Posts

Showing posts from January, 2021

STARA THOMAS, HAFSA KAZINJA KUKABIDHIWA KADI ZA MATIBABU NA WAZIRI BASHUNGWA

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa.  Wanamuziki Stara Thomas na Hafsa Kazinja wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Eric Kisanga (kushoto) na Katibu Mkuu wa umoja huo, Stella Joel  (kulia) baada ya kufanya mazungumzo jijini Arusha juzi kuhusu Kongamano la Fursa kwa wanamuziki litakalofanyika Februari  20, 2021 Jijini humo.   Na Dotto Mwaibale. WANAMUZIKI Maarufu  Nchini Stara Thomas na Hafsa Kazinja ni miongoni mwa baadhi ya wanamuziki watakao pata kadi za bima ya afya ya Taifa (NHIF) zitakazotolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa. Bashungwa ambaye atakuwa mgeni rasmi atatoa kadi hizo katika Kongamano la Fursa kwa wanamuziki litakalofanyika Februari  20, 2021 Jijini Arusha.   "Mastaa hawa Stara Thomas na Hafsa Kazinja tayari wametimiza vigezo vya kupata kadi hizo za bima ya afya baada ya  kukutana na Rais wa Umoja wa Wanamuzi...

WAZIRI BASHUNGWA KUPOKELEWA KWA WIMBO MAALUMU KONGAMANO LA WANAMUZIKI

Image
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Dofa kilichopo Karatu mkoani Arusha wakifanya mazoezi ya  wimbo maalumu watakao muimbia Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa  wakati wa kumpokea katika  kongamano la wanamuziki. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) Stella Joel.   Na Dotto Mwaibale WASANII wa Kikundi cha Sanaa cha Dofa kilichopo Karatu mkoani Arusha wanatarajia kumpokea Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa kwa wimbo maalumu katika kongamano la wanamuziki. Bashungwa atakuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo la Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) litakalofanyika Februari 20, 2021 jijini Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel alisema hivi sasa kikundi hicho kipo katika mazoezi ya wimbo huo maalumu kwa ajili ya kumpokea Waziri Bashungwa. " Waziri Bashungwa anakuja kwenye ...

KAMISHNA WA SKAUTI MKOA WA MBEYA AFANYA ZIARA WILAYANI

Image
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Skauta Sadock Ntole  (wa pili kulia) akisalimiana na  Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kitta alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Godfrey Kawacha, Kamishna wa Skauti Wilaya ya Kyela, Skauta Scholastica Msigwa. na kulia ni Kamishna Msaidizi wa Skauti Wilaya ya Kyela, Skauta Ayubu Mwambete. Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Skauta Sadock Ntole, akisalimiana na  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyasa English Medium, Mika Alinanuswe. Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Skauta Sadock Ntole, akisalimiana na  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Keneth  Nsilano. Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Skauta Sadock Ntole, akisalimiana na Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Kyela, Leah  Katamba. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Skauti Wilaya ya Kyela, Skauta Ayubu Mwambete. Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Skauta Sadock Ntole, akisalimiana na Mkuu wa Kikosi cha Zi...

TAKUKURU SINGIDA YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 270

Image
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda (katikati) akitoa taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha miezi mitatu Oktoba hadi Disemba 2020 mkoani hapa juzi.  Na Dotto Mwaibale, Singida TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imeokoa zaidi ya shilingi 270.7 kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo mikopo umiza. Akitoa taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha miezi mitatu Oktoba hadi Disemba 2020 Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoani hapa Adili Elinipenda alisema Takukuru imeokoa shilingi milioni 270,079,600 ndani ya kipindi hicho kutoka maeneo mbalimbali. Elinipenda alisema shilingi milioni 154,416,000 pekee zimeokolewa kutoka mikopo umiza, shilingi milioni 28,000,000 ziliokolewa kutokana na fidia ya maeneo ya wananchi yaliyotwaliwa kufanya shughuli za uchimbaji madini Wilayani Mkalama,wakati kiasi kingine kikiokolewa kutoka maeneo mengine ikiwemo mahakama ya Manyoni. "Fedha hizi tulizikabidhi kwa wahusika baada ya kuokolewa...

