Sunday, January 30, 2022

YAKUBU- VYUO VIKUU ENDELEENI KUANDAA MATAMASHA

 Na. John Mapepele

Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, sanaa na Michezo. Saidi Yakubu ametoa wito  kwa vyuo vikuu nchini vinavyofundisha sanaa kuandaa matamashaa  ya utamaduni ili kuibua vipaji vitakavyoleta ajira kwa vijana.

Yakubu ameyasema  haya  leo  Januari 29, 2022 alipokuwa akimwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed  Mchengerwa wakati wa kilele cha tamasha la  sanaa la kuadhimisha miaka 60 ya Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam toka kuanzishwa kwake.

Amefafanua kwamba matamasha haya yanasaidia kuibua vipaji na kuendeleza utamaduni wa taifa letu.

Aidha, amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa nafasi ya washindi watatu katika tamasha hili kushiriki kwenye tamasha kubwa la kitaifa la Serengeti litakalofanyika  Dodoma mapema mwezi Machi 2022.

Amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa  kuunga  mkono juhudi za Mhe. Rais katika kuendeleza Utamaduni na dira yake ya 2061 na mikakati yake ya kuimarisha utamaduni wa ubunifu ndani ya Chuo.

Ametaja baadhi ya ubunifu  huo kuwa ni pamoja na  kuanzisha kozi zinazodumisha ubunifu na kuchochea  uzalendo  kwa ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Amesema  kuwa utamaduni, sanaa na michezo ni maeneo muhimu katika maisha ya wananchi ambapo amefafanua kuwa faida ya kuenzi utamaduni ni kuwa unatusaidia kutumia ujuzi, taaluma na teknolojia ya jadi na  kisasa katika kuimarisha afya,rasilimali na kuleta tija kwa ujumla.

Katika shindano hilo Rodney Rutashorwa amekuwa mshindi wa kwanza na kujinyakulia shilingi milioni na Yusufu Mkoma akichukua nafasi ya pili na kupata shilingi laki sana na  nafasi ya tatu ikienda kwa Moses Selestine aliyeibuka na kitita cha shilingi la laki tank.



Saturday, January 29, 2022

MBUNGE TAWHEEDA ANOGESHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO MIAKA 45 CCM -UWT WILAYA YA SINGIDA

Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) ambaye alikuwa mgeni rasmi, akizungumza katika Maadhimisho ya miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida DC yaliyofanyika juzi mkoani Singida. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, William Nyalandu.

Mwenyekiti wa  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida DC Neema Sambaa akimvika  vazi la kimila la kabila la Wanyaturu Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) ikiwa ni kumpa heshima wakati wa maadhimisho hayo ambapo pia alikabidhiwa kibuyu cha jadi cha kabila hilo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) (kulia) muda mfupi baada ya kuwasili wilayani Singida DC kwenye maadhimisho hayo.
Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) akizungumza na Wanawake wa UWT Wilaya ya Singida DC.
Burudani zikiendelea na mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo.
Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) akigawa  zawadi kwa watoto. Kulia ni Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida DC Naomi David
Shamra shamra kwenye maadhimisho hayo zikiendelea ambazo zilifanyika sambamba na kumpa zawadimgeni rasmi.
Maadhimisho yakiendelea.
Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) akipanda mche wa mti katika viwanja vya ofisi ya UWT wakati wa maadhimisho hayo.


Na Mwandishi Wetu 


MBUNGE wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) amewataka Wanawake  kufanya kazi kwa bidii  na kwa  kujiamini pamoja na kuondoa dhana ya kwamba wao hawawezi kuongoza kwa kuwa ni mwanamke kwani  mtu yeyote anaweza kuwa kiongozi.

Hayo aliyasema  wakati wa maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyoadhimishwa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Singida (UWT)

Mhe Tawheda alisema kwa sasa nchi yetu inaongozwa na mwanamke na  anatuongoza vizuri sana! Anatimiza hamu na kiu ya watanzania, analiendesha gurudumu la maendeleo vizuri kwa maslahi mapana ya watanzania.  

"Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi makini na mwenye uwezo mkubwa na  ameudhihirishia ulimwengu  kwamba wanawake tunacho kipaji cha kuongoza licha ya kuwa na majukumu  mengi tuliyonayo ya kifamilia lakini tunapokuwa na jukumu la kuongoza tunalifanya kwa ufanisi mkubwa na kuhakikisha malengo yanatimia" alisema Garlos.

