Posts

Showing posts from January, 2023

KATIBU TAWALA SINGIDA: WAANDISHI WA HABARI KUWENI WAZALENDO KWA KUANDIKA HABARI ZENYE TIJA

Image
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko (kushoto) akifungua mkutano wa Uhamasishaji wa Program ya Shule Bora kwa Wasimamizi wa vyombo vya habari na Wahariri Mkoa wa Singida uliofanyika leo Januari 31, 2023 wilayani Manyoni mkoani hapa. Na Dotto Mwaibale , Manyoni WAANDISHI wa Habari Mkoa wa Singida wametakiwa kuwa wazalendo kwa kuandika habari zenye tija kwa mkoa na Taifa kwa ujumla . Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko  wakati akifungua mkutano wa uhamasishaji wa program ya Shule Bora kwa Wasimamizi wa vyombo vya habari na Wahariri Mkoa wa Singida uliofanyika leo Januari 31, 2023 wilayani Manyoni mkoani hapa. “Waandishi wa habari mnatakiwa muwe wazalendo kwa kuandika habari nyingi za maendeleo ili kuutangaza mkoa wetu na si kuandika zile zinazohusu mabaya tu japo hazikatazwi” alisema Mwaluko. Aidha Mwaluko aliwataka wanahabari kwenda vijiji kuandika habari za uchunguzi ambazo zitasaidia kuibua changamoto za wananchi, watumishi wa afya n...

KATIBU MKUU JUMUIYA YA WAZAZI : WAZAZI TUJIKITE KUTOA ELIMU YA MAADILI KWA JAMII

Image
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Gilbert Kalima akizungumza  na wananchi, Wana CCM na viongozi wa chama hicho wa Wilaya ya Singida katika mkutano uliofanyika Ofisi ya CCM  Mkoa wa Singida ikiwa ni moja ya matukio katika mfululizo wa ziara yake. Na Dotto Mwaibale , Singida KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Gilbert Kalima, ametoa rai kwa wazazi kujikita katika jukumu la kutoa elimu kwa jamii kuhusu suala la maadili kutokana  na hivi sasa kuanza kujitokeza mfululizo wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia hapa nchini. Akizungumza leo na wananchi,wanachama na viongozi wa CCM Wilaya ya Singida, amesema suala la malezi ya watoto ni jukumu la Jumuiya ya Wazazi kwani hivi sasa kumeanza kujitokeza mwenendo usiofaa kwa jamii katika nchi yetu. "Kila tukikaa ndani ya siku mbili ukisikiliza vyombo vya habari wanakwambia kuna unyanyasaji wa kijinsia, mara utasikia baba kamuua mama,mara mama kauawa na mtoto au mama ka...

NHC YATOA SARUJI MIFUKO 75 KUSAIDIA UJENZI WA HOSTELI SINGIDA

Image
Meneja wa Shirika la Nyumb la Taifa (NHC) Mkoa wa Singida, Judith Mwalongo (kulia) kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Fadhili Chimsala, moja ya mfuko wa saruji kati ya 75  yenye thamani ya Sh. Milioni 1.5 iliyotolewa na shirika hilo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Sekondari ya Kintinku iliyopo wilayani Manyoni mkoani Singida leo hii Januari, 25, 2023. Wengine katikati ni dereva wa shirika hilo, Hassan Njiku na Afisa wa shirika hilo, Renalda Mlambo. Na Dotto Mwaibale,   Manyoni SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limetoa mifuko 75 ya saruji yenye thamani ya Sh. Milioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Sekondari ya Kintinku iliyopo wilayani Manyoni mkoani Singida. Akizungumza wakati akikabidhi saruji hiyo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Fadhili Chimsala kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo,  Meneja wa NHC Mkoa wa Singi...

MATUKIO YA MAUAJI WILAYA YA MANYONI WANANCHI WAMLILIA RC SERUKAMBA AWASAIDIE

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Manyoni na Itigi katika kikao cha kusikiliza kero kilichofanyika juzi wilayani humo. Na Dotto Mwaibale,   Singida UTARATIBU wa ziara aliounzisha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba  kwenda kusikiliza kero za wananchi katika wilaya zote mkoani hapa zimekuwa na tija kubwa  kwani zimeibua mambo mengi yakiwemo matukio ya mfululizo ya kuuawa kwa watu wilayani Manyoni. Mauaji ya mfululizo ya watu ambao maiti zao zinaokotwa kila wiki maeneo tofauti ya Wilaya ya Manyoni yamewashtua wananchi wa wilaya hiyo ambao wamelazimika kupaza sauti kumweleza Mkuu wa Mkoa wa Singida,Peter Serukamba, kumuomba aingilie kati na kuwasaidia kuliondoa jambo hilo. Katika hali ya kushangaza,wananchi hao wamesema mauji ya watu ambayo yameibua hofu kubwa kwa jamii baadhi ya pikipiki zinazomilikiwa na askari polisi wa Manyoni kwa ajili kuendesha biashara zao ndizo zinatumika kwenye mauaji hayo. Wananchi wa Manyoni walimwe...