wito na kuhudhuria kikao hiKi kifupi chenye mada zenye tija kwa maendeleao ya benki na wateja kwa ujumla. Hiki kikao kwaajili yenu hivyo msisite kuuliza maswali na kuchangia mada zitakazoleta maboresho makubwa kwenye huduma zetu.
Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja, Lilian Mtali pia aliongezea kwa kusema, “hiki kikao ni muhimu sana kwetu kwani tunategemea sana mrejesho wenu kuhusiana na huduma zetu na wapi tuboreshe ili kuhakikisha tunawapa huduma bora sana. Tunashukuru sana kwa mawazo yenu, maoni kuhusu maboresho pia pongezi mlizotupa tunawaahidi tutafanya Zaidi ili kuhakikisha I&M ni benki pekee ambayo mtakua mkiifikiria mtakapohitaji huduma bora za kibenki.
Wateja pia hawakua mstari wa nyuma kwani walifurahia sana ukaribu ambao benki hiyo umeweka kukutana na wateja wao na kuhakikisha wanapata huduma bora Zaidi na za kisasa za kibenki. Wameipongeza benki ya I&M kwa huduma bora, uharaka katika kujibu changamoto za wateja, pia mifumo ya kidijitali kuhakikisha wateja wanapata huduma saa 24 kupitia iClick, na huduma za kibenki kwa njia ya simu *150*32#.
Mbali na matawi yaliopo Dar es salaam Nyerere, Maktaba, Tawi kuu, Kariakoo na Oysterbay, benki ya I&M pia ipo Moshi, Arusha na Mwanza na muda si mrefu inaanzisha huduma za wakala maeneo mbalimbali na mikoa mbalimbali ili kufikisha huduma kwa haraka.
Friday, September 4, 2020
WORLD VISION YAWANOA WANAHABARI KUHUSU LISHE NA AFYA YA UZAZI
Meneja wa Mradi wa ENRICH, Bi Mwivano Malimbwi (aliyesimama) akitoa mafunzo maalum ya malengo ya mradi huo ya utoaji wa elimu ya lishe na kuboresha afya ya uzazi kwa vijana balehe kwenye mikoa ya Singida na Shinyanga kwa waandishi wa habari ya Mkoa wa Singida (hawapo pichani)
leo, aliyekaa ni mtaalam wa Jinsia na Utetezi wa Mradi Huo Tumaini
Fred
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akiangalia mazao ya asali na mashine ya kukamulia asali ya kikundi cha ufugaji wa nyuki mkoani Singida kinachofadhiliwa wa World Vision hivi karibuni
Na. John Mapepele,Singida
Shirika la World Vision nchini limewataka waandishi wa habari kama wadau wakuu wa Shirika hilo kutoa taarifa sahihi za kazi za shirika hilo kwenye mradi wake wa ENRICH ambao unatekelezwa katika mikoa ya Singida na Shinyanga.
Mradi huo unalengo la kupeleka elimu ya lishe na afya ya uzazi kwa vijana balehe vijijini ili kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto chini ya siku 1000 na ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ili kuboresha maisha ya watanzania.
Akitoa mafunzo maalum kuhusu malengo wa mradi kwa waandishi wa Mkoa wa Singida , Meneja wa Mradi wa ENRICH Bi, Mwivano Malimbwi amesema mradi huu ni wa miaka mitano kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2021 na umejikita katika kuwezesha huduma za lishe ili kuimarisha afya ya mama na mtoto kwa gharama za dola milioni 8.4 za kikanada.
Kwa mujibu wa Malimbwi malengo mahususi ya ENRICH ni kupunguza vifo vya akina mama na watoto kwa kuangalia visababishi vya vifo hivyo ambapo mradi umeelekeza nguvu kwenye kuimarisha mifumo ya utoaji wa afya katika vituo vya kutolea huduma hizo.