Aliwataka Wanawake kuiga mfano wa mhe Rais Samia Suluhu Hassan ambaye  anachapa kazi kwa juhudi na  weledi mkubwa.

Katika maadhimisho hayo  mhe Tawheeda alitembelea Kituo cha Afya cha Ilongero cha Wilaya ya Singida  na kujionea jinsi kinavyotoa huduma pamoja na  kuona changamoto zake na kuahidi kushirikiana na wabunge wa Singida kuzisemea  ambapo pia alipata nafasi ya kuwaona wagonjwa  na kuwapa zawadi  kwa lengo la kuwafariji.

Awali Mbunge Tawheeda alipowasili ofisi za chama alilakiwa na viongozi wa chama wa UWT na Jumuiya ya Wazazi wilayani humo wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo William Nyalandu  na baadaye alipata fursa ya kupanda mti katika ofisi ya chama wilaya   na kuongoza Harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya mtendaji wa chama. 

Miongoni mwa shughuli alizozifanya akiwa wilayani humo ni kugawa kadi kwa wanachama wapya zaidi ya 100 waliojiunga na CCM. 

Maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa  na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mhe.Ramadhani Ighondo na Mhe.Aysharose Mattembe Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.

Viongozi wengine waliokuwepo ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Singida DC, Anthony Katani. Mwenyekiti wa Jumuiya  ya Wazazi Wilaya Singida Alexander Mbogho, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT  Wilaya ya Singida DC Neema Sambaa na Katibu wa UWT wilaya Naomi David.

MCHENGERWA-WASANII KUZOA "MPUNGA" KILA BAADA YA MIEZI SITA

 


 


*****************

Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake kupitia Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) itaanza kugawa mirahaba kwa kazi mbalimbali za wasanii zinazotumika kwenye redio kila baada ya miezi sita ili waweze kunufaika na kazi zao.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa utoaji wa tuzo za muziki na ugawaji wa mirahaba kwa wasanii Januari 28, 2022 kwenye Ukumbi wa kimataifa cha Julius Nyerere. Mhe Mchengerwa amesema Wizara yake inakwenda kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta hizo katika kipindi kifupi kijacho ambapo amewataka watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa kasi na weledi.

Ametoa muda wa wiki tatu kwa watendaji wa Wizara kuandaa App maalum itakayoitwa “sema na Waziri wa Utamaduni “ ambayo itatoa fursa kwa wadau mbalimbali wa sekta ya Sanaa, utamaduni na Michezo kuwasiliana moja kwa moja na yeye pindi wanapotaka kuwasiliana naye badala ya mfumo wa sasa uliozoeleka.

“Naomba niwaahidi hapa kuwa nitakuwa nanyi na milango itakuwa wazi wakati wowote ili kila mmoja wenu mwenye shida aweze kusaidiwa kikamilifu, hii Wizarani kwa ajili yenu inapaswa mfaidike nayo” amesisitiza Mhe. Mchengerwa.

Amelielekeza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhakikisha kuwa linafanya kazi yake ya kukuza, kuendeleza na kuwasaidia wasani wa Tanzania kwa weredi na waache mara moja kufanya kazi kwa mazoea, ambapo amesisitiza kuwa waanzekupanga kwa ajili ya kuandaa tuzo kubwa za kimataifa.

Akizungumzia mchakato wa utoaji wa Tuzo za Muziki ambazo kilele chake kitakuwa Machi 26, 2022 amelitaka BASATA kuhakikisha linatenda haki ya ili kupata kazi zenye kiwango bora.

“Natambua huko nyuma kumekuwa na malalamiko naomba niwaonye, mimim katika kipindi change hakutakuwa na tuzo za msongo”: amesisitiza Mhe Mchengerwa.

Amewashauri wasanii wawe na mazoea ya kujisajiri COSOTA ili kazi zao ziweze kutambulika na waweze kunufaika na kazi hizo.Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Pauline Gekul amesema Sekta za utamaduni, Sanaa na michezo zina umuhimu mkubwa kwa taifa ndiyo maana kiutokana na umuhimu huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Sulkuhu Hassan aliamua kuziundia Wizara hiyo huku akitoa sekta ya habari.

Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikakli imefufua tuzo za muziki baada ya miaka saba kutokuwepo hivyo wadau wa sanaa kwa kushirikiana na Serikali wana wajibu wa kuzilinda na kuzienzi ili ziendelee kuwanufaisha.

Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu amesema sekta ya Sanaa inagusa maisha ya wananchi wote wa Tanzania kwa namna moja au nyingine hivyo Wizara itahakikisha inaandaa mazingira bora ili wasanii waweze kunufaika na kuboresha maisha yao.

