Posts

Showing posts from August, 2021

PROF. LUGHANO KUSILUKA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA VETERINARI TANZANIA

Image
Profesa Lughano Kusiluka Mwenyekiti Mpya Baraza la Veterinari Tanzania. Na Mwandishi Wetu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amemteua Profesa. Lughano Kusiluka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari Tanzania. Profesa Kusiluka ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe anachukua nafasi hiyo iliyokuwa inashikiliwa na Profesa. Rudovick Kazwala ambaye muda wake umeisha. Uteuzi huo utaanza rasmi kesho Septemba 1, 2021 kwa kipindi cha miaka minne (4).  

WAHUDUMU WA AFYA SINGIDA KUTEMBEA NYUMBA KWA NYUMBA KUONDOA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith  Mahenge akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Wataalam wa afya wa Mkoa wa Singida kilichokuwa kinajadili tathmini na vifo vya kinamama vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga kilichofanyika katika Ukumbi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni  mkoani Singida leo. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick akizungumza kwenye kikao hicho.   Na Mwandishi Wetu, Manyoni. WATOA huduma za afya katika ngazi za kata na vijiji wametakiwa kutembelea nyumba kwa nyumba ili kuwatambua mama wajawazito na watoto walioko maeneo hayo ili kuwapatia ushauri wa kiafya kwa kuwa hao ndio wateja wao. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith  Mahenge ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua kikao kazi cha Wataalam wa afya wa Mkoa wa Singida kilichokuwa kinajadili tathmini na vifo vya kinamama vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga kilichofanyika katika ukumbi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ...

MHE. BASHUNGWA AWAPIGANIA WANAMICHEZO KUPATIWA CHANJO DAR

Image
  Waziri  wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa akizungumza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa aliyevalia jezi ya timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) katikati  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mpira wa soka na wachezaji wa timu za taifa za wanawake (Twiga Stars na Tanzanite) alipowatembelea wakiwa mazoezini katika viwanja vya  Kidongo chekundu maarufu kama  JK Park jijini Dar es Salaam. Na John Mapepele, WHUSM   Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya leo Agosti 28, 2021 imeratibu zoezi la hiari la siku mbili kwa timu za Taifa za michezo na wadau wote wa michezo upatiwa chanjo ya Uviko-19 jijini Dar es Salaam ili kujikinga na ugonjwa huo.   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa amesema makundi hayo yamependekezwa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia, pa...

WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA MAJENGO MAPYA YA JESHI LA POLISI MKOA WA SINGIDA

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kushoto) akikata utepe kuzindua jengo jipya la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida leo. Wengine kutoka kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Stella Rutabihirwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Siro, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Christopher Kadio. (Picha zote  Dotto Mwaibale na Godwin Myovela) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua jengo jipya la ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida. Muonekano wa jengo hilo. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua jengo la Kikosi cha Kutuliza Ghasia  (FFU) Mkoa wa Singida. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Siro, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Stella Rutabihirwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio. Waziri Mkuu K...

MAADHIMISHO YA KIMATAIFA YA MUZIKI DUNIANI KUZINDULIWA RASMI JIJINI ARUSHA.

Image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) Stella Joel.  Dotto Mwaibale, Arusha   WANAMUZIKI wa Watanzania wanatarajia kuanza Maadhimisho ya Kimataifa  ya Muziki Duniani yatakayo zinduliwa rasmi kesho kutwa Septemba 1, 2021 jijini Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) Stella Joel alisema kesho kutwa yatazinduliwa rasmi maadhimisho hayo na kuwa mwezi Septemba wote Wanamuziki wa kada zote watashiriki kuhamasisha shughuli mbalimbali za  maendeleo. "Kwa Dar es salaam Wanamuziki watakutana Makumbusho ya Taifa iliyopo Posta kuanzia Saa 4 asubuhi ambao watakuwa na jumbe mbalimbali za Kuhamasisha maendeleo ya muziki na kushiriki shughuli za ujenzi wa Taifa," alisema Joel. Joel alisema kwa upande wa Arusha Wanamuziki watakutana katika Makumbusho ya Taifa na kwa Mkoa wa Mwanza  watakutana na Kufanya ziara ya Utalii wa Ndani na  kujionea vivutio vya utalii wa nchi yetu na kukitangaza ...