Aliongeza kuwa awali wakati mradi ulipoanza walibaini changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya kumchunguza hali ya kiliishe ya mtoto vilikuwa na upungufu mkubwa ambapo vituo vichache vilikuwa na vifaa hivyo vya kupimia urefu na mzingo wa kati wa mkono kwa akina mama na mtoto
Alisema kuwa watoa huduma wachache walipata mafunzo ya afya ya lishe kwenye ngazi ya mkoa na wilaya ambapo hakukuwa na watoa huduma katika maeneo ya vijijini.
Aidha alisema pia hakukuwa na elimu ya uongozi kwenye kamati za afya za mikoa na wilaya ambapo Mradi uliwajengea uwezo ili kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko kwa pamoja badala ya kuwa watoa maamuzi.
Aidha mipango na bajeti ilikuwa ikifanywa kwa hisia badala ya kutumia takwimu sahihi.
Malimbi amesema lengo la pili la Mradi ni kuongeza uzalishaji wa chakula chenye uwingi wa virutubisho ambapa kwenye eneo hili amessisitiza kuwa mkakati umekuwa katika kuongeza uzalishaji ulioongezwa kibailojia, kuongeza utumiaji wa virutubishi kwa watoto na sayansi ya ulaji na ufyonzaji wa virutubishi,
Alisema pia katika mikoa ya Singida na Shinyanga imebarikiwa kuwa na vyakula vya makundi yote na matunda ya asili kama sasati, rade na furu ambayo kama yakitumika kikamilifu yatasaidia sana kuboresha lishe na kupunguza udumavu kwa watoto.
Alipongeza jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Dk. Rehema Nchimbi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa suala la lishe na afya ya uzazi vinakuwa kipaombele cha kwanza kwa wananchi ambapo pia amesema amehamasisha ulaji na ulimaji wa viazi lishe na kuwafanya wananchi wa Mkoa wa Singida tofauti na awali ambapo vilikuwa vikiuzwa nje ya Mkoa.
Aidha amesema Mradi umehamasisha akina mama kulima bustani za mbogamboga kwenye kila kaya ili kuhakikisha kuwa kwenye kila mlo mboga zinakuwepo.
Amesema lengo la mwisho la mradi huo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na uwajibikaji wa wadau wote muhimu na kila mmoja anafanya majukumu yake kwa ufasaha, ambapo ametolea mfano kuwa Serikali kama mdau mkuu ina wajibu wa kuweka vituo vya kutolea huduma na mtoa huduma ambapo jamii inawajibu wa kuvitumia vituo hivyo na watoa huduma.
Mradi wa ENRICH ni Mradi wenye sekta nyingi na unafadhiliwa na Serikali ya nchi ya Canada ambapo unatekelezwa kwa kushirikiana na wabia ambao ni Nutritional International, Canadian Society for International Health anayejikita katika kuimarisha mfumo wa afya.
Ikiwemo Harvest Plus, kwenye Sekta ya Kilimo, Chuo kikuu cha Toronto katika kufanya tathimini na ufuatiliaji wa mradi na World Vision ambaye ni msimamizi mkuu wa fedha wa mradi huo. Serikali ya Tanzania ni mtekelezaji namba moja chini ya TAMISEMI.
Thursday, September 3, 2020
SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AWAFUNDA TAKUKURU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa, Sabina Seja, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo hilo.
Wananchi wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo hilo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondary ya Mlewa wakitoa burudani.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Tuesday, September 1, 2020
SERIKALI YATUMIA SH.BILIONI 470.4 KUTEKELEZA MIRADI MKOANI SINGIDA
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Francis Isack akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo, akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Magufuli.Mgombea Ubunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Yahaya Masere akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe,akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Tatu Ntandu,akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Gwau,akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mussa Sima, akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Magufuli.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SERIKALI imetumia Sh. Bilioni 470.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Singida.
Hayo yalisemwa na Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Magufuli wakati akiwahutumia maelufu ya wanannchi katika mkutano wake wa pili wa kampeni wa kuomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa awamu ya pili uliofanyika viwanja vya Bombadia mjini hapa jana.
Magufuli alisema katika kipindi cha miaka mitano Serikali imefanikiwa kujenga vituo vya afya vilivyowezesha akinama 730 kufanyiwa upasuaji hivyo kuokoa maisha yao na watoto wao.