Katika tukio hilo Mhe. Mchengerwa amewaongoza mamia ya wadau waliohudhuria hafla hiyo kuimba wimbo wa hongera mwanangu wa Bibi Titi Mohamed huku akifafanua kwamba toka enzi za ukoloni muziki ulitumika katika ukombozi wa Tanzania

CCM SINGIDA YAIPONGEZA WILAYA YA SINGIDA DC KWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo  Kata ya Msange Wilaya ya Singida DC jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC Ester Chaula.
Mwenyekiti wa CCM  Kata ya Msange Joel Ndweti akizungumza kwenye ziara hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida DC. William Nyalandu.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo akizungumza kwenye ziara hiyo Kata ya Msange.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Ester Chaula akichangia jambo wakati akielezea ukarabati wa madara katika Shule ya Msingi Msange.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Eliya Digha akizungumza wakati wa ziara hiyo Kijiji cha Mangida.
Mzee maarufu wa Kata ya Msange Philemoni Mnyawi (kushoto) kwa niaba ya wazee wa kata hiyo akimvika shuka Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida DC. William Nyalandu kama ishara ya heshima ya kimila kwa kabila la Wanyaturu wakati wa ziara
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Alhajj Killimbah akivikwa shuka la heshima.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Idara ya Oganaizesheni Dafroza Lucas akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Jangwa katika ziara hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa  wilaya hiyo wakiwa nyumbani kwa Mzee maarufu wa Ilongero na muasisi wa CCM, Seif Muhomi ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana  kwa ajili ya kutoa rambirambi..


wajumbe wa kamati hiyo ya utekelezaji ya wilaya hiyo wakiwa Shule ya Msingi ya Msange wakati wa ziara hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida DC William Nyalandu akizungumza kwenye ziara hiyo.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Msange Mariam Wela akisoma taarifa ya ukarabati wa madarasa ya shule hiyo.
Muonekano wa madarasa ya Shule ya Msingi Msange baada ya kukarabatiwa.
Zawadi ya mbuzi ikitolewa kwa Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Singida.
Zawadi zikitolewa.
Zawadi zikitolewa.
Zawadi zikitolewa.
Ukaguzi wa madarasa Shule ya Msingi Msange ukuendelea.
Ukaguzi wa vyoo Shule ya Msingi, Jangwa ukiendelea.
Wananchi wa Kijiji cha Jangwa wakiwa kwenye mkutano wakati wa ziara hiyo.
Wananchi wa Kijiji cha Jangwa wakiwa kwenye mkutano wakati wa ziara hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi  Jangwa Jumanne Mangu akisoma taarifa ya shule hiyo wakati wa ziara hiyo.
Mzee Philemoni Mnyawi akionesha furaha yake kabla ya kutoa zawadi kwa baadhi ya viongozi waliokuwepo kwenye ziara hiyo.

Thursday, January 27, 2022

RC SINGIDA AKEMEA MAUAJI YA BODABODA, ATOA MILIONI 2 KWA KIKUNDI CHA VIJANA

Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dk. Binilith Mahenge akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Iguguno Youth Group , Vicky Mwaisakila Sh.2. Milioni alizowaahidi hivi karibu kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali wakati wa ziara ya siku moja ya kukagua ujenzi wa miradi ya barabara wilayani Iramba. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo.
Vijana wa Iguguno Youth Group wakiwa kazini.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATOA TUZO YA KISWAHILI KWA WASHINDI

    


**************************

Na. John Mapepele, WUSM

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa Majaliwa leo Januari 27, 2022 ametoa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati -Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa washindi wa mwaka 2021 jijini Dar es Salaam.

Katika kundi la Riwaya Halfani Sudy ameibuka kuwa mshindi wa kwanza, Mohamed Omary ameibuka mshindi wa kwanza kundi la shairi, wakati Mbwana Kidato ameibuka mshindi wa pili katika kundi la tamthilia na Lukas Lubungo kuwa mshindi wa pili kwenye kundi la hadithi za kubuni.

Amesema dhamira ya Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ya kutekeleza mkakati wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili Kitaifa na Kimataifa, ambao utazinduliwa hivi karibuni itafanikiwa ikiwa wadau wote watajitoa kwa dhati kutekeleza mkakati huu na kusimamia maendeleo ya lugha hii adhimu na aushi.

