Saturday, February 27, 2021

TAASISI TA UHASIBU SINGIDA YAZINDUA UMOJA WA WANAFUNZI WA FANI YA UNUNUZI NA UGAVI

Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania  (TIA) Tawi la Singida,  Dkt. James Mrema akisoma taarifa  wakati wa hafla ya kuzindua  rasmi umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi. 

Mwenyekiti wa umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi,  Evarist Peter akisoma taarifa ya umoja huo.

Mgeni  rasmi wa hafla ya kuzindua rasmi umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi  mkoani Singida,  Kaimu Afisa Vijana wa mkoa  huo, Frederick  Ndahani (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali. Kulia ni mkuu wa Taasisi hiyo, Singida na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji  Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Taasisi hiyo nchini,  Godfred Mbanyi  wakifuatilia taarifa ya umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi.


Mlezi wa umoja huo, Mhadhiri Msaidizi, Eliaichi Kyara, akifuatilia hafla hiyo.

Mgeni rasmi akihutubia wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi katika Taasisi hiyo ya Uhasibu Tawi la Singida.

Mgeni rasmi Frederick  Ndahani (Wa pili kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na viongozi.Kulia  ni Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Tawi la Singida, Dkt. James Mrema na wa tatu kutoka kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji  Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Taasisi hiyo nchini, Godfred Mbanyi na kushoto ni Mlezi wa umoja huo, Mhadhiri Msaidizi, Eliaichi Kyara na Afisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU) Mkoa wa Singida, Samson Julius.


Na Dotto Mwaibale, Singida.


TAASISI ya  Uhasibu Tanzania (TIA) Tawi la Singida imefungua rasmi umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi ili kuwaweka pamoja na kutengeneza mahusiano mazuri na bodi ya ununuzi na ugavi (PSPTB)


Akisoma taarifa ya umoja huo wa wanafunzi wanaochukua fani hiyo kabla ya kuzinduliwa Mwenyekiti  wa umoja huo Evarist Peter alisema umoja huo uliundwa tangu mwaka 2017 ambapo unajumuisha vyuo 14 hapa nchini vinavyotoa fani hiyo huku wanafunzi wakiwa 590.

"Tunatarajia kupata mafunzo mbalimbali yatakayo tusaidia kukuza ujuzi wetu wa fani ya ununuzi na ugavi ambapo tunatarajia kuleta wataalamu kutoka maeneo na taasisi mbalimbali ikiwemo bodi yetu ya ununuzi na ugavi na wakala wa ununuzi na ugavi (GPSA) na hii ni kwa maslahi yetu na taifa kwa ujumla." alisema Peter.

Mlezi wa umoja huo, Mhadhiri Msaidizi, Eliaichi Kyara alisema lengo la kuanzishwa kwa umoja huo ni pamoja na kuwawezesha wanafunzi wa fani husika kupata warsha na mafunzo mbalimbali ya ununuzi na ugavi,kuwakutanisha na kuwaweka pamoja wanafunzi wanaochukua fani hiyo hapa nchini,kupata uelewa na kutengeneza mahusiano mazuri na bodi ya ununuzi na ugavi pamoja na kutengeneza fursa ya wanafunzi hao kujiajiri na kuajiriwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi hiyo Tawi la Singida,  Dkt. James Mrema alisema licha ya kuwepo fursa ya chuo hicho mkoani hapo, mwitikio wa wakazi wa mkoa huo ni mdogo kwani wanachuo wengi wanaosoma chuoni hapo wanatoka mikoa mingine.

"Wakazi wa mkoa huu hawachangamkii fursa ya kuwepo taasisi hiyo kwa mamlaka yako tunakuomba uone namna ya kuwahamasisha wazazi ili kuwaleta watoto wao wanaohitimu kidato cha nne na sita nakuomba kwa nafasi yako kuzielekeza halmashauri za mkoa huu kutupatia fursa ya kuendesha mafunzo mbalimbali kwa watumishi wake ili kuwajengea uwezo kwa lengo la kuboresha ufanisi na utendaji wenye tija katika maeneo yao."alisema Mrema.

Akizindua umoja huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Kaimu Afisa Vijana wa Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani aliwaagiza wanafunzi hao kuhamasishana ili wafuate maadili na miiko ya masuala ya ununuzi na ugavi ili wakati wanapopata ajira waweze kuwatumikia watanzania kwa moyo wa kizalendo.

"Bodi ya ununuzi na ugavi endeleeni kuwakumbusha wanafunzi wanaochukua fani hii ili wafuate maadili na miiko mbalimbali ya ununuzi na ugavi awamu hii ya tano kama kuna mtu anafikiri akiajiriwa anaenda kupiga hela hiyo afute nafasi hiyo haipo." alisema na kuongeza.

"Niwaombe wanafunzi kupitia fursa hii mlioipata na mtakapopata ajira serikalini mkasimamie fedha za Serikali,mnao wajibu wa kuisadia jamii kufuata taratibu za manunuzi na ugavi." alisema Ndahani.

