Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Kejeri Gillah (wa pili kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Washiriki wa Mkutano wa uwasilishaji wa utafiti wa awali kuhusu Gugu Kongwa uliofanyika jijini Dodoma jana. Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Prof. Antony Sangeda akiwasilisha sehemu ya utafiti wa Gugu Kongwa kwa Wadau wa Sekta ya Mifugo katika Mkutano wa uwasilishaji wa Utafiti huo uliofanyika jijini Dodoma jana. Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI), Prof. Erick Komba akitoa maoni yake katika Mkutano wa uwasilishaji wa utafiti wa awali kuhusu Gugu Kongwa uliofanyika jijini Dodoma jana. Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Kejeri Gillah (kulia) akiwa na wadau wengine wakifuatilia uwasilishaji wa utafiti wa awali kuhusu Gugu Kongwa uliofanyika jijini Dodoma jana. Na Mbaraka ...