Posts

Showing posts from June, 2021

FAINALI ZA KIHISTORIA UMISSETA 2021 ZAUNGURUMA MTWARA

Image
    Mwandishi Maalum, Mtwara Michezo inayoendelea kwenye Mashindano ya Taaluma na Michezo kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) yanafikia fainali Julai 1, 2021 kwenye viwanja mbalimbali vya mjini Mtwara ambapo mashindano hayo yatafungwa rasmi Julai 2,2021. Kwa mujibu wa Msemaji wa mashindano hayo, John Mapepele fainali ya soka kwa wavulana itakuwa baina ya timu ya Pemba na Mtwara na itachezwa siku ya kufunga mashindano hayo Julai 2, 2021 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu soka utachezwa kesho baina ya timu ya mkoa wa Dodoma na Geita. Amesema mchezo wa Soka kwa upande wa wasichana utakuwa baina ya timu ya mkoa wa Mwanza na Tabora ambao utachezwa mchana Julai 1,2021 ambapo hadi sasa mshindi wa tatu ni mkoa wa Arusha.   Pia fainali ya Mpira wa Pete itakuwa dhidi ya timu ya mkoa wa Mwanza na Songwe Kwa upande wa mpira wa Wavu fainali wasichana itachezwa baina ya mkoa wa Dar es Salaam na Mtwara wakati wavulana itakuwa kati ya Dar es Salaa...

TAASISI YA WoLaOTa YAOMBA MABORESHO KATIKA SEKTA YA ELIMU

Image
 Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uboreshaji Maadili kwenye Utumishi wa Umma na Sekta Binafsi Tanzania (WoLaOTa) , Samwel Olesaitabau, akizungumza na waandishi wa habari juzi. Na Dotto Mwaibale, Singida TAASISI ya Uboreshaji Maadili kwenye Utumishi wa Umma na Sekta Binafsi Tanzania (WoLaOTa) yenye makao yake makuu mkoani hapa imemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta ya elimu kwa kuwa  na makundi mawili ya wakaguzi wa elimu.  Ombi hilo limetolewa na  Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Samwel Olesaitabau katika mkutano wake na waandishi wa habari mkoani hapa juzi wakati akitoa maoni yake kuhusu siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwa madarakani. "Kwa niaba ya Bodi ya WoLaOTa nampongeza Rais Samia katika kuunda Serikali yake yupo makini na ameanza vizuri na mara nyingi nyota njema ni ya asubuhi," alisema Olesaitabau. Olesaitabau alisema wanamuomba Rais Samia kuboresha sekta hiyo kwa kuweka wakaguzi au wadhibiti ubora wa elimu wenye sifa na wawe katika makundi mawi...

MAAFISA VIJANA NA MAAFISA MAENDELEO NGAZI ZA HALMASHAURI WATAKIWA KUWASAIDIA VIJANA.

Image
Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (wa pili kulia) akiwaelekeza jambo  viongozi wa mradi wa kilimo wa vijana  ujulikanao kwa jina la Singida Youth Agricultural Group uliopo Uhamaka Manispaa ya  Singida alipofanya ziara ya kukagua mradi huo juzi.   Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (wa pili kulia) akisisitiza jambo katika ziara hiyo. Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (wa pili kulia) na viongozi wa kikundi hicho wakiangalia bwawa la ufugaji wa samaki. Ukaguzi wa shamba ukifanyika katika ziara hiyo.  Na Dotto Mwaibale, Singida KAIMU Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani amewataka Maafisa Maendeleo ngazi za Halmshauri na Kata kuwasaidia vijana kuwaweka pamoja na kuunda vikundi. Ndahani alitoa ombi hilo juzi wakati akikagua mradi wa kilimo wa vijana  ujulikanao kwa jina la Singida Youth Agricultural Group uliopo Uhamaka Manispaa ya  Singida. Vijana hao kupitia mradi huo wanajishughuli...

MFUMO WA RIPAT CHACHU YA MAGEUZI YA KILIMO NCHINI USAMBAE NCHI NZIMA.

Image
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA (Taaluma) Prof. Maulid Mwatawala akitoa nasaha zake kabla ya kufunga mradi huo wa RIPAT - SUA.  Mratibu wa Mradi upande wa SUA Dkt. Emmanuel Malisa akieleza utekelezaji wa mradi huo hatua kwa hatua toka mwanzo hadi hapo unapofikia tamati. Zidia Malundo akisoma risala kwa niaba ya vikundi vyote 22 vilivyoshiriki kwenye mradi huo mbele ya mgeni rasmi. Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ugani na utafiti kutoka Wizara ya Kilimo Charles Mjema akitoa salamu za Wizara kwenye hafla hiyo ya kufunga mradi. Rasi wa Ndani ya Sayansi za Jamii na Insia ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Samweli Kabote akitoa akizungumza kwenye hafla hiyo kuhusu mashirikiano kati ya SUA na shirika la RECODA. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manispaa ya Morogooro, Michael Waluse akitoa salamu za Manispaa kuhusu mafanikio na mikakati ya kuendeza Mbinu hiyo kwenye kata zote za Manispaa ya Morogoro. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmas...

