MWAMKO DUNI WA WAZAZI WAWAKOSESHA WATOTO CHAKULA SHULENI
Ofisa Elimu Msingi katika Manispaa ya Singida, Omary Maje akifafanua jambo kuhusiana na hali halisi ya mwamko wa wazazi juu ya uchangiaji chakula kwa wanafunzi. Wanafunzi wakipata chakula moja ya shule za msingi. Na Abby Nkungu, Singida MWAMKO duni wa wazazi kuwachangia chakula cha mchana watoto wao wanaosoma bado ni changamoto kubwa ambapo asilimia 66.1 ya shule za msingi za Serikali katika Manispaa ya Singida hazitoi huduma hiyo. Hali hiyo inatajwa kuathiri usikivu, umakini, uelewa na ufaulu hasa kwa watoto wasiozidi miaka minane ambao bado wanahitaji lishe bora kwa ajili ya ukuaji wa ubongo ili waweze kufanya vyema darasani. Ofisa elimu Msingi Manispaa ya Singida, Omary Maje alisema kuwa kati ya shule 53 za msingi za Serikali zilizopo halmashauri hiyo, 18 tu (sawa na asilimia 33.9) ndizo zinazotoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wake. “Manispaa hii kuna jumla ya shule 71. Shule 53 ni za Serikali, 13 binafsi na 5 za awali tu. Wenzetu wa binafsi shu...