MILA, DESTURI ,UKOSEFU WA ELIMU VIMETAJWA KUWA NI SABABU YA KUWEPO KWA VITENDO VYA UKATILI MKOANI SINGIDA
p> Mmoja wa Shujaa kutoka Taasisi ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) akitolewa damu kwa ajili ya kuchangia akiba ya damu wakati Mashujaa kutoka SMAUJATA walipotembelea Hospitali ya Makiungu iliyopo wilayani Ikungi kwa ajili ya kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili, pamoja na kuwajulia hali wagonjwa ambapo pia walifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali hiyo katika ziara iliyofanyika jumamosi.. Uchangiaji wa damu ukifanyika. Mashujaa wakifanya usafi kuzunguka viunga mbalimbali vya Hospitali hiyo. Usafi ukiendelea. Mashujaa wa SMAUJATA wakiwafariji wagojwa kwa kufanya maombi pamoja. Sabuni zikitolewa kwa wagonjwa. Picha ya pamoja wakati wa ziara hiyo. Na Dotto Mwaibale , Singida MILA na desturi na ukosefu wa elimu vimetajwa kuwa sababu ya kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii kwa watoto ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukeketaji kwa watoto wadogo. Sababu hizo zimetolewa na wananchi wa Wilaya ya S...