RC NCHIMBI AWATAFAKARISHA WATENDAJI WA MAHAKAMA YA MIAKA 100, AAGIZA TAKUKURU KUANZA KUWAMULIKA “BUSH LAWYERS”

Image
Mkuu waMkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akihutubia kwenye sherehe zamaadhimisho ya uzinduzi wa wiki ya sheria, kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi juzi. Nchimbi akiwa na viongozi mbalimbali w amahakama na serikali kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Luhaula akizungumza kwenye uzinduzi huo. Dkt Rehema Nchimbi akihutubia kwenye sherehe za maadhimisho ya uzinduzi wa wiki ya sheria mwaka huu, kwenye viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida. Mkuu wa Mkoa akitembelea moja ya banda la wadau wa mahakama linalojishughulisha na kazi za usaidizi wa msaada wa kisheria wilaya ya Singida. Akiwa kwenyebanda la Jeshi la Magereza. Akiwa kwenye banda la Watumishi wa Mahakama. Baadhi ya Watumishi na Mahakimu wa Wilaya ya Iramba wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzihuo Wananchi kutoka Taasisi na Asasi mbalimbali wakishiriki maadhimisho hayo Mada mbalimbali zikiwasilishwa. Sherehe zauzinduzi zikiendelea.   Na Godwin Myovela, Singida MKUU waMkoawaS...

WAZIRI BASHUNGWA KUTOA KADI ZA MATIBABU KWA WANAMUZIKI

Image
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Stella Joel.   Na Dotto Mwaibale WAZIRIa wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) litakalofanyika Februari 13, 2021 jijini Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel alisema pamoja na mambo mengine Bashungwa atatoa  kadi za Bima ya Afya ya NHIF kwa Wanamuziki pamoja na kusikiliza changamoto zao mbalimbali ili kuzipatia ufumbuzi. "Serikali imetukumbuka wanamuziki kwa kutupatia kadi za bima ya afya ya Taifa kwa gharama nafuu kupitia Tanzania Music Foundation (TAMUFO) jambo litakalo tusaidia wanamuziki kupata matibabu." alisema Joel.  Joel aliwataja baadhi ya wanamuziki watakao kabidhiwa kadi hizo kuwa ni wa muziki wa Injili, bongo fleva, dansi, taarabu na ngoma za asili.  Aidha Joel alisema kitendo...

SKAUTI JIJINI MBEYA WAKARABATI MAENEO YALIYO ATHIRIWA NA MAFURIKO

Image
Vijana wa Chama cha Skauti Mkoa wa Mbeya wakikarabati kivuko cha watembea kwa miguu  katika Mtaa wa Mayombo Kata ya Iwambi baada ya kuharibiwa na mafuriko. Vijana wa Chama cha Skauti Mkoa wa Mbeya wakiwajibika. Vijana wa Chama cha Skauti Mkoa wa Mbeya wakisafisha mitaro Kazi ikiendelea. Kazi ikiendelea.   Na Dotto Mwaibale  KUTOKANA  na mvua zinazo endelea kunyesha Mkoa  wa Mbeya na kuharibu miundombinu ya barabara Chama cha Skauti mkoani humo kimeendelea kutoa huduma ya kukarabati miundombinu hiyo kwa wathirika wa mafuriko. Akizungumza na waandishi wa habari juzi Kamishna wa Skauti  Mkoa wa Mbeya, Sadock Ntole alisema  mvua iliyonyesha Januari 23 mwaka huu ilileta athari kubwa kSatika Kata ya Iwambi na kuharibu miundombinu mbalimbali. Alisema kufuata hali hiyo walikaa na kuratibu namna ya kufika katika maeneo hayo kutoa msaada ambapo kikosi cha uokoaji cha skauti wapatao 16 walikwenda kutoa huduma ya kusafisha  mitaro na makaravati.   "...

