SERIKALI SINGIDA YAKAMATA MALORI YENYE TANI 40 ZA MAZAO YASIYO LIPIWA USHURU
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili akikagua moja ya lori lililokamatwa na shehena ya maharage ambayo yanadaiwa kutolipiwa ushuru. Mfanyabiashara wa maharage , Philipp Lehema akizungumza na Mkuu wa Wilaya Paskas Muragili baada ya kukamatwa kwa maharage hayo. Mkaguzi wa mazao katika Kituo cha Njia Panda, Juma Athumani akitoa maelezo kwa DC Muragili jinsi alivyo yakamata magari hayo. Malori yaliyokamatwa na mzigo huo. Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Hassan Ngoma (katikati) akizungumzia tukio hilo. DC Muragili (kushoto) akizungumza na dereva Moses Zelothe ambaye gari lake lilikamatwa na mchele ambao haukulipiwa ushuru. Diwani Mstaafu Hamisi Labu akiipongeza Serikali kwa kuyakamata magari hayo na kuwaomba wafanyabiashara kujenga tabia ya kulipa ushuru wa mazao pasipo shuruti. Na Dotto Mwaibale, Singida SERIKALI mkoani Singida imekamata malori matano yenye magunia ya mazao mchanganyiko zaidi ya tani 40 yaliyokuwa yakipitia mkoani hapa bila ya kuwa na nya...