Mhe. Majaliwa amezipongeza kampuni za SAFAL na ALAF kwa kufadhili tukio hilo na ametoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano huo kwa kuwekeza katika lugha hiyo, huku akisisita kuwa kuwekeza katika Kiswahili itakuwa ni njia mojawapo ya kurudisha fadhila kwa wananchi ambao ndio wateja wa bidhaa hiyo.

Aidha, Mhe Majaliwa amesema Kiswahili kimetambuliwa kimataifa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kutangaza tarehe 7 mwezi Julai, kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani ambapo ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuanza kuandaa wiki ya maadhimisho ya kiswahili katika siku ya mwaka huu.

Naye, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake itashirikiana na wadau mbalimbali kukuza lugha ya kiswahili ili kufika sehemu mbalimbali duniani.

Mhe. Mchengerwa ameelekeza wadau mbalimbali wa lugha ya hiyo kuhakikisha wanaisherekea kwa namna ya pekee siku ya kiswahili ya Julai 7 mwaka huu kwa namna ya kipekee ili kuthibitishia dunia kuwa Tanzania ndiyo chimbuko la lugha hiyo.

Katika halfa hiyo, Waziri Mkuu Mhe Majaliwa na Mhe. Mchengerwa walitumia nafasi hiyo kumtakia heri ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa wimbo wa kiswahili wa heri ya kuzaliwa uliongozwa na Jaji Mkuu wa tuzo hizo Profesa Aldin Mutembei kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salam.

Wednesday, January 26, 2022

RC SINGIDA ATEMBELEA MGODI WA SHANTA GOLD ATAKA USHIRIKIANO

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (mwenye koti la bluu) akiangalia moja ya eneo la machimbo ya dhahabu Mara baada ya kutembelea Kampuni ya Shanta Gold inayoendesha shughuli hizo  katika kijiji Cha Mang'onyi Wilaya ya Ikungi.

RC.Mahenge  akiendelea na ukaguzi wa Mgodi wa machimbo ya dhahabu unaomilikiwa na Kampuni ya Shanta Gold.

Ukaguzi wa mgodi huo ukiendeleaZiara unaendelea
Ukaguzi ukiendelea.
 


Na Mwandishi Wetu, Singida

 

WAWEKEZAJI  mkoani Singida wametakiwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya wakati wa kuanzisha 

miradi ya Maendeleo ya Kijamii  (Community socially responsibility – CSR ) ili kukubaliana aina za miradi na namna itakavyotekelezwa lengo likiwa ni  kuepuka matumizi makubwa ya fedha kwa kazi ambazo zingetumia fedha kidogo.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Dk. Binilith Mahenge leo January 26, 2022 alipotembelea machimbo ya madini ya dhahabu yanayochimbwa na Kampuni ya  Shanta Gold iliyopo Kijiji cha Mang’onyi wilayani Ikungi ambapo alieleza kwamba miradi yote inayoanzishwa na wawekezaji ipitie katika Halmashauri za wilaya ambazo zinafahamu mahitaji ya wahusika na  gharama halisi za ujenzi katika maeneo hayo.

Akitolea mfano kwa madarasa yaliyokamilika hivi karibuni kupitia fedha za uviko 19  Mahenge alisema kila darasa liligharimu kiasi cha Sh.milioni 20, ikilinganishwa na madarasa yaliyojengwa na Shanta Gold ambayo yamegharimu Sh.milioni 28 kwa kila darasa.

“Kama mradi huu mgeshirikisha Halmashauri kwa kiasi kikubwa mngetumia Force Account na mngepata wakandarasi wa bei ndogo na fedha zingebaki zikafanya maendeleo mengine katika jamii. Niwashauri mshirikiane ipasavyo na Halmashauri kupanga aina ya miradi mnayotaka kuipeleka kwa jamii”, alisema Mahenge.

Hata hivyo Mahenge ameipongeza kampuni hiyo ya Shanta Gold  kwa kutumia zaidi ya milioni 190 kwa kupeleka huduma kwa jamii ikiwemo ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na uchimbaji wa visima vya maji huduma ambazo zinafaidisha vijiji vya Mang’onyi, Sambaru, Mlumbi, Tupendane na Mwau.

Aidha, Dkt. Mahenge ameitaka jamii inayozunguka mgodi huo kutumia fursa na kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku na mama lishe pamoja na kuomba ajira katika kampuni hiyo kwa kuwa kadri mradi unavyokuwa ndivyo mahitaji yatakavyoongezeka.

