Posts

Showing posts from September, 2021

SINGIDA DC YAPONGEZWA KWA UELEWA WA UHAMASISHAJI CHANJO YA UVIKO 19

Image
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) Idara ya Jamii  na Lishe, Dinah Atinda, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi Wilaya ya Singida DC      katika kikao kilichoketi mkoani hapa jana.     Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Paskas Muragili, akizungumza kwenye kikao hicho. Kikao kikiendelea. Picha ya pamoja.  Picha ya pamoja. Na Dotto Mwaibale, Singida. MWAKILISHI kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) Idara ya Jamii  na Lishe, Dinah Atinda amewapongeza wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi Wilaya ya Singida DC kwa kuwa na uelewa mpana wa uhamasishaji wa chanjo ya Uviko 19 ambao unaendelea nchini kote. Atinda alitoa pongezi hizo jana kwa niaba ya wenzake katika semina ya siku moja iliyokuwa ikitolewa kwa wajumbe hao wilayani humo. " Tunapita katika Halmashauri zote kuangalia namna kinavyofanyankazi hiki kikao cha PHC lakini napenda ...

MSD KUANZISHA KIWANDA CHA DAWA ZA NGOZI NCHINI

Image
Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa (MSD), Meja Jenerali Gabriel Mhidze akizungumza na  waandishi wa habari kwenye semina ya  siku moja iliyoandaliwa na MSD iliyokuwa na lengo la kutoa taarifa ya mafanikio na mwelekeo wa MSD,  jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD Erick Mapunda. Wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye semina hiyo. Waandishi wa Habari wakiwa kwenye semina hiyo. Semina ikiendelea. Na Dotto Mwaibale MKURUGENZI  Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Meja Jenerali Gabriel(Dkt) Mhidze amesema MSD iko mbioni kuanzisha kiwanda cha dawa za ngozi,ikiwemo mafuta maalumu ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Meja Jenerali Mhidze aliyaeleza hayo jana  mbele ya waandishi wa habari alipokuwa akizungumzia kuhusu majukumu na maboresho ya MSD. Alisema kiwanda hicho, ambacho mashine zake zimeshafika kitazalisha pia dawa za meno na dawa za macho. Aidha Mkurugenzi Mkuu huyo wa MSD ameeleza kuwa kiwanda cha  MSD cha kuzalisha mipir...

Wadau wa Maendeleo Kutia Nguvu Kwenye Uhamasishaji na Elimu ya Chanjo Mkoa Wa Singida

Image
  SERIKALI imewapongeza Wadau mbalimbali wa maendeleo waliojitokeza katika kikao kazi cha Sekta ya Afya Mkoani Singida na kujitolea viwezeshi mbalimbali vitakavyosaidia  kuendesha zoezi la  utoaji wa  hamasa, elimu na chanjo kwa jamii . Baadhi ya wadau hao wameahidi kusaidia upatikanaji wa  magari ya matangazo, mafuta kwa ajili ya safari za vijijini  huku wengine wakiwa tayari kusaidia kupeleka elimu waliyoipata kuhamasisha jamii juu ya  zoezi la uchanjaji lengo likiwa na kufanikisha kwa kiwango kikubwa. Pongezi hizo zimetolewa leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mganga Mkuu wa Mkoa Victorina Ludovick wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa  Hoteli ya KBH na kubainisha kwamba  jitihada zinazooneshwa na wadu hao zitasaidia katika kuwafikia watu wengi vijijini na kutoa elimu ya chanjo. Mganga Mkuu wa Mkoa  Singida Victorina Ludovick akieleza jambo wakati wa mkutano huo. Pamoja na hayo Mganga mkuu amesema kwam...

