Wednesday, August 31, 2022

MSAJILI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI ATEMBELEA JOWUTA

Katibu Mkuu wa JOWUTA Selemani Msuya (kulia) akitoa maelezo kwa Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi nchini, Pendo Berege ambaye ametembelea ofisi za makao makuu ya JOWUTA yaliyopo Chang'ombe Madukani wilayani Temeke jijini Dar es Salaam. 

Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi nchini Pendo Berege akisaini kitabu cha wageni cha JOWUTA alipotembelea ofisini za makao makuu yake.

Friday, August 26, 2022

SINGIDA YAPUNGUZA UDUMAVU WA WATOTO WADOGO KWA ASILIMIA 10


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick (aliyesimama) akichangia jambo katika moja ya mikutano  ya kuhamasisha matumizi ya Lishe bora kwa watoto mkoani hapa.

Lishe bora kwa watoto wadogo ni suluhisho la udumavu kwa jamii kama afanyavyo mama huyu.

Thursday, August 25, 2022

SHEIKH MKOA WA SINGIDA, KATIBU MWENEZI WA CCM WAHESABIWA WATOA KAULI NZITO YA SENSA

Sheikh wa Mkoa wa Singida,Issa Nassoro akihesabiwa na Karani wa Sensa wakati wa zoezi la kuhesabiwa lililofanyika nyumbani kwake eneo la Manguanjuki nje Kidogo ya Manispaa ya Singida jana.
Sheikh wa Mkoa wa Singida,Issa Nassoro, Karani wa Sensa ya Watu wa Makazi akiwa katika picha ya pamoja na familia yake baada ya kuhesabiwa.

Tuesday, August 23, 2022

SENSA YASHIKA KASI SINGIDA, RC ATOA WITO WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA MAKARANI

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba,  akihesabiwa na Karani wa Sensa, Jasmini Kinga katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake Mtaa wa Utemini mkoani hapa leo hii Agosti 23, 2022.
 Karani wa Sensa ya Watu na Makazi, James Rutihinde akijitambulisha kwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko kabla ya zoezi hilo lililofanyika nyumbani kwake mkoani hapa.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri  akihesabiwa na Karani wa Sensa, Peter Samike katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake mkoani hapa leo hii Agosti 23, 2022.

Monday, August 22, 2022

SERIKALI YATOA PIKIPIKI KWA RUWASA, JUMUIYA ZA WATUMIA MAJI SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Peter Serukamba (katikati) akikata utepe kuashiria kuzipokea na kuzigawa pikipiki tisa kwa Jumuiya za Watumia Maji (CBWSOs) na kwa watendaji wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika hafla iliyofanyika leo Agosti 22,2022 katika Ofisi za Bodi ya Maji Bonde la Kati mjini hapa. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Tawala Msaidi anayeshughulikia Uzalishaji na Uchumi Mkoa wa Singida, Stanslaus Choaji, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida, Lucas Said na Afisa Maji Bodi ya Maji Bonde la Kati, Danford Samson.

Pikipili zilizotolewa na Serikali.

DIWANI IRAMBA ALIYEKUFA KWA AJALI AZIKWA NA MAELFU YA WATU, SIRI MABASI KWENDA MWENDO KASI YAFICHUKA


Diwani Winjuka Songelaeli Mkumbo akiwa katika pozi enzi za uhai wake.

Vijana wa Green Gurd wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba mkoani Singida wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa Diwani wa Viti Maalum wa Tarafa ya Kinampanda, Winjuka Songelaeli Mkumbo wakati wakiupeleka kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika Kijiji cha Simbalugwala Kata ya Mukulu jana. Diwani Winjuka alifariki dunia kwa ajali ya gari Agosti 17, 2022 baada ya Basi la Tanzanite lenye namba za usajili T 916 DNU alilokuwa akisafiria kutoka Singida kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka Mlima Saranda uliopo Wilaya ya Manyoni na kusababisha vifo vya watu watano na wengine kujeruhiwa.

Marehemu Winjuka Songalaeli Mkumbo enzi za uhai wake.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakiwa wamejipanga tayari kwa kuelekea ibada ya mazishi ya mwenzao Winjuka Songalieli Mkumbo yaliyofanyika jana Kijiji cha Simbalugwala.

Madiwa hao wakiwa tayari kwa ajili ya ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu wa Kanisa la Assemblies of God Singida Kaskazini, Noel Lameck.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomora akiongoza msafara wa madiwa kwenda kwenye ibada hiyo. 
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa tayari mbele ya eneo maalum ilipofanyika ibada hiyo.
Mme wa marehemu, Winjuka,  John Lyanga akiwa na huzuni kubwa wakati wa ibada hiyo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Mkoa wa Singida, Prisca Maleta anayeishi Manyoni ambaye alishuhudia ajali hiyo akizungumzia tukio hilo
Vijana wa Green Gurd wa CCM wakiwa tayari kwa lolote wakati wa ibada hiyo.
Huzuni wakati wa ibada hiyo.
Mjomba wa marehemu ambaye ni mwanzilishi wa Taasisi ya Ndugu ya Sweden Mzee Amoni Gyunda akifarijiana na baadhi ya ndugu wakati wa ibada hiyo.
Ni huzuni tupu.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ni huzuni tupu ya kuondokewa na mpendwa wao. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Singida, Diana Chilolo na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Gwau.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iramba, Samuel Ashery wakati wa ibada hiyo.
Ibada ikiendelea.
Ni huzuni tupu katika ibada hiyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Mwalimu Ephrahim Kolimba akiwaekeleza masuala ya itifaki vijana wa Green Gurd wakati wa ibada hiyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Mwalimu Ephrahim Kolimba (kulia) akiwa na Katibu Mwenezi wa CCM wa wilaya hiyo, Abbas Michael wakati wa ibada hiyo.
Chakula kikiwa tayari wakati wa ibada hiyo.
Taswira ya ibada hiyo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Iramba ambao walikuwa wakiwezeshwa na marehemu Winjuka kupitia Taasisi ya Ndugu ya Sweden wakiwa kwenye ibada hiyo. Watoto zaidi ya 900 walikuwa wakisaidiwa na taasisi hiyo.
Katibu wa Kanisa la T.A.G Singida Kaskazini,  Mchungaji Danford Mlumba, akisali wakati akiuombea mwili wa marehemu kabla ya kufanyika ibada hiyo.
Waombolezaji wakiwa wamejipanga foleni wakati mwili wa marehemu ukipelekwa kwenye ibada hiyo.
Mwangalizi wa kanisa hilo , Joel Masinsi akiongoza itifaki za ibada hiyo.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) wilayani humo,  Glory Chubwa akiongoza wimbo maalum katika ibada hiyo.
Ibada ikendelea.
Samson Shila akisoma wasifu wa marehemu.
Katibu wa Kanisa la T.A.G Singida Kaskazini,  Mchungaji Danford Mlumba, akizungumza katika  ibada hiyo.

Askofu Noel Lameck akiongoza ibada hiyo.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko, akitoa salama za rambirambi za mkoa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomola akizungumza katika ibada hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akitoa salamu za rambirambi.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Gwau akitoa salamu za rambirambi.
Mbunge wa Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk.Mwigulu Nchemba akitoa salamu za rambirambi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace akitoa salamu za rambirambi.
Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mjomba wa marehemu Mzee Amon Gyunda ambaye ni mwanzilishi wa Taasisi ya Ndugu ya Sweden akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mwanfamilia ya marehemu, Evaline Lyanga, akitoa neno la shukurani.