REA YAZINDUA MRADI WA KUSAMBAZA UMEME MAENEO YA VIJIJI MIJI SINGIDA, MKANDARASI AKABIDHIWA RASMI MBELE YA DC
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili (katikati) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida akiwasha kifaa maalumu cha kupiga king'ora kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi mpya wa kusambaza umeme kwenye Vijiji Miji viliyopo pembezoni mwa Manispaa ya Singida katika hafla iliyofanyika Kata ya Mwankoko Desemba 29,2022 ambao utagharimu Sh. 7.11 Bilioni zilizotolewa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) amapo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) litakuwa msimamizi wa mradi huo. Na Dotto Mwaibale , Singida SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imezindua mradi mpya wa kusambaza umeme kwenye Vijiji Miji viliyopo pembezoni mwa Manispaa ya Singida ambao utagharimu Sh. 7.11 Bilioni na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) litakuwa msimamizi wa mradi huo. Mradi huo wa kusambaza umeme katika Vijiji Miji (Peri-urban Electrification) ambao umezinduliwa Desemba 29, 2022 Kitongoji cha Kitope Darajani Kata ya Mwankoko utatekelezwa kwenye vito...