SERIKALI YASHAURIWA KUFUFUA SHULE ZA UFUNDI NCHINI

Image
Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (wa pili kushoto) akizungumza na Walimu wa Ufundi  wa Shule ya Msingi Makiungua iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida alipoitembelea juzi kwa lengo la kukagua uwezeshwaji mafunzo na ujuzi kwa vijana. Madawati yakitengenezwa. na Shule ya Msingi Makiungu iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida. Madawati yaliyotengenezwa. Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (kulia) akikagua utengenezaji wa madawati. Madawati yaliyotengenezwa.   Na Dotto Mwaibale, Singida. KAIMU Afisa Vijana mkoani hapa,  Frederick Ndahani ameishauri Serikali kufufua Shule za Msingi za ufundi Nchini.   Ndahani alitoa ushauri huo juzi alipotembelea  Shule ya Msingi Makiungu iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida kwa lengo la kukagua uwezeshwaji mafunzo na ujuzi kwa vijana. Ndahani alisema Shule ya Msingi Makiungu ni moja ya shule zilizofanya  vizuri katika ...

WADAU WA TIBA ASILI WATAKIWA KUCHANGAMKIA SOKO LA DAWA ZAO KIMATAIFA

Image
   Mkurugenzi msaidizi wa tiba asili na tiba mbadala kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt. Paul Mhame akitoa hotuba ya uzinduzi wa jukwaa hili. Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA upande wa utawala na fedha Prof. Amandus Mhairwa akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua rasmi jukwaa. Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akitia neno kwa wagana hao wa tiba asili na wadau wengine wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo. Mkuu wa mradi huo wa GRILI Dkt. Faitha Mabiki akieleza kwa kifupia majukumua na malengo ya mradi huo wa GRILI na yale ambayo yamefanyika toka mradi uanzishwe.     Wadau wa tiba sili na tiba mbadala kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wakifuatilia hotuba na maneno ya uzunduzi wa Jukwaa lao kutoka kwa viongozi. Na Calvin Gwabara,   Morogoro. Wataalamu wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wametakiwa kushirikiana na wataalamu wa tiba asili na taasisi zingine katika kufanya ta...

NGURUWE WENYE THAMANI YA MIL. 370 WAMEKUFA KWA HOMA, SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KUDHIBITI

Image
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kudhibiti ugonjwa wa homa ya Nguruwe kwenye Mkutano uliofanyika jijini Dodoma juzi.   Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Hezron Nonga (kushoto) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ugonjwa wa homa ya Nguruwe katika Mkutano uliofanyika jijini Dodoma juzi. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki. Na Mbaraka Kambona,   Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha ugonjwa wa homa ya Nguruwe ulioikumba Mikoa ya Kanda ya Ziwa hivi karibuni unadhibitiwa, huku akisema kuwa tangu ugonjwa huo uanze mpaka sasa umeshasababisha vifo vya Nguruwe 1500 wenye thamani ya shilingi milioni 375.   Ndaki aliyasema hayo juzi jijini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali...

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WATAFITI KUBORESHA TIBA ASILI NCHINI

Image
1.      Mratibu wa Tiba asili Mkoa wa Morogoro Dkt. Ngalula Wille akizungumza katika uzinduzi wa Maonesho ya siku moja ya wadau wa tiba asili na bidhaa zake yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa niaba ya  Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Amandus Mhairwa,  akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua maonesho hayo kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda. 1.      Muwakilishi wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma,  Prof. Samweli Kabote akitoa shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya hutuba yake ya ufunguzi, Mkuu wa Mradi wa GRILI, Dkt. Faith Mabiki ambao ndio waandaaji wa maonesho akieleza malengo ya maonesho hayo na uzinduzi wa jukwaa la Ubunifu wa Tiba Asili Tanzania. Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na viongozi wa meza kuu mara baada ya kufungua maonesho hayo. Mgeni rasmi na ujumbe aliofuatana nao wakitembelea mabanda ya maonesho ya...