Aidha amewaambia kwa kushirikiana na viongozi wa umoja huo atangalia namna na wao kupata nafasi ya kwenda kujifunza masuala ya manunuzi na ugavi katika ofisi ya mkuu wa mkoa ili waendelee kupata uzoefu zaidi wa kivitendo.

Hata hivyo aliwataka wanafunzi hao kubadili fikra kuwa kusoma sio lazima kuajiriwa wanaweza kujiajiri wenyewe kupitia taaluma walioipata,hivyo wafikiri nje ya boksi ili kujikwamua kiuchumi.

"Taaluma ya ununuzi na ugavi ni taaluma muhimu sana kwa familia, jamii na taifa kwa ujumla hivyo mkaanzishe miradi mbalimbali itakayowasaidia kiuchumi..naamini kwa taaluma yenu mtaisimamia vyema miradi hiyo." alisema Ndahani.

NAIBU WAZIRI GEKUL ATEMBELEA KAMPUNI YA TANGA FRESH NA MNADA WA NG’OMBE WA NDEREMA MKOANI TANGA

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul ( wanne kutoka kulia) akiangalia bidhaa mbalimbali za maziwa zinazozalishwa na Kampuni ya Tanga Fresh alipotembelea kukagua shughuli za Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Tanga mapema leo.

Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wapili kulia) walipokutana katika kikao cha Wavuvi na Naibu Waziri huyo kilichofanyika Mkoani Tanga mapema leo lengo la kikao hicho ni kusikiliza kero za Wavuvi wa Mkoani Tanga.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul akikagua risiti aliyopewa mfanyabiashara aliyenunua Ng’ombe katika Mnada wa Nderema uliopo katika Halmashauri ya Mji, Handeni, Mkoani Tanga leo . Naibu Waziri alitembelea mnada huo kukagua shughuli zinazoendelea katika mnada huo.



 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (katikati) akiangalia Ng’ombe waliopelekwa katika Mnada wa Nderema kwa ajili ya kuuzwa. Naibu Waziri alitembelea mnada huo uliopo Katika Halmashauri ya Mji, Handeni, Mkoani Tanga leo  kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika Mnadani hapo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul ( wanne kutoka kulia) akiangalia bidhaa mbalimbali za maziwa zinazozalishwa na Kampuni ya Tanga Fresh alipotembelea kukagua shughuli za Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Tanga mapema leo.

Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wapili kulia) walipokutana katika kikao cha Wavuvi na Naibu Waziri huyo kilichofanyika Mkoani Tanga mapema leo lengo la kikao hicho ni kusikiliza kero za Wavuvi wa Mkoani Tanga.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul akikagua risiti aliyopewa mfanyabiashara aliyenunua Ng’ombe katika Mnada wa Nderema uliopo katika Halmashauri ya Mji, Handeni, Mkoani Tanga leo . Naibu Waziri alitembelea mnada huo kukagua shughuli zinazoendelea katika mnada huo.



 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (katikati) akiangalia Ng’ombe waliopelekwa katika Mnada wa Nderema kwa ajili ya kuuzwa. Naibu Waziri alitembelea mnada huo uliopo Katika Halmashauri ya Mji, Handeni, Mkoani Tanga leo  kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika Mnadani hapo.

Thursday, February 25, 2021

CHUO CHA ABC BIBLE COLLEGE AND TRAINING CENTER CHAFANYA MAHAFALI YAKE YA KWANZA

Mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya Chuo cha ABC Bible College and Training Center kilichopo jijini Dar es Salaam, Askofu Dkt.John   Mwakilema Mkuu  wa Chuo  cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT),  (kulia mbele mwenye joho jekundu) akiongoza maandamano wakati wakiingia kanisani kuanza mahafali hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki. Nyuma yake ni Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing  Center (ABC)   Flaston Ndabila  na kushoto ni Askofu  Mkuu  James Mwaipyana wa Kanisa la Glory  Temple Church  International .


Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Dkt.John   Mwakilema Mkuu  wa Chuo  cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT), akimkabidhi cheti Naomi Mushi mmoa wa wahimu wa  masomo ya kuhudumia jamii hasa watu wanaokuwa katika majanga mbalimbali ikiwemo mafuriko. Kushoto ni  Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing  Center (ABC)   Flaston Ndabila.

Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing  Center (ABC)   Flaston Ndabila, akizungumza kwenye mahafali hayo.

Wakufunzi wa wahitimu hao wakiwa  kwenye mahafali hayo.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Dkt.John   Mwakilema Mkuu  wa Chuo  cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT), akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa ngazi ya cheti wa  masomo ya kuhudumia jamii hasa watu wanaokuwa katika majanga mbalimbali ikiwemo mafuriko.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Dkt.John   Mwakilema Mkuu  wa Chuo  cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT), akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa ngazi ya Diploma ya Theolojia.
Wahitimu wakionesha vyeti vyao.
Wahitimu wa  masomo  ya Theolojia  wakiingia kanisani kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa  masomo ya kuhudumia jamii hasa watu wanaokuwa katika majanga mbalimbali ikiwemo mafuriko wakiingia kanisani kwenye mahafali hayo.