MPANGO WA USIMAMIZI WA MAZINGIRA WILAYA ZA SINGIDA MBIONI KUKAMILIKA

Image
Mratibu wa Sera kutoka Shirika la Kuendeleza Kilimo Hai nchini (TOAM), Paul Chilewa, akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha wataalam kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Wizara ya Kilimo, TAMISEMI, na Mashirika ya kuendeleza Kilimo Hai nchini (TOAM, GIZ na Helvetas), ambacho kilifanyika juzi mkoani hapa lengo likiwa ni kutathmini na kuweka mikakati ya kuhakikisha ajenda ya 'Kilimo Himilivu' na 'Mabadiliko ya Tabianchi' vinaingizwa katika Mpango wa Mazingira wa miaka mitano ndani ya halmashauri za wilaya za Singida. Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho. Mratibu wa Mradi wa Kilimo Himilivu cha Pamba kutoka GIZ kwa mkoa wa Singida, Leonard Mtama, akichangia jambo kwenye kikao hicho. Kikao kikiendelea. Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Mkalama,  Seleman Musunga, akizungumza  kwenye kikao hicho. Afisa Mazingira kutoka Wilaya ya Iramba, Yohana Dondi,akizungumza  kwenye kikao hicho. Washiriki wa kikao hicho wakiwa katika picha ya pamoja, Godwin Myovela na Dotto M...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YARIDHISHWA NA MIRADI SINGIDA

Image
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheriaya hiyo Najma  Murtaza  Giga (katikati) akizungumza na Wanachuo cha Ufundi Veta Mkoa wa Singida na wadau wengine baada ya Wajumbe wa kamati hiyo kutembelea chuo hicho jana. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida, Selemani Mwenda na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu Profesa Jamal  Katundu. Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo walipotembelea karakana ya mitambo mbalimbali chuo cha Veta Singida. Wajumbe wa kamati hiyo wakinunua bidhaa za wajasiriamali waliowezeshwa na Serikali. Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo walipotembelea banda la Mjasiriamali aliyetengeneza majiko kwa kutumia teknolojia ya udongo na mabati. Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo walipotembelea SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu. Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani akizungumza na Wanafunzi wa SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye ...

WAZAZI WAHIMIZWA KUZINGATIA LISHE BORA KWA WATOTO

Image
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Asimwe Rwiguza (kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Juma Irando (katikati) pamoja na Katibu wa Chama cha Ushirika cha Wanawake, Nronga, Hellen Ussiri kwa pamoja wakinywa maziwa ikiwa ni ishara ya kuzindua Awamu ya Pili ya Unywaji wa maziwa Shuleni katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro jana. Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt.George Msalya akizungumzia maendeleo ya tasnia ya maziwa kwenye uzinduzi huo.     Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Asimwe Rwiguza akizungumza kwenye uzinduzi huo. Mmoja wa Maafisa wa Chama cha Ushirika cha Wanawake Nronga akigawa maziwa kwa Wanafunzi. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Asimwe Rwiguza (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa majokofu kwa wafanyabiashara. Na Mbaraka Kambona, Kilimanjaro WAZAZI nchini wamehimizwa kuweka mkazo katika kuwapatia watoto wao lishe bora ikiwemo kuhakikisha wanakunywa maziwa kila waka...

SHIRIKA LA POSTA MKOANI SINGIDA LAFUNGUA PAZIA MASHINDANO MBALIMBALI KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA POSTA OKTOBA 9, 2021

Image
Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Singida, Joseph Mutatina akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi kompyuta  tano zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mussa  Sima kwa ajili ya Shule ya Msingi Nyerere mjini hapa jana. Diwani wa Kata ya Mghanga Manispaa ya Singida, Vellerian Kimambo akizungumza  wakati akikabidhi kompyuta hizo. Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa kompyuta hizo. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Charles Ngowi akizungumza wakati wa hafla hiyo. Katibu wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Kata ya Mghanga, Issa Mwanja akizungumza wakati wa hafla hiyo. Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida, Hamisi Karage akizungumza wakati wa hafla hiyo. Makabidhiano ya kompyuta hizo yakifanyika. Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule hiyo baadaya hafla hiyo. Walimu wa shule hiyo, wazazi, pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha yapamoja baada ya kumpokea msaada wa kompyuta hizo. . Na Godwin Myovela...