Posts

Showing posts from January, 2022

YAKUBU- VYUO VIKUU ENDELEENI KUANDAA MATAMASHA

Image
  Na. John Mapepele Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, sanaa na Michezo. Saidi Yakubu ametoa wito  kwa vyuo vikuu nchini vinavyofundisha sanaa kuandaa matamashaa  ya utamaduni ili kuibua vipaji vitakavyoleta ajira kwa vijana. Yakubu ameyasema  haya  leo  Januari 29, 2022 alipokuwa akimwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed  Mchengerwa wakati wa kilele cha tamasha la  sanaa la kuadhimisha miaka 60 ya Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam toka kuanzishwa kwake. Amefafanua kwamba matamasha haya yanasaidia kuibua vipaji na kuendeleza utamaduni wa taifa letu. Aidha, amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa nafasi ya washindi watatu katika tamasha hili kushiriki kwenye tamasha kubwa la kitaifa la Serengeti litakalofanyika  Dodoma mapema mwezi Machi 2022. Amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa  kuunga  mkono juhudi za Mhe. Rais katika kuendeleza Utamaduni na dira yake ya 2061 na mikakati yake ya kuimaris...

MBUNGE TAWHEEDA ANOGESHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO MIAKA 45 CCM -UWT WILAYA YA SINGIDA

Image
Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) ambaye alikuwa mgeni rasmi, akizungumza katika Maadhimisho ya miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida DC yaliyofanyika juzi mkoani Singida. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, William Nyalandu. Mwenyekiti wa  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida DC Neema Sambaa akimvika  vazi la kimila la kabila la Wanyaturu Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) ikiwa ni kumpa heshima wakati wa maadhimisho hayo ambapo pia alikabidhiwa kibuyu cha jadi cha kabila hilo. Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) (kulia) muda mfupi baada ya kuwasili wilayani Singida DC kwenye maadhimisho hayo. Mbunge wa Jimbo la Mjini Magharibi Viti Maalum Mhe. Tawheeda Garlos (MNEC) akizungumza na Wanawake wa UWT Wilaya ya...

MCHENGERWA-WASANII KUZOA "MPUNGA" KILA BAADA YA MIEZI SITA

Image
    ***************** Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake kupitia Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) itaanza kugawa mirahaba kwa kazi mbalimbali za wasanii zinazotumika kwenye redio kila baada ya miezi sita ili waweze kunufaika na kazi zao. Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa utoaji wa tuzo za muziki na ugawaji wa mirahaba kwa wasanii Januari 28, 2022 kwenye Ukumbi wa kimataifa cha Julius Nyerere. Mhe Mchengerwa amesema Wizara yake inakwenda kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta hizo katika kipindi kifupi kijacho ambapo amewataka watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa kasi na weledi. Ametoa muda wa wiki tatu kwa watendaji wa Wizara kuandaa App maalum itakayoitwa “sema na Waziri wa Utamaduni “ ambayo itatoa fursa kwa wadau mbalimbali wa sekta ya Sanaa, utamaduni na Michezo kuwasiliana moja kwa moja na yeye pindi wanapotaka kuwasiliana naye badala ya mfumo wa sasa uliozoeleka. “Naomba niwaahidi hapa kuwa n...

CCM SINGIDA YAIPONGEZA WILAYA YA SINGIDA DC KWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo  Kata ya Msange Wilaya ya Singida DC jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC Ester Chaula. Mwenyekiti wa CCM  Kata ya Msange Joel Ndweti akizungumza kwenye ziara hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida DC. William Nyalandu. Mbunge wa Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo akizungumza kwenye ziara hiyo Kata ya Msange. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Ester Chaula akichangia jambo wakati akielezea ukarabati wa madara katika Shule ya Msingi Msange. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Eliya Digha akizungumza wakati wa ziara hiyo Kijiji cha Mangida. Mzee maarufu wa Kata ya Msange Philemoni Mnyawi (kushoto) kwa niaba ya wazee wa kata hiyo akimvika shuka Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya ...