Wahitimu wakiombewa.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Dkt.John   Mwakilema Mkuu  wa Chuo  cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT), akimkabidhi cheti, Dkt. Gad Ndabila.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Dkt.John   Mwakilema Mkuu  wa Chuo  cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT), akimkabidhi cheti Edward Mhoja mmoja wa wahitimu hao.
 


Na Dotto Mwaibale 


CHUO cha ABC Bible College and Training Center kilichopo jijini Dar es Salaam kimefanya mahafali yake ya  kwanza   kwa kutoa  wahitimu 20.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika  mahafali hayo Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing  Center (ABC)   Flaston Ndabila alisema kuwa Chuo hicho ni chuo kishiriki cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT)C

Alisema chuo hicho kinatoa Certificate na Diploma ya Theology na Certficate ya masomo ya kuhudumia jamii hasa watu wanaokuwa katika majanga mbalimbali ikiwemo mafuriko na kuwaelimisha juu ya kanuni bora za afya yao yaani Community Health Worker kwa kushirikiana na Bright Fature Ministries (U.S.A)

"Chuo chetu kinatumia darasa lililopo katika kanisa letu hapa Mtaa wa  Mandela Tabata wakati huu tukiendelea  na ujenzi wa  chuo kilichopo Manispaa ya  Ilala eneo la Kinyerezi kwa Makofia."alisema Ndabila.

Ndabila alisema chuo hicho  kina matawi katika  Mkoa wa Morogoro ambacho kwenye  mahafali hayo kimetoa wahitimu wawili na tawi la Kibaha ambao wametoa wahitimu watano na kuwa matawi hayo  yanafundisha mwisho kiwango cha cheti.

Aidha Ndabila alisema kuwa masomo ya chuo hicho yalianza rasmi Novemba 5, 2019 na jumla ya wahitimu wakiwa ni 43,  ngazi ya    diploma  wakihitimu 18, Community Health Worker wakiwa 20 na Certificate 7.

Ndabila alitumia nafasi hiyo kumshukuru Askofu Dkt.John   Mwakilema Mkuu  wa Chuo cha  Zoe  kwa kutoa mkono wa  shirika  na kutoa maelekezo maalumu  ya  somo la jinsi ya kuweka mikakati.

"Nitumie nafasi hii kuwashukuru walimu wote kwa  muda wao wa   kufundisha ambao ni Askofu Oreliani Ngonyani, Mchungaji Benjamin Mwalilino, Mwalimu Michael, walimu wa matawi ya Kibaha na Morogoro na Madam Tamari Shunda  (U.S.A) kwa kuwesha darasa la Community Healthy Worker pamoja na Dkt. Barnabas (MD) na Dkt.Gad Ndabila (MD) kwa kufundisha vyema."alisema Ndabila.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo Askofu Dkt.John   Mwakilema alisema kuwa nyakati  hizi kuna umuhimu mkubwa kwa wachungaji kusoma na kuwa wabobevu wa masuala mbalimbali  na si kujikita katika eneo moja tu la Theolojia jambo litakalo saidia kuleta mabadiliko chanya ya kiroho na maendeleo ya kiuchumi kwa waumini wao na kanisa kwa ujumla.

Katika mahafali hayo viongozi mbalimbali wa Serikali ya mtaa wa Mandela lilipo kanisa hilo waliudhuria wakiwepo Askofu  Mkuu  James Mwaipyana wa Kanisa la Glory  Temple Church  International,  Askofu Sedrick Ndonde Katibu  Mkuu  wa Kanisa la Restoration Bible Church na Apostle John Kazidi wa Kanisa la Messiah Pentecoste Church  ambao walikuwa wanenaji.

Wednesday, February 24, 2021

WAZIRI MKUU AZINDUA MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI SINGIDA

 

WAZIRI
anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Singida kulia ni Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na katikati ni Katibu Tawala wa
Mkoa wa Singida Angelina Lutambi

 

WAZIRI anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Singida kulia ni Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na katikati ni Katibu Tawala wa
Mkoa wa Singida Angelina Lutambi

Kikundi cha Ngoma Asili cha Sarakasi wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo huo

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi mwenye kilemba cheupe akishiriki kucheza ngoma ya asilina wadau mbalimbali



WAZIRI wa Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikagua baadhi bidhaa zilizoletwa na wadau mbalimbali

Kwaya ya Chuo cha Utumishi Singida wakitumbuiza wakati wa tukio hilo
Na John Mapepele, Singida

Waziri
kuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassimu Majaliwa 
amezitaka  Mamlaka zote za Mikoa  kujipanga kikamilifu kutangaza fursa
za uwekezaji zinapatikana kwenye  mikoa yao kwa kushirikiana Kituo cha 
Taifa  cha Uwezekezaji  ili kuhakikisha kuwa fursa zote zilizoainishwa
kwenye  miongozo ya  uwekezaji  zinapata wawekezaji makini ili kuongeza 
mapato na ajira kwa wananchi

 Akisoma  hotuba  ya Mheshimiwa
Waziri Mkuu kwenye  tukio la uzinduzi wa Mwongozo wa Fursa za Uwekezaji
Mkoa wa Singida,   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji Profesa Kitila
Mkumbo amesema kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo  wa miaka  mitano(5)
Serikali imedhamilia  kuimarisha  ustawi wa wananchi wake  kwa kuzalisha
ajira  milioni nane na kukuza uchumi wake kwa asilimia nane  hivyo
uwekezaji  makini unatakiwa ili kufanikisha azma hiyo.