Awali akitoa taairifa ya mgodi Meneja wa mradi huo Kundael Mtiro alisema mpaka kufikia sasa mradi ulitakiwa kufikia asilimia 46.14 katika utekelezaji wake lakini kwa sababu ambazo zimekuwa nje ya uwezo mpaka sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 43.62 .

Hata hivyo Mtiro  akaendelea kufafanua kwamba mpaka Juni,2022 mradi utakuwa unakamilisha  robo ya nne ya mwaka ambapo wanategemea kwamba utakuwa umekamilika kwa kuwa tayari washasimika mabomba katika maeno yote yanayohusika pamoja na uchimbaji wa visima, ujenzi wa ofisi na makazi umekamilika kwa asiliami 80.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Murro alisema mgodi huo utainua uchumi wa Singida na taifa kwa ujumla ambapo utasisimua sekta nyingine za elimu barabara, zahanati na wananchi kupata ajira.

Alisema wilaya imeendelea kusimamia hali ya usalama katika eneo la mradi na imehakikisha wanachi wote waliokuwa wanastahili kupata fidia zao wamelipwa kwa wakati.

YAKUBU- MAANDALIZI YA TUZO YA KISWAHILI YAKAMILIKA

  


**************************

Na. John Mapepele

Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Saidi Yakubu amesema maandalizi ya hafla ya utoaji wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati - Cornell ya Fasihi ya Afrika hapo kesho Januari 27, 2022 jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi yamekamilika.

Akizungumza leo Januari 26, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akikagua ukumbi utakaotumika, Yakubu amekishukuru Chuo Kikuu cha Cornell cha nchini Marekani na kampuni ya Alaf kwa mchango wao wa kutambua na kukuza lugha la Kiswahili kupitia utoaji wa tuzo hizo.

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mkakati wake wa kukikuza Kiswahili duniani.

"Kwa namna ya pekee tunampongeza Mhe. Rais wetu kwa mapenzi yake makubwa ya kukuza Kiswahili ambapo juzi tu akiwa kwenye sherehe na mabalozi amesema Sera ya nje zitazingatia kukuza Kiswahili ."Ameongeza Yakubu.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo anashughulikia Lugha, Dkt. Resani Mnata ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kuenea katika nchi mbalimbali duniani.

Mtaalam anayeratibu tukio hilo la utoaji wa tuzo hizo Mustafa Hassanali amesema tukio hilo limeratibiwa kwa ujuzi wa hali ya juu ili kutoa hadhi inayositahili kwa tuzo hizo

Tuesday, January 25, 2022

RAIS SAMIA AZIDI KUKIPAISHA KISWAHILI DUNIANI

  


**************************

Na John Mapepele

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan amesema Sera mpya ya mambo ya nje itaendelea kuzingatia pamoja na mambo mengine kukuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya kidiplomasia.

Mhe. Rais amesema hayo wakati akizungumza na mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao Januari 24, 2022 hapa nchini pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika sherehe za mwaka mpya 2022 ( Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Rais Samia amewashukuru wote waliopitisha maazimio ya kuifanya tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa siku ya lugha ya Kiswahili duniani.

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itahakikisha inasimamia maendeleo ya Lugha ya Kiswahili kwa faida ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu amefafanua kuwa Kiswahili ni miongoni mwa lugha kubwa duniani ambayo vyuo vikuu, vyombo vya habari na wananchi wa nchi mbalimbali duniani wamekuwa wakitumia katika mawasiliano.

"Lugha ya Kiswahili ni kitu ambacho kitaliletea uchumi mkubwa taifa letu, tumejipanga kuliletea mapato makubwa taifa letu kupitia lugha hii” amesisitiza Yakubu

Ameongeza kuwa kupitia BAKITA mapinduzi makubwa yanakwenda kufanyika ikiwa ni pamoja na kubidhaisha lugha hiyo duniani.“

Monday, January 24, 2022

VIJANA WAHAMASISHWA KUCHANGIA DAMU SALAMA KUOKOA MAISHA

Mkurugenzi wa Chou cha Hermargs na Mlezi wa Rotaract SUA Profesa Robinson Mdegela akitoa neno kwa vijana hao walioshiriki kwenye zoezi la uchangiaji wa Damu kabla ya zoezi hilo kuanza wakati wa kutoa umuhimu wa uchngiaji wa damu.
Mkuu wa Chuo cha Afya Hermargs ambao ni wenyeji wa zoezi hilo Benedict Lubusha akitoa neno la ukaribisho na shukrani kwa vijana hao.
 Vijana kutoka Rotaract SUA na  Hermargs wakichanga damu salama.
Picha namba 9 havijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa k



Vijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kuchangia damu.
Vijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kuchangia damu.
Vijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kuchangia damu.
Vijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kuchangia damu.

