Posts

Showing posts from December, 2020

KANISA LA ABC LAWAKUMBUKA WAJANE, WAGANE KRISMAS

Image
Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC) la Mtaa wa Mandela jijini Dar es Salaam, Flaston Ndabila (katikati) akikabidhi juzi msaada wa chakula na vitu vingine kwa Wagane na Wajane. Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC) la Mtaa wa Mandela jijini Dar es Salaam, Flaston Ndabila akikabidhi juzi msaada wa vifaa vya shule kwa watoto wenye uhitaji.Kulia ni mke wake Janeth Ndabila. Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC) la Mtaa wa Mandela jijini Dar es Salaam, Flaston Ndabila akikabidhi juzi msaada wa vifaa vya shule kwa watoto wenye uhitaji.Kulia ni Mke wake Janeth Ndabila. Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC) la Mtaa wa Mandela jijini Dar es Salaam, Flaston Ndabila akikabidhi juzi msaada wa chakula kwa Nasaba  Seifu. Mgane Hussein Libe akishukuru baada ya kupokea msaada huo. umbe wa Serikali ya mtaa wa Mandela, Leonard  Chalema na Tabrisa Bushiri  Wajane wakiondoka katika kanisa hilo baada ya k...

NDAHANI AWATAKA WAZAZI KUWAPA WATOTO WAO MLO KAMILI

Image
Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani, akikabidhi vyeti  katika Mahafali ya Elimu ya Awali ambapo alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi jana. Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani, akikabidhi vyeti. Mtoto akionesha cheti baada ya kukabidhiwa. Mkuu wa Shule hiyo Sister Malietha, akisoma risara katika mahafali hayo. Picha ya pamoja na mgeni rasmi. Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani, akihutubia katika mahafali hayo.   Na Dotto Mwaibale, Singida KAIMU Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani amewataka wazazi na walezi kujenga tabia ya kuwapa watoto wao mlo kamili  badala ya chipsi. Ndahani alitoa ombi hilo jana katika mahafali ya Elimu ya Awali ambapo alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi. "Nawaombeni wazazi na walezi waleeni watoto katika maadili mema, mkizingatia mlo kamili  kuliko kuwapa chipsi" alisema Ndahani. Aidha Ndahani aliwaambia wazazi hao wajenge tabia ya kuwashiri...

GEKUL AONYA WANAOJIHUSISHA UVUVI HARAMU, UKWEPAJI KODI

Image
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti alipomtembelea ofisini kwake jana.Waziri Gekul yupo mkoani Manyara kwa ziara ya Kikazi. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (kushoto) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Ukuzaji Viumbe Maji, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Imani Kapinga alipokuwa akimpa maelekezo Mwakilishi wa Kampuni ya XIN SI LU,  Suvi Zeng (katikati) alipotembelea eneo la ufugaji wa Samaki katika Mabwawa la Kampuni hiyo jana. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (kulia) akipokea samaki aina Sato kutoka kwa Mkurugenzi, Idara ya Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Magese Bulayi alipotembelea  eneo la   Kampuni ya XIN SI LU kutoka China iliyowekeza katika ufugaji wa Samaki kwenye Mabwawa Mkoani Manyara jana.   Na Mbaraka Kambona, Manyara   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul amewataka wale wote wanaojihusisha na uvuvi usiozingatia sheria na ...

TAKUKURU SINGIDA YAZIDI KUWABANA WAKOPESHAJI HARAMU, NDANI YA MIEZI MITATU YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 80

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi, akimbidhi Sh.milioni 8,600,000, Esther Pununta (wa pili kushoto) mbele ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Manispaa ya Singida, mkoani hapa juzi, akiwa ni mmoja wa waathirika waliopitiwa na wimbi  la  ‘Mikopo Umiza,’ ambazo ziliokolewa na Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Singida. Kushoto ni mtoto wake Naomy Geuza. Wa tatu kutoka kulia ni Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda, Wengine ni Mstahiki Meya Yagi Kiaratu na Naibu Meya, Hassan Mkata. Muathirika wa Mikopo Umiza  Mwalimu Mstaafu Seleman Haji, akimkabidhi shilingi milioni 46 mke wake Magdalena Gunda baada ya kukabidhiwa na  Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dk .Rehema Nchimbi,  Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dk. Rehema Nchimbi, akizungumza na Wajumbe  wa Baraza la Madiwani la Manispaa ya Singida (hawapo pichani) baada ya kukabidhi fedha hizo. Muathirika wa Mikopo Umiza  Loth Mwangu,  akiwa na fedha...