Amesema 
ili kuwapata wawekezaji makaini watendaji wote wa Serikali hawana budi
kutoa taarifa sahihi za fursa zinazopatikana  katika maeneo yao na
utaratibu wote wa namna ya  kuufuata ili kuweza kuwekeza.

“Ndugu
zangu ni muhimu sana tubadilike  taarifa za uwekekezaji tunazozitoa
ziwe  sahihi na ziwe zinafanana, ukienda kwa Mkuu wa  Mkoa upate taarifa
sawa na ukichukua taarifa hiyo kwa  Katibu Tawala wa Mkoa na Mkurugenzi
Mtendaji wa  Halmashauri hapo tutakuwa tumefanikiwa” amesisitiza
Profesa Mkumbo.

Amezitaka  mamlaka hizo kutowakwamisha 
wawekezaji kwa  kuhakikisha  maeneo ya uwekezaji  yanapatikana mara moja
ili pindi Wawekezaji wanapofika wanapatiwa   maeneo hayo na
wanahudumiwa  kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto zozote
zinazojitokeza.

Amesema  balozi  namba moja  anayeweza kuleta au
kutoleta wawekezazi katika nchi yoyote  duniani ni Muwekezaji aliye
ndani ya nchi husika  hivyo  ni muhimu  kuwapa huduma  bora  ili waweze
kutuletea wawekezaji wengi zaidi ambapo amesisitiza  uwekezaji ufanywe
kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya  Serikali ili nchi yetu
iweze kunufaika.

Amekemea tabia  ya kupenda kutoa lawama  baada
ya  kuingia mikataba  mibovu na wawekezaji na badala yake amewataka 
watendaji kuwa makini katika  mchakato mzima wa majadiliano na kufunga
mikataba hiyo na wawekezaji.

Aidha, ameitaka  kila Mkoa kuangalia
kuangalia maeneo  machache ya kipekee ili kufanya uwekezaji  wenye tija
badala ya kwenda na maeneo mengi ambayo  hayana  tija.

Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais John Pombe
Magufuli kwa kubuni mikkakati  kabambe ya uwekezaji ambayotayari katika
kipindi kifupi imeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii kwenye
nchi yetu.

Amesema Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa ambayo
ilikuwa ikionekana kama  mikoa masikini lakini sasa  umekuwa  ni
miongoni mwa mikoa ambayo inaweza kuongoza  kuleta  mapato makubwa kwa
nchi  kutokana na  kuboreshwa kwa  mazingira na fursa nyingi zilizopo.

Ametaja
baadhi ya fursa za uwekezaji  zinazopatikana kuwa ni pamoja na madini,
kilimo  cha Alizeti na Korosho, mafuta asilina na gesi pia elimu.

GEKUL AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA KITUO CHA UKAGUZI WA MIFUGO RUVU DARAJANI

Msimamizi  wa Ujenzi wa Bwawa la Kunyweshea Mifugo la Chamakweza, Robert Baltazar akimuonesha michoro ya bwawa hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wa kwanza kulia) alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa hilo lililopo Chalinze, Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani Februari 24, 2021. Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarist Ndikilo. 

    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia) alipofanya ziara kukagua Kituo cha Ukaguzi wa Mifugo cha Ruvu Darajani kilichopo Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani jana.
    Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Rogers Shengoto akijibu moja ya hoja ziliyoibuliwa katika ziara ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul aliyoifanya Mkoani Pwani. 

     


    Na Mbaraka Kambona, Pwani

     

    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul amemsimamisha kazi Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Mifugo cha Ruvu Darajani, Gabriel Lyakurwa kwa tuhuma za kutorosha mifugo na kusababisha upotevu wa mapato ya Serikali, huku akimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarist Ndikilo kuwachukulia hatua Watumishi waliochini ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ambao walikuwa wanashirikiana na Mkuu huyo wa kituo.   

    Gekul alitoa maamuzi hayo baada ya Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani kuibua tuhuma hizo katika ziara yake aliyoifanya kwenye kituo hicho kilichopo Ruvu Darajani, Wilayani Bagamoyo jana. 

    Mhandisi Ndikilo alisema uchunguzi alioufanya umebaini kuwa Mkuu wa kituo hicho amekuwa akishirikiana na wenzake wasiowaaminifu kutorosha mifugo inayopelekwa katika kituo hicho kwa ajili ya kukaguliwa kabla ya kuruhusiwa kupelekwa katika maeneo mengine ya minada. 