MAFUNZO YA CHANJO KWA KAMATI ZA AFYA YA MSINGI WILAYA YA MKALAMA YAZAA MATUNDA

Image
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) Idara ya Afya Ustawi wa Jamii na Lishe, Dinah Atinda akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati ya Msingi ya Afya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida yenye mpango harakishi wa kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu chanjo ya Uviko 19 na kuchanja. Richard Magodi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara ya Mpango wa Taifa wa Chanjo akishiriki kutoa mafunzo hayo. Mkuu wa wilaya hiyo Sophia Kizigo (katikati) akishiriki mafunzo hayo. Mafunzo hayo yakiendelea. Nyuma mwenye miwani ni  Mchungaji Sefine Kanga wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) Usharika wa Dumanga. Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) Idara ya Afya Ustawi wa Jamii na Lishe, Dinah Atinda na Afisa Msanifu Patrice Makhao kutoka  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia mafu...

SERIKALI YATUMIA SH. BILIONI 52.975 KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI SINGIDA

Image
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa akionesha Jarida la Nchi Yetu wakati akitoa taarifa ya wiki ya Serikali kwa waandishi wa habari mkoani Singida leo. Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa hiyo. Taarifa ikitolewa. Waandishi wa habari wakisikiliza taarifa hiyo. Waandishi wa habari wakisikiliza taarifa hiyo. Kushoto ni Afisa Habari Msaidizi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mwanahabari Elisante Mkumbo akiuliza swali kwenye mkutano huo. Mwanahabari Damiano Mkumbo akiuliza swali kwenye mkutano huo. Mwanahabari  Edina Alex akiangalia   Jarida la Nchi Yetu kwenye mkutano huo.  Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo. Mkutano ukiendelea. Kazi ikiendelea, Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu akiuliza swali kwenye mkutano huo. Na Dotto Mwaibale, Singida SERIKALI imetoa Sh.Bilioni 52.975  mkoani Singida kwa ajili  ya kutek...

MKOA WA SINGIDA WABAINIKA KUWA NA ALMASI BORA TANZANIA

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JICT LTD inayojishughulisha na Utafiti wa Almasi Javan Bidogo ambaye pia ni mmiliki wa mradi wa utafuta wa Almasi katika Kijiji cha Mbereseke kilichopo Wilaya ya Iramba mkoani hapa, akimuelekeza jambo Naibu Waziri Wizara ya Madini Profesa Shukuru Manya (wa pili kulia mbele) wakati alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea na kukagua mradi huo jana. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JICT LTD inayojishughulisha na Utafiti wa Almasi Javan Bidogo ambaye pia ni mmiliki wa mradi wa utafuta wa Almasi katika Kijiji cha Mbereseke kilichopo Wilaya ya Iramba mkoani hapa, akitoa maelezo kwa  Naibu Waziri Wizara ya Madini Profesa Shukuru Manya (katikati) wakati alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea na kukagua mradi huo jana. Mkuu wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda akizungumza wakati wa ziara hiyo. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Madini Profesa Shukuru Manya, Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahaman Mwanga, K...

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MADINI AMALIZA MGOGORO WA UMILIKI MGODI KWA DAKIKA 120

Image
Naibu Waziri Wizara ya Madini Profesa Shukuru Manya akizungumza na wachimbaji wadogo wa mgodi wa dhahabu wa Kijiji cha Matongo katika mkutano wa hadhara alipokwenda kutatua mgogoro wa umiliki wa mgodi huo jana uliopo wilayani Ikungi mkoani Singida Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahaman Mwanga akizungumza na wachimbaji wakati wa utatuzi wa mgogoro huo. Kaimu Afisa  Madini Mkazi Mkoa wa Singida, Chone Malembo  akizungumza na wananchi katika mkutano huo. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumza na wananchi katika mkutano huo. Naibu Waziri wa Madini Profesa Shukuru Manya (wa nne kulia)akizungumza na wachimbaji wadogo wa mgodi wa dhahabu wa Kijiji cha Matongo wakati akikagua maduara ya uchimbaji. Wachimbaji wadogo wa mgodi huo wakiwa mkutanoni. Mchimbaji Abdulkheri Abdulkadir kutoka Geita, akizungumza kero zinazo wasibu wachimbaji kwenye mgodi huo. Mchimbaji  kutoka Mkoa wa Iringa Geita, akizungumza kero zinazo wasibu wachimbaji kwenye mgodi huo. Mmiliki wa mgodi huo Rich...