Posts

Showing posts from February, 2021

TAASISI TA UHASIBU SINGIDA YAZINDUA UMOJA WA WANAFUNZI WA FANI YA UNUNUZI NA UGAVI

Image
Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania  (TIA) Tawi la Singida,  Dkt. James Mrema akisoma taarifa  wakati wa hafla ya kuzindua  rasmi umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi.  Mwenyekiti wa umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi,  Evarist Peter akisoma taarifa ya umoja huo. Mgeni  rasmi wa hafla ya kuzindua rasmi umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi  mkoani Singida,  Kaimu Afisa Vijana wa mkoa  huo, Frederick  Ndahani (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali. Kulia ni mkuu wa Taasisi hiyo, Singida na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji  Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Taasisi hiyo nchini,  Godfred Mbanyi  wakifuatilia taarifa ya umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi. Mlezi wa umoja huo, Mhadhiri Msaidizi, Eliaichi Kyara, akifuatilia hafla hiyo. Mgeni rasmi akihutubia wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi katika Taasisi hiyo ya Uhasibu Tawi la Singid...

NAIBU WAZIRI GEKUL ATEMBELEA KAMPUNI YA TANGA FRESH NA MNADA WA NG’OMBE WA NDEREMA MKOANI TANGA

Image
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul ( wanne kutoka kulia) akiangalia bidhaa mbalimbali za maziwa zinazozalishwa na Kampuni ya Tanga Fresh alipotembelea kukagua shughuli za Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Tanga mapema leo. Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wapili kulia) walipokutana katika kikao cha Wavuvi na Naibu Waziri huyo kilichofanyika Mkoani Tanga mapema leo lengo la kikao hicho ni kusikiliza kero za Wavuvi wa Mkoani Tanga. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul akikagua risiti aliyopewa mfanyabiashara aliyenunua Ng’ombe katika Mnada wa Nderema uliopo katika Halmashauri ya Mji, Handeni, Mkoani Tanga leo . Naibu Waziri alitembelea mnada huo kukagua shughuli zinazoendelea katika mnada huo.  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (katikati) akiangalia Ng’ombe waliopelekwa katika Mnada wa Nderema kwa ajili ya kuuzwa. Naibu Waziri alitembelea mnada huo ulio...

CHUO CHA ABC BIBLE COLLEGE AND TRAINING CENTER CHAFANYA MAHAFALI YAKE YA KWANZA

Image
Mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya Chuo cha ABC Bible College and Training Center kilichopo jijini Dar es Salaam, Askofu Dkt.John   Mwakilema Mkuu  wa Chuo  cha Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT),  (kulia mbele mwenye joho jekundu) akiongoza maandamano wakati wakiingia kanisani kuanza mahafali hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki. Nyuma yake ni Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant Blessing  Center (ABC)   Flaston Ndabila  na kushoto ni Askofu  Mkuu  James Mwaipyana wa Kanisa la Glory  Temple Church  International . Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Dkt.John   Mwakilema Mkuu  wa Chuo  cha  Zoe Institute of Apostolic Testmony and Seminary (ZIAT), akimkabidhi cheti Naomi Mushi mmoa wa wahimu wa    masomo ya kuhudumia jamii hasa watu wanaokuwa katika majanga mbalimbali ikiwemo mafuriko. Kushoto ni   Askofu Kiongozi wa Kanisa la Abundant B...

WAZIRI MKUU AZINDUA MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI SINGIDA

Image
  WAZIRI anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Singida kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Angelina Lutambi   WAZIRI anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Singida kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Angelina Lutambi Kikundi cha Ngoma Asili cha Sarakasi wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi mwenye kilemba cheupe akishiriki kucheza ngoma ya asilina wadau mbalimbali WAZIRI wa Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikagua baadhi bidhaa zilizoletwa na wadau mbalimbali Kwaya ya Chuo cha Utumishi Singida wakitumbuiza wakati wa tukio hilo Na John Mapepele, Singida Waziri kuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassimu Majaliwa  amezitaka  Maml...

GEKUL AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA KITUO CHA UKAGUZI WA MIFUGO RUVU DARAJANI

Image
Msimamizi  wa Ujenzi wa Bwawa la Kunyweshea Mifugo la Chamakweza, Robert Baltazar akimuonesha michoro ya bwawa hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wa kwanza kulia) alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa hilo lililopo Chalinze, Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani Februari 24, 2021. Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarist Ndikilo.   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia) alipofanya ziara kukagua Kituo cha Ukaguzi wa Mifugo cha Ruvu Darajani kilichopo Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani jana. Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Rogers Shengoto akijibu moja ya hoja ziliyoibuliwa katika ziara ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul aliyoifanya Mkoani Pwani.     Na Mbaraka Kambona, Pwani   Naibu Wazi...

