WAZAZI WA WANAFUNZI WALIOFAULU KWENDA SEKONDARI LAKINI HAWAJARIPOTI SHULENI KUFIKISHWA KORTINI IRAMBA
Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda akitoa maelekezo kwa wajumbe wa kamati ya Siasa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo wakati wakikagua moja ya caravati linalojengwa katika Barabara ya Maluga Mtaa Saba -Misuna na Mgungia hadi Kaselya wakati kamati hizo zilipokuwa zikikagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake Tarafa ya Shelui wilayani humo jana. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba, Samuel Ashery akizungumza wakati kamati hizo zilipokuwa zikikagua mradi wa maji wa Kijiji cha Wembere uliopo katika Tarafa hiyo. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi akizungumza kwenye ziara hiyo. Afisa Tarafa ya Kinampanda Cholo Mtaki akiwatambulisha viongozi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kitukutu wakati wa ziara ya kamati hizo. Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Iramba Mhandisi Ez...