    “Mhe. Naibu Waziri nimefanya uchunguzi wa kina na kugundua kuwa utoroshaji huu unahusisha mtandao wa watu wengi wakiwemo baadhi ya Wananchi, Wafanyabiashara na Watumishi wa Serikali…, kwa mfano tarehe 17 mwezi huu wa pili kuna Magari matano yalileta ng’ombe katika kituo hiki kwa ajili ya kukaguliwa lakini ni gari moja tu lililokwenda Dar es Salaam kama kawaida ilivyo, huku mengine yaliyobaki yakichepushwa na mifugo ilipelekwa Kisarawe, Kibaha na Kijiji cha Kidogozero kinyemela,” alisema Mhandisi Ndikilo. 

    Kufuatia tuhuma hizo, Naibu Waziri Gekul alitoa maagizo hayo ya kusimamishwa kazi mkuu huyo wa kituo huku akisema kuwa Wizara itaunda tume maalum kwa ajili ya kwenda kuchunguza tuhuma hizo ikiwemo kupitia mahesabu yote ili kubaini ni kwa kiasi gani mapato ya Serikali yamepotea na wale wote watakaoonekana kuhusika katika upotevu huo watachukuliwa hatua kali. 

    "Hatuwezi kucheza na maduhuli ya Serikali, haiwezekani tuwe na ng’ombe zaidi ya milioni 33 lakini mchango wa sekta ya mifugo katika pato la taifa hauzidi asilimia 7, ni kwa sababu ya michezo kama hii, hatutakubali, na tutakwenda kukagua katika maeneo yote ya minada," alisema Gekul. 

    Naye, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete alisema kuwa katika jambo ambalo wamekuwa wakilisemea sana ni kituo hicho kukithiri kwa vitendo vya ubadhilifu ambavyo vimekuwa vikichangia Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kupoteza mapato. 

    Ridhiwani alimuomba Naibu Waziri huyo kuhakikisha anachukua hatua madhubuti za kudhibiti vitendo hivyo vya ubadhirifu ikiwemo kuondoa mtandao wote wa waharifu ili halmashauri iweze kupata mapato yanayostahili.

    Monday, February 22, 2021

    DC IKUNGI AIAGIZA HALMASHAURI KUWAACHIA WANANCHI MASHAMBA YA KUPANDA KOROSHO

    Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,  Edward Mpogolo (kushoto) akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Ulyampiti na Mwau katika eneo lenye mgogoro.

    Wananchi wa Vijiji vya Ulyampiti na Mwau wakiwa katika eneo lenye mgogoro.


    Na Dotto Mwaibale, Singida


    MKUU wa Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Edward Mpogolo ameagiza Halmashauri  kuwaachia mashamba yao wananchi zaidi ya 36 ambayo walimpa mkulima mmoja mgeni bila ya kufuata utaratibu ili apande korosho.

    Katika hatua nyingine Mpogolo ameiagiza halmashauri ya kijiji  na Idara ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kumpatia eneo lingine mkulima huyo ili aweze kuliandaa na kuanzisha kilimo hicho badala ya kuyachukua mashamba ya wananchi hao waliyo yaendeleza na kupanda mazao ya chakula.

    Mpogolo amechukua hatua hiyo baada ya kutokea mgogoro wa kugombea mashamba baada ya mkulima mgeni kupewa mashamba ya wananchi waliyoyafyeka na kuyatumia kwa kilimo.

    Mpogolo alisema kama halmashauri imetenga eneo hilo kwa kilimo cha korosho ni vyema na wananchi hao wakawezeshwa na wao kunufaika na zao hilo la korosho badala ya kuwafukuza.

    Vijiji vilivyokuwa na mgogoro huo ni Ulyampiti na Mwau huku kila upande ukiomba kuangaliwa upya wa mipaka ya maeneo yao ya ardhi.

    Mpogolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo lililotengwa na Halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo cha zao la korosho.

    Aidha mkuu huyo wa wilaya  alisisitiza  kwamba kutokana na mgogoro wa mipaka uliopo katika eneo hilo ni marufuku kwa viongozi wa serikali za vijiji hivyo kuendelea kukata na kugawa maeneo kwa wananchi au wawekezaji wenye ni ya kulima zao hilo la kibiashara bila kufuata taratibu.

    “Sasa ndugu zangu pambaneni mlime, wewe ambaye hujapalilia nenda ukapalilie usije ukauwa watoto lakini kwenda kujikatia maeneo  mengine wenyewe ni marufuku kwa sababu kuna mgogoro kwenye maeneo  ya mipaka." alisema Mpogolo. 

    Mpogolo alitaja mkulima huyo mgeni aliyepewa ekari 300 kwenye maeneo ya wananchi kutoziendeleza kutokana na  mgogoro uliyopo.

    Hata hivyo Mpogolo alitumia fursa hiyo pia kuuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi kwa kushirikiana na kamati za watu Tisa za ugawaji ardhi na usuluhishi migogoro kutoka katika vijiji vya Mwau na Ulyampiti na kuunda kamati ya kushughulikia mgogoro wa mpaka wa vijiji hivyo. Alisema wakati zoezi hilo likiendelea wananchi kwa upande wao wataendelea na shughuli za kilimo kwenye maeneo yao waliyokuwa wakiyatumia awali.

