Posts

Showing posts from October, 2020

CCM SINGIDA KUIBUKA NA USHINDI WA KISHINDO

Image
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dodoma baada ya kuhitimisha kampeni zake za uchaguzi  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Hassan Kilimba akiwa katika moja ya mikutano ya kampeni Tarafa ya Makiungu mkoani hapa.   Na Godwin Myovela, Singida MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa Alhaji Juma Hassan Kilimba amesema kwa idadi ya kura zote zitakazopigwa kwa nafasi ya Udiwani, Ubunge na Rais, chama hicho kinatarajia kuibuka na ushindi wa asilimia 83.75 Akitoa ufafanuzi mbele ya vyombo vya habari jana, Kilimba alisema kwa kuanza na madiwani CCM ilisimamisha viti vyote 136, na kati ya hivyo viti 35 vilipita bila kupingwa hatua iliyokifanya chama hicho kubaki kikishindania viti 101 vya nafasi hiyo pekee. Kilimba alisema kwa upande wa Ubunge walifanikiwa kusimamisha wagombea wote 8 kwa idadi ya majimbo yaliyopo, na katika siku zote 60 za Kampeni, kuanzia Septemba walipoanza m...

TAKUKURU SINGIDA YAOKOA SH.MILIONI 33.5 ZA WASTAAFU

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi (kushoto) akimkabidhi juzi Mwalimu Mstaafu kutoka Wilaya ya Singida  Amosi Njoghomi kiasi cha shilingi milioni 18.8 zilizookolewa kutoka kwa mmoja wa wakopeshaji wa ‘Riba Umiza.’ Mwalimu Njoghomi alikopa shilingi milioni 2, lakini mkopeshaji alimtaka arejeshe fedha taslimu shilingi milioni 31 hadi serikali ilipoingilia kati na kumsaidia.   Na Edina Alex, Singida  TAASISI  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imeokoa sh.milioni 33.5 walizokopeshwa watumishi wa umma wastaafu na makampuni ya kukopesha fedha zenye riba kubwa maarufu kama mikopo umiza bila ya kufuata sheria. Akitoa taarifa ya utekelezaji huo juzi  Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida,  Adili Elinipenda  alisema operesheni hiyo wameifanya kufuatia agizo la mkuu wa mkoa huo la kuwatokomeza wakopeshaji haramu  ambao wamekuwa wanawakandamiza  wananchi  hasa watumishi wa umma  wanao karibia kustaafu.  ...

MARAIS WASTAAFU WAOMBWA KUMSHAURI RAIS MAGUFULI KUTUVUSHA SALAMA UCHAGUZI MKUU UTAKAO ANZA KESHO

Image
Askofu Kiongozi wa Kanisa la  Abundant Blessing Centre (ABC) lililopo Tabata Mandela jijini Dar e Salaam, Flaston Ndabila (kulia) akiongoza maombi maalumu ya kuiombea nchi kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho. Askofu Kiongozi wa Kanisa la  Abundant Blessing Centre (ABC) lililopo Tabata Mandela jijini Dar e Salaam, Flaston Ndabila (kulia) akiongoza maombi hayo maalumu. Muumini wa kanisa hilo, Mariam Luvanda akiombea nchi amani katika maombi hayo. Maombi yakiendelea. Muumini wa kanisa hilo Daniel Hezron Mpemba akiomba kwa hisia kali katika maombi hayo. Mama Askofu, Janeth Ndabila akiomba kwenye maombi hayo.  Maombi yakiendelea. Mzee Gerald Enock akiomba huku akililia amani ya nchi isipotee wakati huu wa mchakato wa kupiga kura. Maombi yakiendelea. Maombi yakiendelea. Waumini wa kanisa hilo wakiomba huku wakililia amani isipotee wakati wa kupiga kura. Maombi yakiendelea. Katibu wa kanisa hilo, Jane Magigita  (kushoto) akiomba katika maombi hayo. Kulia n Muumini wa...

SERIKALI YA JPM YAZIBANA KAMPUNI ZINAZOUMIZA WATUMISHI NA WASTAAFU KWA KUTOZA RIBA KUBWA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida (RC) Dkt Rehema Nchimbi akimkabidhi Mwalimu Mstaafu kutoka Wilaya ya Singida   A mosi Njoghomi kiasi cha shilingi milioni 18.8 zilizookolewa kutoka kwa mmoja wa wakopeshaji wa ‘Riba Umiza.’ Mwalimu Njoghomi alikopa shilingi milioni 2, lakini mkopeshaji alimtaka arejeshe fedha taslimu shilingi milioni 31 hadi serikali ilipoingilia kati na kumsaidia.  Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Singida, Suzan Shesha (kulia) akishuhudia tukio la Mwalimu Njoghomi kukabidhiwa pesa zilizookolewa. Kushoto ni Mwenyekiti Mstaafu wa CWT mkoa wa Singida, Aran Jumbe. Familia ya Mwalimu Mstaafu Albert Mpahi ikipokea kiasi cha shilingi milioni 2 zilizookolewa kutoka kwa moja ya Kampuni za Mikopo zisizofuata utaratibu. Mwalimu Mpahi alikopa shilingi milioni 7.2 na mkopeshaji wake akamtaka arejeshe fedha taslimu Shilingi Milioni 17 hadi serikali ilipoingilia kati. RC Nchimbi akimkabidhi Mwalimu Mstaafu kutoka Wilaya ya Ikungi  Gerase Mshumbusi kiasi cha shilingi mili...