RC SINGIDA AKEMEA MAUAJI YA BODABODA, ATOA MILIONI 2 KWA KIKUNDI CHA VIJANA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dk. Binilith Mahenge akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Iguguno Youth Group , Vicky Mwaisakila Sh.2. Milioni alizowaahidi hivi karibu kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali wakati wa ziara ya siku moja ya kukagua ujenzi wa miradi ya barabara wilayani Iramba. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo. Vijana wa Iguguno Youth Group wakiwa kazini.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATOA TUZO YA KISWAHILI KWA WASHINDI

Image
        ************************** Na. John Mapepele, WUSM Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa Majaliwa leo Januari 27, 2022 ametoa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati -Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa washindi wa mwaka 2021 jijini Dar es Salaam. Katika kundi la Riwaya Halfani Sudy ameibuka kuwa mshindi wa kwanza, Mohamed Omary ameibuka mshindi wa kwanza kundi la shairi, wakati Mbwana Kidato ameibuka mshindi wa pili katika kundi la tamthilia na Lukas Lubungo kuwa mshindi wa pili kwenye kundi la hadithi za kubuni. Amesema dhamira ya Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ya kutekeleza mkakati wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili Kitaifa na Kimataifa, ambao utazinduliwa hivi karibuni itafanikiwa ikiwa wadau wote watajitoa kwa dhati kutekeleza mkakati huu na kusimamia maendeleo ya lugha hii adhimu na aushi. Mhe. Majaliwa amezipongeza kampuni za SAFAL na ALAF kwa kufadhili tukio hilo na ametoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano huo...

RC SINGIDA ATEMBELEA MGODI WA SHANTA GOLD ATAKA USHIRIKIANO

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (mwenye koti la bluu) akiangalia moja ya eneo la machimbo ya dhahabu Mara baada ya kutembelea Kampuni ya Shanta Gold inayoendesha shughuli hizo  katika kijiji Cha Mang'onyi Wilaya ya Ikungi. RC.Mahenge  akiendelea na ukaguzi wa Mgodi wa machimbo ya dhahabu unaomilikiwa na Kampuni ya Shanta Gold. Ukaguzi wa mgodi huo ukiendeleaZiara unaendelea Ukaguzi ukiendelea.   Na Mwandishi Wetu, Singida   WAWEKEZAJI  mkoani Singida wametakiwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya wakati wa kuanzisha  miradi ya Maendeleo ya Kijamii  (Community socially responsibility – CSR ) ili kukubaliana aina za miradi na namna itakavyotekelezwa lengo likiwa ni  kuepuka matumizi makubwa ya fedha kwa kazi ambazo zingetumia fedha kidogo. Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Dk. Binilith Mahenge leo January 26, 2022 alipotembelea machimbo ya madini ya dhahabu yanayochimbwa na Kampuni ya  Shanta Gold iliyopo ...

YAKUBU- MAANDALIZI YA TUZO YA KISWAHILI YAKAMILIKA

Image
    ************************** Na. John Mapepele Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Saidi Yakubu amesema maandalizi ya hafla ya utoaji wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati - Cornell ya Fasihi ya Afrika hapo kesho Januari 27, 2022 jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi yamekamilika. Akizungumza leo Januari 26, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akikagua ukumbi utakaotumika, Yakubu amekishukuru Chuo Kikuu cha Cornell cha nchini Marekani na kampuni ya Alaf kwa mchango wao wa kutambua na kukuza lugha la Kiswahili kupitia utoaji wa tuzo hizo. Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mkakati wake wa kukikuza Kiswahili duniani. "Kwa namna ya pekee tunampongeza Mhe. Rais wetu kwa mapenzi yake makubwa ya kukuza Kiswahili ambapo juzi tu akiwa kwenye sherehe na mabalozi amesema Sera ya nje zitazingatia kukuza Kiswahili ."Ameongeza Yakubu. Mkurugenzi Msaidizi wa Id...

RAIS SAMIA AZIDI KUKIPAISHA KISWAHILI DUNIANI

Image
    ************************** Na John Mapepele Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan amesema Sera mpya ya mambo ya nje itaendelea kuzingatia pamoja na mambo mengine kukuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya kidiplomasia. Mhe. Rais amesema hayo wakati akizungumza na mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao Januari 24, 2022 hapa nchini pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika sherehe za mwaka mpya 2022 ( Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam. Aidha, Mhe. Rais Samia amewashukuru wote waliopitisha maazimio ya kuifanya tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa siku ya lugha ya Kiswahili duniani. Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itahakikisha inasimamia maendeleo ya Lugha ya Kiswahili kwa faida ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Said...