KATIBU WA TAMUFO STELLA JOEL ATOA WIMBO KUHAMASISHA MAENDELEO

Image
Mwimbaji wa Muziki wa Injili Nchini Tanzania na  Katibu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) , Stella Joel akiwa katika muonekano wa picha tofauti baada ya kuachia wimbo wa kuhamasisha maendeleo unaoitwa Tanzania ya Maendeleo.  Stella Joel akiwa katika pozi.  Stella Joel akitafakari ukuu wa Mungu baada ya kutoa wimbo huo ambao unabamba hivi sasa hapa nchini. Na Dotto Mwaibale BAADA ya kimya cha muda mrefu, Mwimbaji wa Muziki wa Injili Nchini Tanzania, Stella Joel ameachia wimbo wa kuhamasisha maendeleo unaoitwa Tanzania ya Maendeleo. Mara ya mwisho Stella aliachia wimbo wa Hakuna Mwanamke mbaya alioshirikiana na malkia wa muziki wa Injili, Rose Muhando. Stella ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) alisema, imefika hatua kwa wasanii kuhamasisha nyimbo zinazochochea maendeleo na kuisaidia jamii kutatua changamoto zake. “Baada ya Tanzania kufikia uchumi wa kati nikaona ni vyema niweke hilo kwenye muziki, nyimbo za aina hii zinachangia sana kupiga hatu...

BAKWATA SINGIDA YAPONGEZA UJENZI WA SHULE

Image
Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Buruan Mlau akihutubia  kwenye Mahafali ya Shule ya Awali ya Al Wafaa inayo milikiwa na Taasisi ya Dhi Nureyn iliyopo eneo la Mandewa yaliyofanyika jana mkoani hapa. Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Buruan Mlau akikabidhi vyeti kwenye Mahafali ya Shule ya Awali ya Al Wafaa inayo milikiwa na Taasisi ya Dhi Nureyn iliyopo eneo la Mandewa yaliyofanyika jana mkoani hapa. Kutoka kulia ni Sheikh wa Wilaya ya Singida, Issa  Simba, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mikidadi Abrahman na kushoto ni mmiliki wa shule hiyo, Hamisi Ntandu, Wanafunzi wakiwa kwenye mahafali hayo. Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Buruan Mlau akikabidhi vitabu kwenye Mahafali hayo. Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Buruan Mlau akikabidhi vitabu kwenye Mahafali hayo. Wanafunzi wakiwa na vitabu walivyo kabidhiwa baada ya k...

WADAU WAKUTANA KUTATHIMINI UTEKELEZAJI WA MRADI WA SWIOFish

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah  akitoa maelezo ya tathmini ya maendeleo ya Mradi wa SWIOFish kwa Uongozi wa Benki ya Dunia kupitia njia ya mtandao katika kikao cha kufanya tathmini kilichofanyika jana mjini Dodoma. Afisa Uvuvi Mwandamizi, Upendo Hamidu akifafanua jambo katika kikao hicho. Sehemu ya Wajumbe kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Taasisi zinazotekeleza Mradi wa SWIOFish Tanzania Bara na Visiwani pamoja na Mamlaka ya Bahari Kuu wakiwa katika majadiliano na viongozi wa Benki ya Dunia kwa njia ya mtandao kuhusu kufanya tathmini ya mradi huo, Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah. Na Mwandishi Wetu, Dodoma. TAASISI zinazohusika na utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) wamekutana kujadili na kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo wa miaka sita (6) ili kupima mafanikio na mapungufu yaliyojitokeza kabla ya kufanya ma...

RC NCHIMBI: WAZAZI MSIWE MBALI NA VIJANA KIPINDI HIKI BAADA YA MITIHANI

Image
Kaimu Afisa Vijana wa Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani akihutubia mahafali ya 10 ya Shule ya Sekondari Utaho iliyopo wilaya ya Ikungi, mkoani Singida jana. Mwonekano wa kisima hicho ambacho hakijaanza kufanya kazi kutokana na kukosa mabomba ya kusambazia maji Mkuu wa shule ya Sekondari Utaho, Mwavita Malagila, akizungumza kwenye mahafali hayo. Wanafunzi wakiingia kwenye viwanja vya shule hiyo kabla ya kuanza mahafali hayo Maandamano kuelekea kwenye viwanja kabla ya kuanza kwa sherehe za mahafali hayo. Kulia ni Mkuu wa shule ya Sekondari Utaho, Mwavita Malagila Meza kuu ikishiriki kuimba wimbo wa Taifa Wanafunzi wakiimba wimbo wa uzalendo kabla ya mahafali hayo Wahitimu wakiingia kwenye viwanja vya shule hiyo kabla ya kuanza mahafali hayo. Ndahani akikagua moja ya visima vilivyochimbwa kwa umahiri mkubwa ndani ya shamba la mwekezaji huyo kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa maji kwa jamii inayozunguka maeneo hayo. Embe zilizotokana na shamba hilo lililopo eneo la Utaho Mwenyekiti wa B...