DC IKUNGI AIAGIZA HALMASHAURI KUWAACHIA WANANCHI MASHAMBA YA KUPANDA KOROSHO

Image
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,  Edward Mpogolo (kushoto) akizungumza na wananchi wa Vijiji vya  Ulyampiti na Mwau katika eneo lenye mgogoro. Wananchi wa Vijiji vya  Ulyampiti na Mwau wakiwa katika eneo lenye mgogoro. Na Dotto Mwaibale, Singida MKUU wa Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Edward Mpogolo ameagiza Halmashauri  kuwaachia mashamba yao wananchi zaidi ya 36 ambayo walimpa mkulima mmoja mgeni bila ya kufuata utaratibu ili apande korosho. Katika hatua nyingine Mpogolo ameiagiza halmashauri ya kijiji  na Idara ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kumpatia eneo lingine mkulima huyo ili aweze kuliandaa na kuanzisha kilimo hicho badala ya kuyachukua mashamba ya wananchi hao waliyo yaendeleza na kupanda mazao ya chakula. Mpogolo amechukua hatua hiyo baada ya kutokea mgogoro wa kugombea mashamba baada ya mkulima mgeni kupewa mashamba ya wananchi waliyoyafyeka na kuyatumia kwa kilimo. Mpogolo alisema kama halmashauri imetenga eneo hilo kwa kilimo cha korosho ni...

DC IKUNGI AIAGIZA HALMASHAURI KUWAACHIA WANANCHI MASHAMBA YA KUPANDA KOROSHO

Image
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,  Edward Mpogolo. Na Dotto Mwaibale, Singida MKUU wa Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Edward Mpogolo ameagiza Halmashauri  kuwaachia mashamba yao wananchi zaidi ya 36 ambayo walimpa mkulima mmoja mgeni bila ya kufuata utaratibu ili apande korosho. Katika hatua nyingine Mpogolo ameiagiza halmashauri ya kijiji  na Idara ya Kilimo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kumpatia eneo lingine mkulima huyo ili aweze kuliandaa na kuanzisha kilimo hicho badala ya kuyachukua mashamba ya wananchi hao waliyo yaendeleza na kupanda mazao ya chakula. Mpogolo amechukua hatua hiyo baada ya kutokea mgogoro wa kugombea mashamba baada ya mkulima mgeni kupewa mashamba ya wananchi waliyoyafyeka na kuyatumia kwa kilimo. Mpogolo alisema kama halmashauri imetenga eneo hilo kwa kilimo cha korosho ni vyema na wananchi hao wakawezeshwa na wao kunufaika na zao hilo la korosho badala ya kuwafukuza. Vijiji vilivyokuwa na mgogoro huo ni Ulyampiti na Mwau huku kila upande ukiomba k...

KIMIMBI HERBAL CLINIC YAIOMBA NIMR KURUHUSU DAWA YA COVID 19

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Kimimbi Herbal Clinic inayojishughulisha na utengenezaji wa dawa za asili, Kafana Mussa  akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kiwalani jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi Mtendaji wa Kimimbi Herbal Clinic inayojishughulisha na utengenezaji wa dawa za asili, Kafana Mussa (kushoto) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kiwalani jijini Dar es Salaam jana. Ofisi ya   Kimimbi Herbal Clinic iliyopo Kiwalani jijini Dar es Salaam.  Kipeperushi kinacho onesha magonjwa yanayotibiwa na dawa hiyo. Na Dotto Mwaibale KIMIMBI Herbal Clinic inayojishughulisha na utengenezaji wa dawa za asili imeiomba Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kuruhusu dawa ya Kafana 20 inayotibu ugonjwa wa Corona ili iwasaidie wananchi. Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Clinic hiyo Kafana Mussa wakati akizungumza   na waandishi wa habari ofisini kwake Kiwalani jijini Dar es Salaam ja...

TALIRI YAJIKITA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFUGAJI NCHINI

Image
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima (katikati- aliyevaa suti nyeusi) akijadiliana jambo na baadhi ya Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Maafisa wengine wa kituo cha TALIRI Mpwapwa alipotembelea kituo hicho jana. Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima (katikati- aliyevaa suti nyeusi) akijadiliana jambo na baadhi ya Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Maafisa wengine wa kituo cha TALIRI Mpwapwa alipotembelea kituo hicho jana. Baadhi ya Ng'ombe wanaofugwa katika kituo cha TALIRI Mpwapwa kilichopo Wilayani Mpwapwa wakinywa maji katika kisima kilichotengwa kando ya Josho la Nunge kwa ajili ya kunyweshea mifugo. Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani, Dkt. Angello Mwilawa akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani)   kuhusu utafiti wa malisho unaofanywa na Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TAL...

WANAMUZIKI KUKUTANA KESHO HOTELI YA MOUNT MERU JIJINI ARUSHA

Image
Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa. Katibu Mkuu wa wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), , Stella Joel. Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Dofa kutoka Karatu ambao wataimba wimbo maalumu kwenye kongamano hilo. Na Dotto Mwaibale WANAMUZIKI watakutana  kesho katika kongamano la fursa litakalofanyika Hoteli ya Mont Meru  jijini Arusha. Mgeni  rasmi  katika kongamano hilo  anatarajiwa  kuwa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ambaye atawakabidhi baadhi ya wanamuziki kadi za bima ya afya ya Taifa (NHIF).   "Wanamuziki watakao pata kadi hizo ni wale ambao wametimiza vigezo kama walivyoeleza Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Eric Kisanga na Katibu Mkuu wa umoja huo, Stella Joel ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo. Baadhi ya wanamuziki maarufu watakao kuwepo kwenye kongamano hilo ni Emanuel Mbasha (Dsm) Stara Thomas (Dsm) Hafsa kazinja, Rehema Tajiri (Dsm) Edson Mwasabwite (Dsm) 6. Emanuel Mabisa (Dsm)...