WANAOISHI MLIMA ULUGURU KUFUNDISHWA MBINU ZA KUENDELEA KUISHI HUKO BILA KUSHUSHWA.

Image
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manispaa ya Morogoro, Fikiri Juma  ( kulia) akiwa na Mgombea Udiwani, Juma Kiduka kwenye mkutano wa kampeni wa lalasalama uliofanyika kwenye Mtaa wa Folkland mjini Morogoro juzi Wananchi wa Kata ya Magadu wakifuatilia mkutano huo wa kampeni wa kumnadi mgombea Udiwani wa Kata hiyo bwana Juma Kiduka. Wananchi wa Kata ya Magadu wakifuatilia mkutano huo. Wananchi wa Kata ya Magadu wakifuatilia mkutano huo Mkutano ukiendelea.   Na Calvin Gwabara, Morogoro. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma amewahakikishia wananchi wanaoishi kwenye mlima Uluguru kuwa hawatashushwa bali watafundishwa njia na mbinu bora za kuishi milimani kama wanavyofanya watu wa Lushoto na kwingine duniani. Fikiri aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni ya udiwani kwenye Kata ya Magadu ambayo sehemu ya jamii ya watu wa kata hiyo wanaishi kwenye mlima Uluguru na kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji. “ Tumezielekeza Taasisi mbalimbali ...

KILIMO SHADIDI CHA MPUNGA KUONGEZA TIJA KWA WAKULIMA NCHINI.

Image
Dkt. Devotha Kilave Mtafiti akiwasilisha matokeo ya utafiti wa Kilimo Shadidi cha Mpunga mbele ya waandishi wa habari. Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia uwasilishwaji wa matokeo hayo ya utafiti ili wayafikishe kwa jamii. Waandishi wa habari wakochukua vipeperushi na machapisho mbalimbali ya matokeo ya Tafiti zilizofanhwa na Mradi wa APRA Tanzania. Mkuu wa Mradi wa APRA Tanzania Profesa. Aida Isinika akichangia neno kwenye uwasilishwaji wa matokeo ya utafiti wa Kilimo Shadidi cha mpunga uliowasioishwa na Dkt. Devotha Kilave. Waandishi wa habari wakifuatilia uwasilishwaji wa matokeo hayo ya utafiti wa Mradi wa APRA Mkoani Morogoro kwenye ukumbi wa ICE - SUA. Mwandishi wa habari wa Gazeti ka the Citizen Jacob Mosenda akiuliza swali kwa watafiti ili kupata ufafanuzi zaidi. Waandishi wa habari wakifuatilia uwasilishwaji wa matokeo hayo ya utafiti wa Mradi wa APRA Mkoani Morogoro kwenye ukumbi wa ICE - SUA.   Na Calvin Gwabara, Morogoro WATAFITI...

SINGIDA YATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI BIASHARA USAFIRISHAJI BINADAMU

Image
Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Seperatus Fella, akiweka mkakati wa namna bora ya kukabiliana na biashara hiyo, alipokutana na wadau mbalimbali kwenye mafunzo maalumu mkoani Singida juzi. Afisa wa Sekretarieti hiyo, Ahmad Said Mwen-dadi, akitoa mada kwenye mafunzo hayo. wa Sekretarieti hiyo, Alex Lupilya akitoa mada kwenye mafunzo hayo. Picha ya Pamoja ya baadhi ya wadau walioshiriki mafunzo hayo.   Na Godwin Myovela, Singida WAKAZI mkoani hapa wametakiwa kuwa makini kabla ya kuwaruhusu mabinti kuchukuliwa na kupelekwa maeneo mbalimbali nchini kwa kigezo cha kutafutiwa au kufanya kazi za ndani, badala yake wahakikishe kwanza wanahusisha uongozi wa Serikali ya Mtaa husika ili mchakato huo ufanyike kihalali. Pia ‘dalali’ au mtu yeyote anayetaka kumchukua binti yako hakikisha anakuwa na mdhamini wa kuwezesha kurahisisha   mawasiliano ya mara kwa mara, lengo hasa ni kuwa na uhakika wa mazingira ya usalama wa mwanao ...

ASKOFU FLASTON NDABILA AOMBA AMANI SIKU YA KUPIGA KURA

Image
Askofu Kiongozi wa Kanisa la  Abundant Blessing Centre (ABC) lililopo Tabata Mandela jijini Dar e Salaam, Flaston Ndabila (kulia) akiongoza maombi maalumu ya kuiombea nchi kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 28, 2020. Muumini wa kanisa hilo, Mariam Luvanda akiombea nchi amani katika maombi hayo. Mama Askofu, Janeth Ndabila akiomba kwenye maombi hayo.  Maombi yakiendelea. Mzee Gerald Enock akiomba huku akililia amani ya nchi isipotee wakati huu wa mchakato wa kupiga kura. Maombi yakiendelea. Muumini wa kanisa hilo Daniel Hezron Mpemba akiomba kwa hisia kali katika maombi hayo. Waumini wa kanisa hilo wakiomba huku wakililia amani isipotee wakati wa kupiga kura. Maombi yakiendelea. Maombi yakiendelea. Maombi yakiendelea. Na Dotto Mwaibale WANANCHI nchini wametakiwa kuilinda amani siku ya kupiga kura na kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuwachagua viongozi wanaowataka. Ombi hilo linetolewa jana na Askofu Kiongozi wa Kanisa la  Abundant Blessing Centre (ABC) l...