ESTL YAKUTANA NA MAKUNDI MBALIMBALI NDANI YA JAMII KUJADILI NAMNA YA KUTOKOMEZA UKATILI NA UKEKETAJI SINGIDA
Mratibu wa mradi wa kutokomeza ukatili na ukeketaji kutoka Shirika la la kiserikali la Empower Society Transform Lives (ESTL) , Annamaria Mashaka akitoa mafunzo mbele ya watu maarufu na Mangariba wastaafu, mafunzo yaliyofanyika jana katika Shule ya Sekondari Mungumaji. Wakatikati mbele ni Mohamed Msafiri mtu maarufu, wa kwanza kulia ni Mwalimu Doris Pantaleo na kushoto ni Hamida Senge wote wakazi wa Kata ya Mungumaji wakifuatilia mafunzo. Mmoja wa watoa elimu kutoka Shirika la ESTL, Brigita Mwaka akitoa mafunzo kwa Vijana wa Mungumaji walio nje ya Shule.. Afisa Ufatiliaji na tathimini wa Shirika lisilo la kiserikali la Empower Society Transform Lives (ESTL)Mkoa wa Singida, Philbert Swai, akielekeza jambo katika kikao hicho. Na Dotto Mwaibale, Singida SHIRIKA lisilo la kiserikali la Empower Society Transform Lives (ESTL)Mkoa wa Singida limekutana na makundi mbalimbali ya wakazi wa Kata ya Mungumaji kujadili namna ya kutokomeza ukatili wa ki...