 Vijana walioshiriki zoezi la kuchangia damu salama wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kuchangia damu.


Na: Amina Hezron,Morogoro.


KWAKUTAMBUA uhitaji nmkubwa wa dam hasa kwa mkoa wa Morogoro Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA)  na Chuo cha Afya  Hermargs ambao ni wanachama Rotaract wameungana kuchangia damu ili iweze kusaidia kupunguza uhitaji mkubwa wa dam una kusaidia jamii na watu wenye uhitaji.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mlezi wa kikundi cha Rotaract SUA Profesa Robinson Mdegela amesema kuwa mkoa wa Morogoro ni moja ya mikoa mbayo imekuwa ikipokea majuruhi na watu wengi pale zinapotokea ajali kutokana na kuwa katikati na kuunganisha safari za Dar Mwanza,Dar Mbeya na mikoa mingine hivyo kumekuwa na uhitaji mkubwa sana damu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

“Wamefanya kazi nzuri ambayo ni mbegu ya kuzidi kuhamasishana na kusaidiana ili changamoto ya ukosefu wa damu isiendelee kuwepo na vijana Wetu hawa wanawajibu wa kufanya changizo kama walivyofanya siku ya leo ili iwe chachu kwa jamii na vijana wengine lakini pia kutoa mchango wao kwa jamii “, alisema Profesa  Mdegela.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Afya Hermargs ambao ni wenyeji wa zoezi hilo Benedict Lubusha amewashukuru walezi wa vikundi vyote ambavyo vimewezesha kufanyika kwa zoezi zima la uchangiaji wa damu salama itakayosaidia kuokoa maisha ya makundi maalum.


“Tunajua kuwa kila siku ajari zinatokea na tunajua kuwa hakuna sehemu duniani kuna kiwanda cha damu lakini hii damu inatoka kwa binadamu kwahiyo na sisi leo tumefanya uchangiaji wa damu kwaajili ya wenzetu ambao wanauhitaji wa damu”, alisema Lubasha.

Aliongeza “Ukiangalia kwa Mkoa wa Morogoro vyuo vipo vingi  ukichukua kwa haraka haraka jumla tunapata wanafunzi zaidi ya elfu ishirini kwa mfano tukiweza kupata wanafunzi nusu ya hao wakachangia damu tutakuwa tumelisaidia taifa kwakiasi kikubwa kwakuwa huwezi jua lini na wewe utakuwa na uhitaji wa damu”.

Naye mmoja ya wanafunzi waliojitokeza kuchangia damu kutoka SUA, Khatibu Mgunya amewataka vijana kuwa na moyo wa kujitolea kwa kujijengea mazoea ya kwenda kuchangia damu mara kwa mara ili kuepusha vifo vya watoto na wajawazito vinavyotokana na kukosekana kwa damu.

Naye Mwanafunzi wa kazi ya ufamasia Katika chuo cha Hermargs Agneta Lwebangila amewataka vijana wengine kujitokeza kuchangia damu kwakuwa itasaidia kuokoa maisha ya wengine.

“Kuna watu wanaogopa kuchangia damu wakidhani kufanya hivyo kuna madhara yeyote si kweli mimi leo ni mara yangu ya kwanza kuchangia damu na sijapata madhara yeyote nipo salama kabisa hivyo wasiogope tuungane kwa pamoja tuokoe maisha ya wengine kupitia kuwasaidia damu salama”, alisema Agneta.

Kwa upande wake muuguzi na Mratibu wa kitengo cha damu salama kutoka Katika kitengo cha Hospital ya rufaa Mkoa Morogoro Vaileth Mrija amewataka wananchi kuhamasika kuchangia damu ili kuokoa pia maisha ya watoto ambao wa matatizo ya Cell mundu pamoja na magonjwa ya Kansa ambao nao wamekuwa na uhitaji mkubwa wa damu.

“Maahitaji ya Damu kwa siku kwenye hospitali yetu ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ni wastani wa zaidi ya chupa 23 hivyo unaweza kuona uhitaji ulivyo mkubwa na pale kwa bahati mbaya zinapotokea ajali uhitaji huwa mkubwa zaidi kulingana na tatizo lenyewe hivyo tunashukuru vijana hawa kwa kuamua kuchangia damu” alisema Bi Mrija.