    “Sasa katika kipindi hiki natoa maagizo kwanza kwa mtaalamu  ardhi wa Wilaya kwa kwa kushirikiana na Halmashauri za vijiji vyote viwili mtatengeneza kamati jumuishi na wajumbe tisa kutoka katika kila kijiji kushughulikia mipaka.

    Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye eneo lenye mgogoro wa mipaka baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mwau, walisema kwamba mgogoro huo wa mpaka umetokana na uongozi wa Kijiji cha Ulyampiti kugawa eneo kwa wageni bila kuushirikisha uongozi wa Kijiji cha Mwau.

    “Kwa sababu migongano ya mipaka siyo la hapa tu bali wengi  tunagongana kwa sababu ya kutoshirikishana, sasa mimi nakuomba mheshimiwa DC kwa kuwa leo umekanyaga ardhi hii tupe uamuzi kama si watu wa Ulyampiti utuambie kama ni wa Mwau we angalia mwenyewe Ulyampiti mpaka uko wapi na Mwau vile vile? alihoji kwa Shabani  Kijanga.

    DC IKUNGI AIAGIZA HALMASHAURI KUWAACHIA WANANCHI MASHAMBA YA KUPANDA KOROSHO

    Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,  Edward Mpogolo.


    Na Dotto Mwaibale, Singida


    MKUU wa Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Edward Mpogolo ameagiza Halmashauri  kuwaachia mashamba yao wananchi zaidi ya 36 ambayo walimpa mkulima mmoja mgeni bila ya kufuata utaratibu ili apande korosho.

    Katika hatua nyingine Mpogolo ameiagiza halmashauri ya kijiji  na Idara ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kumpatia eneo lingine mkulima huyo ili aweze kuliandaa na kuanzisha kilimo hicho badala ya kuyachukua mashamba ya wananchi hao waliyo yaendeleza na kupanda mazao ya chakula.

    Mpogolo amechukua hatua hiyo baada ya kutokea mgogoro wa kugombea mashamba baada ya mkulima mgeni kupewa mashamba ya wananchi waliyoyafyeka na kuyatumia kwa kilimo.

    Mpogolo alisema kama halmashauri imetenga eneo hilo kwa kilimo cha korosho ni vyema na wananchi hao wakawezeshwa na wao kunufaika na zao hilo la korosho badala ya kuwafukuza.

    Vijiji vilivyokuwa na mgogoro huo ni Ulyampiti na Mwau huku kila upande ukiomba kuangaliwa upya wa mipaka ya maeneo yao ya ardhi.

    Mpogolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo lililotengwa na Halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo cha zao la korosho.

    Aidha mkuu huyo wa wilaya  alisisitiza  kwamba kutokana na mgogoro wa mipaka uliopo katika eneo hilo ni marufuku kwa viongozi wa serikali za vijiji hivyo kuendelea kukata na kugawa maeneo kwa wananchi au wawekezaji wenye ni ya kulima zao hilo la kibiashara bila kufuata taratibu.

    “Sasa ndugu zangu pambaneni mlime, wewe ambaye hujapalilia nenda ukapalilie usije ukauwa watoto lakini kwenda kujikatia maeneo  mengine wenyewe ni marufuku kwa sababu kuna mgogoro kwenye maeneo  ya mipaka." alisema Mpogolo. 

    Mpogolo alitaja mkulima huyo mgeni aliyepewa ekari 300 kwenye maeneo ya wananchi kutoziendeleza kutokana na  mgogoro uliyopo.

    Hata hivyo Mpogolo alitumia fursa hiyo pia kuuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi kwa kushirikiana na kamati za watu Tisa za ugawaji ardhi na usuluhishi migogoro kutoka katika vijiji vya Mwau na Ulyampiti na kuunda kamati ya kushughulikia mgogoro wa mpaka wa vijiji hivyo. Alisema wakati zoezi hilo likiendelea wananchi kwa upande wao wataendelea na shughuli za kilimo kwenye maeneo yao waliyokuwa wakiyatumia awali.

    “Sasa katika kipindi hiki natoa maagizo kwanza kwa mtaalamu  ardhi wa Wilaya kwa kwa kushirikiana na Halmashauri za vijiji vyote viwili mtatengeneza kamati jumuishi na wajumbe tisa kutoka katika kila kijiji kushughulikia mipaka.

    Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye eneo lenye mgogoro wa mipaka baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mwau, walisema kwamba mgogoro huo wa mpaka umetokana na uongozi wa Kijiji cha Ulyampiti kugawa eneo kwa wageni bila kuushirikisha uongozi wa Kijiji cha Mwau.

    “Kwa sababu migongano ya mipaka siyo la hapa tu bali wengi  tunagongana kwa sababu ya kutoshirikishana, sasa mimi nakuomba mheshimiwa DC kwa kuwa leo umekanyaga ardhi hii tupe uamuzi kama si watu wa Ulyampiti utuambie kama ni wa Mwau we angalia mwenyewe Ulyampiti mpaka uko wapi na Mwau vile vile? alihoji kwa Shabani  Kijanga.