RC MAHENGE AKERWA NA MLUNDIKANO WA TAKA MANISPAA YA SINGIDA ATOA SIKU TATU ZIONDOSHWE

Image
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge alipofika kukagua  Ofisi za Manispaa ya Singida baada ya kuzungumza na watumishi na watendaji wa manispaa hiyo wakati akianza ziara yake ya kwanza ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi,  kuhamasisha ukusanyaji wa mapato, ulipaji wa kodi na ushuru. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Singida (hawapo pichani) katika mkutano alioufanya jana  wakati wa ziara hiyo. Watumishi na watendaji wa Manispaa ya Singida wakimsikiliza mkuu wa mkoa wakati alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano huo. Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Deus Luziga akizungumza kwenye mkutano huo. Mkutano ukiendelea. Watumishi na watendaji wa Manispaa ya Singida wakimsikiliza mkuu wa mkoa wakati alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano huo. Katibu Mwenezi  na Itikadi  wa  Chama cha Mapinduzi ( CCM )  Mkoa wa S...

TEWW INAVYOWASAIDIA WASICHANA WALIOISHIA NJIANI KUMALIZA MASOMO YAO

Image
Timu ya Viongozi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima nchini (TEWW) mkoani Iringa wakiwa wamemtembelea mmoja wa wasichana aliyekatisha masomo yake baada ya kupata ujauzito ili arejee shuleni. Mmoja wa Mabinti (katikati) ambaye ndoto zake zilizima baada ya kupata ujauzito akiwaelekeza wenzake baada ya kurudi shule kupitia mpango wa TEWW. Baadhi ya walimu na wanafunzi wanaosoma kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu wazima nchini (TEWW) mkoani Iringa kupitia Kituo cha Sabasaba wakiwa katika picha ya pamoja. Na Mwandishi wetu, Iringa TAASISIi ya Elimu ya Watu wazima nchini (TEWW) inatekeleza mpango wa kuwasaidia wasichana waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwamo mimba, kumaliza elimu ya sekondari. Taasisi hiyo imebeba jukumu la kuwasaidia wasichana hao wakati ambapo  bado sera ya elimu ikiwa haijaruhusu, kuendelea na masomo kupitia mfumo wa kawaida. Mkurugenzi Mkuu wa TEWW, Dkt Michael Ng’umbi amesema katika taarifa yake kuwa kwa namna ya pekee mfumo huo umekuwa mkombozi kwa wasichan...

RC SINGIDA: AMUAPISHA MKUU MPYA WA WILAYA YA IRAMBA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akimuapisha Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akimkabidhi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi   ( CCM) Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Semani Mwenda baada ya kumuapisha.  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza baada ya kumuapisha mkuu huyo wa wilaya. Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Semani Mwenda akizungumza baada ya kuapishwa. Familia ya mkuu huyo mpya wa wilaya ya Iramba ikiwa kwenye hafla ya uapisho wa mpendwa wao. Hafla ikiendelea. Hafla ikiendelea. iongozi wa dini wakiwa kwenye hafla hiyo ya uapisho wa mkuu huyo wa wilaya.  Hafla ikiendelea. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili(kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro  (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Selemani ...

KAMISHNA WA ARDHI MSAIDIZI MKOA WA SINGIDA AANZA KUPIMA MAENEO YA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA

Image
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida Shamim Hoza (katikati) akiweka alama ya mpaka litakapopita  bomba la mafuta ghafi kati ya Tanzania na Uganda wakati wa uzinduzi wa upimaji mkuza wa bomba hilo katika Kijiji cha Mseko Wilaya ya Iramba mkoani hapa jana. Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida Shamim Hoza, akizungumza na wananchi kuhusu faida ya mradi wa bomba la mafuta ghafi kati ya Tanzania na Uganda wakati wa uzinduzi wa upimaji mkuza wa bomba hilo katika Wilaya ya Iramba mkoani hapa jana.   Mpima Ardhi Mkoa wa Singida Sesaria Martin  akizungumza na wananchi katika mkutano huo.   Afisa Ardhi  Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Singida Benedict Mwombeki  akizungumza na wananchi katika mkutano huo. Mwenyekiti wa Kijiji cha Mseko, Salum Kisaba akizungumza na wananchi katika mkutano huo.   Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mseko, Miriam Kaali akizungumza na wananchi katika mkutano huo. Wapima Ardhi Mkoa wa Singida wakipima eneo la Mkuz...