Alisema mbali ya vituo hivyo vya afya serikali imejenga Hospitali tatu za wilaya katika Wilaya za Mkalama, Ikungi na Singida.
" Ndani ya kipindi hicho viwanda zaidi ya 8,500 vimejengwa katika mkoa huu huku tukizalisha ajira milioni sita na kama mtanipa ridhaa ya kuongoza nchi kwa mara nyingine tena tutazalisha ajira milioni 8." alisema Magufuli huku akishangiliwa.
Aidha Magufuli alisema Sh. bilioni 52.6 zimetumika kujenga miundombinu ya shule yakiwemo madarasa, maabara na miundombinu mingine huku
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika na hiyo ni moja ya hatua ya kuboresha sekta ya afya.
Mgombea huyo wa Urais alisema kulikuwa na vijiji 2018 tu vilivyokuwa vimefikishiwa umeme mwaka 2015 lakini katika miaka mitano ya uongozi wake vijiji 9570 vimefikiwa kati ya vijiji 12280 nchi nzima huku sh. bilioni 310 zikitumika kujenga miundombinu wezeshi na sh. bilioni 27.2 zikitumika kutekeleza miradi ya maji ipatayo 66.
Akiongelea uandikishaji wanafunzi umeongezeka kutoka milioni 1 hadi milioni 1.6 baada ya kuanza kwa mpango wa elimu bure.
Magufuli aliongeza kuwa katika kipindi hicho jumla ya sh. bilioni 17 zimetumika kujenga barabara za Singida mjini na kuziwekea taa huku ujenzi wa barabara ya Chaya Singida hadi Tabora ikibakia kilometa tu 20 kukamilika.
Alisema viituo vya afya 487 vimejengwa Tanzania nzima na bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere litakalozalisha megawati 2,115.
Alisema vijiji 9,570 vimefikiwa na nishati ya umeme ikilinganishwa na vijiji 2,018 vilivyokuwa na umeme mwaka 2015.
Alisena katika kipindi hicho bajeti ya Wizara ya Afya imeongezwa kutoka sh. bilioni 30 hadi bilioni 270.
" Niko hapa kwa unyenyekevu mkubwa kuomba kura za vyama vyote kwa sababu maendeleo hayana chama" alisema Magufuli.
Magufuli alisema katika kipindi hicho katika Mkoa wa Singida visima vinne virefu vimechimbwa ili kuongeza upatikanaji wa maji ambapo sh. bilioni 66 zimetumika kutekeleza miradi ya maji na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kutoka asilimia 41 hadi 54.
Alisema mbali ya kutekeleza miradi hiyo ya maji shule kongwe ikiwemo Mwenge Sekondari zimekarabatiwa ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha sekta ya elimu.
Alisema ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa sh. bilioni 850 hadi kufikia zaidi ya sh.Trilioni 1.5 huku Tozo 114 zikifutwa katika sekta ya kilimo na wafanyabiashara ndogondogo wakifutiwa kodi 54.
Alisema Serikali imeweza kukusanya sh Ttrioni1.5-1.9 kwa mwezi ukilinganisha na Bilioni 850 zilizokuwa zikiikusanywa hapo awali.
Akiendelea kuongelea mafanikio ya Seikali kwa kipindi hicho cha miaka mitano alisema kwa mujibu wa ripoti ya "Global Peace Index" Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki, ya 6 Afrika na 52 duniani kwa amani.
Magufuli aliongeza kueleza kuwa ndani ya miaka hiyo mitano mitandao ya simu imeimarika nchi nzima huku waki jenga ukuta wa kilometa 25 eneo la Mererani ambao umesaidia kudhibiti wizi wa madini ya Tanzanite na upotevu wa mapato ya nchi.
Mgombea huyo alimaliza hutuba yake kwa kuwanadi wagombea wote wa nafasi ya ubunge na udiwani wa chama hicho pamoja na kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na janga LA Corona kutokana na maombi tuliyofanya kama taifa na kuwa hiyo imetoa somo kubwa kwa mataifa mengi duniani kuwa Mungu anaweza.