    Sunday, February 21, 2021

    KIMIMBI HERBAL CLINIC YAIOMBA NIMR KURUHUSU DAWA YA COVID 19

    Mkurugenzi Mtendaji wa Kimimbi Herbal Clinic inayojishughulisha na utengenezaji wa dawa za asili, Kafana Mussa  akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kiwalani jijini Dar es Salaam jana.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Kimimbi Herbal Clinic inayojishughulisha na utengenezaji wa dawa za asili, Kafana Mussa (kushoto) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kiwalani jijini Dar es Salaam jana.
    Ofisi ya   Kimimbi Herbal Clinic iliyopo Kiwalani jijini Dar es Salaam.

     Kipeperushi kinacho onesha magonjwa yanayotibiwa na dawa hiyo.



    Na Dotto Mwaibale


    KIMIMBI Herbal Clinic inayojishughulisha na utengenezaji wa dawa za asili imeiomba Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kuruhusu dawa ya Kafana 20 inayotibu ugonjwa wa Corona ili iwasaidie wananchi.

    Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Clinic hiyo Kafana Mussa wakati akizungumza   na waandishi wa habari ofisini kwake Kiwalani jijini Dar es Salaam jana.

    "Ombi letu kubwa kwa NIMR ni kuruhusu dawa yetu hii ili kuwasaidia wananchi katika kipindi hiki cha ugonjwa wa   Covid-19" alisema Kafana.

    Alisema mara baada ya kugundulika  kwa ugonjwa huo nchini China wao kama watafiti walichukua jukumu la kufanya utafiti na kutengeneza dawa yao ya kwanza ya kutibu ugonjwa huo ambayo waliipa jina la Kafana 20.

    Alisema walianza kuifanyia majaribio yasio rasmi kwa watu waliokuwa na viashiria vya ugonjwa huo na kuonesha mafanikio makubwa.

    Mussa alisema April 10, 2020 waliandika barua kwenda Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ili kupata kibali ambapo waliambiwa waende NIMR.

    Alisema baada ya kufika NIMR walitakiwa kueleza namna walivyotengeneza dawa hiyo ambayo ilitumia sampuri ya miti aina tano. 

    " Baada ya kutoa maelezo hayo na kuifanyia utafiti wao walituambia dawa hiyo hawataweza kuitoa kwa sababu miti iliyotumika kutengeneza ni mingi hivyo itawawia vigumu kuipata na kutengeneza dawa nyingi vinginevyo wamtafute mwekezaji mkubwa ambaye atapanda aina ya miti hiyo kwa wingi ili waingie naye ubia wa kutengeneza dawa hiyo." alisema Mussa.

    Mussa alisema jambo lingine waliloelezwa ni kuwa licha ya wao kuitengeneza wanao paswa kuitoa dawa hiyo ni NIMR kwa maana Serikali ambayo itachukua asilimia 90 ya fedha za mauzo na wao watachukua asilimia 10 tu.

    Mkurugenzi huyo Kafana Mussa ameiomba Serikali kuruhusu dawa hiyo ili kusaidia wananchi katika kipindi hiki cha Covid-19 kama ambavyo Rais Dkt.John Magufuli  amekuwa akihimiza  kufanya maombI pamoja na kutumia dawa za asili na kujifukiza ikiwa na kuchukua hatua zote za kujikinga na ugonjwa huo.

    Mussa alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi ambao watakuwa na viashiria vya ugonjwa huo kuwasiliana na Clinic hiyo kwa namba za simu 0743068792 na 0674456789 kwa msaada wa kitabibu.

    Friday, February 19, 2021

    TALIRI YAJIKITA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFUGAJI NCHINI

     

    Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima (katikati- aliyevaa suti nyeusi) akijadiliana jambo na baadhi ya Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Maafisa wengine wa kituo cha TALIRI Mpwapwa alipotembelea kituo hicho jana.

    Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima (katikati- aliyevaa suti nyeusi) akijadiliana jambo na baadhi ya Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Maafisa wengine wa kituo cha TALIRI Mpwapwa alipotembelea kituo hicho jana.
    Baadhi ya Ng'ombe wanaofugwa katika kituo cha TALIRI Mpwapwa kilichopo Wilayani Mpwapwa wakinywa maji katika kisima kilichotengwa kando ya Josho la Nunge kwa ajili ya kunyweshea mifugo.
    Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani, Dkt. Angello Mwilawa akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani)  kuhusu utafiti wa malisho unaofanywa na Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Mpwapwa kilichopo Wilayani Mpwapwa alipotembelea   moja ya Shamba la Malisho ya mifugo la kituo hicho jana. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Utafiti na Mafunzo, Dkt. Hassan Mruttu.

     


    Na Mbaraka Kambona, Mpwapwa

     

    Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima amesema utafiti wanaoufanya umejikita katika kutatua changamoto za mbegu bora za mifugo na mbegu bora za malisho kwa wafugaji ili sekta ya mifugo iweze kuchangia vyema katika pato la Taifa. 

    Dkt. Kizima aliyasema hayo alipotembelea kukagua shughuli zinazofanywa na Kituo cha TALIRI Mpwapwa kilichopo Wilayani Mpwapwa, Mkoani Dodoma jana. 

    Alisema kuwa lengo la utafiti wanaoufanya ni kuhakikisha wanapata mbegu bora za mifugo na kuzalisha mbego bora za malisho ya mifugo ambazo zitakazosaidia kutatua changamoto za upatikanaji wa mbegu bora za mifugo zinazohimili mazingira yaliyopo na malisho inayoikabili nchi kwa sasa. 

    Aliongeza kuwa kwa sasa taasisi hiyo inaendelea na kufanya Tathmini ya ubora, ustahimilivu na makuzi ya malisho ya mifugo yatakayofaa kwa chakula cha kutosha kwa ajili ya mifugo. 

    Kwa mujibu wa Dkt. Kizima, matokeo yoyote ya utafiti lazima yabadilishwe kuwa biashara kwa sababu wafugaji wakifanya ufugaji unaoendana na mazingira yao itawasaidia kutengeneza uchumi na kuwaongezea tija katika ufugaji wao. 

    “Tafiti tunazozifanya zinalenga kuimarisha mnyororo wa thamani wa mifugo ili mchango wa sekta ya mifugo uweze kuonekana katika uchumi wa kati,” alisema Dkt. Kizima. 

    Dkt. Kizima alisema kuwa TALIRI imesambaza vituo vyake katika Kanda Saba nchini ili kuwa karibu na wafugaji kuwasaidia kutatua changamoto zao ili waweze kufanya ufugaji wenye tija. 

    Alisema vituo hivyo vipo katika Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kati, Kanda ya Kusini, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. 

    Naye, Mkurugenzi, Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani, Dkt. Angello Mwilawa alisema kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imezihamasisha Halmashauri zote nchini kuanzisha mashamba darasa ya malisho ili wafugaji waweze kujifunza na kupata mbegu bora za malisho kwa ajili ya mifugo. 

    “Tunawahimiza wafugaji kuona umuhimu wa kulima malisho ili yaweze kuwasaidia kupata lishe ya uhakika kwa mifugo yao na pia kwa kulima malisho kutawapunguzia migogoro ya mara kwa mara kati yao na wakulima,” alisema Dkt. Mwilawa. 

    Aliongeza kuwa wanawahamasisha wafugaji hususan walio katika nyanda kame wastawishe malisho ya mifugo wakati wa masika na kuyatunza ili yaweze kuwasaidia kulisha mifugo yao wakati wa kiangazi.

    Thursday, February 18, 2021

    WANAMUZIKI KUKUTANA KESHO HOTELI YA MOUNT MERU JIJINI ARUSHA

    Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa.

    Katibu Mkuu wa wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), , Stella Joel.
    Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Dofa kutoka Karatu ambao wataimba wimbo maalumu kwenye kongamano hilo.



    Na Dotto Mwaibale


    WANAMUZIKI watakutana  kesho katika kongamano la fursa litakalofanyika Hoteli ya Mont Meru  jijini Arusha.

    Mgeni  rasmi  katika kongamano hilo  anatarajiwa  kuwa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ambaye atawakabidhi baadhi ya wanamuziki kadi za bima ya afya ya Taifa (NHIF).

      "Wanamuziki watakao pata kadi hizo ni wale ambao wametimiza vigezo kama walivyoeleza Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Eric Kisanga na Katibu Mkuu wa umoja huo, Stella Joel ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo.

    Baadhi ya wanamuziki maarufu watakao kuwepo kwenye kongamano hilo ni Emanuel Mbasha (Dsm) Stara Thomas (Dsm) Hafsa kazinja, Rehema Tajiri (Dsm) Edson Mwasabwite (Dsm) 6. Emanuel Mabisa (Dsm)  Rajabu Samatta (Dsm) Goodluck Gozbert (Dsm) Ann Annie (Moshi) Kida Waziri, Agness Lukumay (Karatu) Angel Tango (Mwanza) JCB Makala (Arusha) Renatha Sedekia (Arusha) na Andrew Mnzava (Moshi)

    Akiwazungumzia Wanamuziki hao Katibu Mkuu wa TAMiUFO Stella Joel alisema wanaishukuru Serikali kwa kuwakumbuka kuwapatia kadi hizo ambazo zitawasaidia kupata vipimo na matibabu katika hospitali za Serikali na binafsi.

    Joel alisema kabla ya hapo wanamuziki wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa kushindwa kumudu gharama za vipimo na matibabu.

    " Kwa hatua hii iliyochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano hakika wanamuziki wote tunakila sababu ya kuipongeza  kwa kutekeleza ahadi yake kwa vitendo ya kutusaidia wasanii" alisema Joel.

    Rais wa TAMUFO,  Eric Kisanga alisema kongamano hilo ni la kipekee kwani litawahusisha wanamuziki wa kada zote  na kuwa maandalizi yote yamekwisha kamilika.

    " Maandalizi yote ya kongamano letu ili la fursa kwa wanamuziki yamekwisha kamilika kwa asilimia kubwa na sasa tupo kumalizia mambo madogo yaliyosalia" alisema Kisanga.

    Kisanga alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi na wadau wengine kwenye kongamano hilo.