Posts

Showing posts from February, 2023

WANANCHI IBOFWE WAMBEBA MBUNGE NYAMOGA WAKISHUKURU KWA UJENZI WA ZAHANATI, BARABARA

Image
Wananchi wa Kijiji cha Ibofwe, Kata ya Irole wilayani Kilolo mkoani Iringa wakiwa wamembeba Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Justine Nyamoga ikiwa ni kuonesha shukurani zao baada ya mbunge huyo kufanikisha ujenzi wa Zahanati na Barabara katika kijiji hicho. Mbunge Nyamoga alibebwa leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika kijiji hicho. Na Mwandishi Wetu, Kilolo,   Iringa Awali, wananchi wa Kijiji cha Ibofwe, Kata ya Irole Wilayani Kilolo walimuomba Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Justine Nyamoga  ashuke kwenye gari kisha wakampakia kwenye bodaboda. Ilipobaki umbali wa kama kilometa moja hadi kufika eneo la mkutano, wananchi hao wakamuomba ashuke kwenye bodaboda ili wambebe. Haikuwa rahisi kwake kukubali kubebwa lakini kwa sababu yalikuwa ndiyo mapokezi ya wanakijiji, hakuwa na budu kukubali. "Mbunge wetu, kikosi cha mapokezi kipo tayari kukubeba, sisi wananchi tumeamua kukubeba na usihofi hatutakuangusha," alisema mmoja wao huku akipiga saluti. Mwen...

SOKO LA BIDHAA TANZANIA LAPANDISHA BEI YA MAZAO YA WAKULIMA NCHINI

Image
Meneja Uendeshaji Biashara wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Augustino Mbulumi akizungumza katika mafunzo yaliyokuwa yakitolewa kwa waandishi wa habari wa mikoa ya  Dodoma na Singida juzi Februari 22, 2023 (hawapo pichani) kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo iliyochini ya Wizara ya Fedha na Mipango. Na Dotto Mwaibale,   Dodoma MFUMO wa ununuzi wa mazao kwa njia ya mtandao unaoendeshwa na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) umesaidia kupandisha bei ya mazao ya wakulima ambayo uuzwa kwa mnada. Hayo yamebainishwa na Afisa wa Teknolojia ya Habari na Mawasilino (TEHAMA) kutoka TMX, Goodluck Luhanjo wakati akizungumza katika mafunzo yaliyokuwa yakitolewa kwa waandishi wa habari wa mikoa ya  Dodoma na Singida kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango. Alisema katika kipindi cha kuanzia mwaka 2018 hadi 2022  TMX imefanikiwa kuuzwa kwa tani 107,056,619 za bidhaa mbalimbali zenye thamani ...

RC SERUKAMBA AWATAKA WARATIBU KUONGEZA BIDII UTOAJI ELIMU YA VVU

Image
p> Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza na waratibu wa UKIMWI wa Wizara,Mikoa na Halmashauri wakati wa kikao  cha usambazaji wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022. Kutoka kulia ni  Mkurugenzi wa fedha na Utawala wa TACAIDS, Yasin Abasi na kushoto ni Mratibu wa UKIMWI Mkoa wa Singida, Patrick Kasango.   Na Mwandishi Wetu, Singida MKUU wa Mkoa wa Singida,  Peter Serukamba amewaagiza waratibu wa UKIMWI nchini  kuzungumza na jamii kwa uwazi kuhusu mabadiliko ya tabia katika kujikinga na maambukizi ya VVU ifikapo 2030 kuwe na Tanzania isiyokuwa na UKIMWI. Akizungumza leo Februari 20,2023 wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022 iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana aalisema iwapo jamii itaelewa vizuri na ikakubali kubadili tabia Tanzania itafikia malengo ya Dunia ya 2030 ya  kumaliza UKIMWI. Serukam...

MSD YATOA UFAFANUZI DAWA ZILIZOMALIZA MUDA

Image
 Na Mwandishi Wetu BOHARI ya Dawa (MSD) imesema bidhaa za afya, hususani dawa zina utaratibu maalumu wa utunzaji na matumizi yake, ambapo dawa zilizokwisha muda wake wa matumizi haziruhusiwi kusambazwa, wala kutumika ndani ya bohari. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na MSD na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano MSD Etty Kusiluka ilisema bohari imesikitishwa na taarifa iliyotolewa juzi February 18, 2023 Gazeti la Nipashe toleo Na. 0581225 yenye kichwa cha habari “Wagonjwa wapewa dawa zilizoisha muda wa matumizi” katika ukurasa wake wa kwanza na wa pili. “Bohari ya Dawa (MSD) imesikitishwa na taarifa iliyoripotiwa na gazeti hilo ambapo kichwa cha habari cha taarifa hiyo na kile kilichoripotiwa ndani ya taarifa husika haviendani hivyo kusababisha taharuki kwa wananchi, vituo vya kutolea huduma za afya nchini, Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla. Taarifa hii pia imeharibu taswira ya MSD,alisema. Alisema uongozi wa MSD umesikitishwa na upotoshaji huo ambapo kwa mujibu wa...

VETA KANDA YA KATI YATOA MAFUNZO YA UFUGAJI KUKU KWA WAJASIRIAMALI WILAYA YA IKUNGI

Image
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati, John Mwanja akizungumza leo Februari 14,2023 wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wajasiriamali wa kata za Ikungi na Unyahati wilayani Ikungi mkoani Singida. Kutoka kulia ni Afisa Masoko na Utafiti Veta Kanda ya Kati, Sadan Komungoma na Afisa Maendeleo  ya Jamii Wilaya ya Ikungi, Haika Masawe. ............................................................ Na Dotto Mwaibale ,  Ikungi MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Kanda ya Kati imeanza kutoa  mafunzo ya ufugaji wa kuku kisasa kwa wajasiriamali ili kuwawezesha wananchi kuondokane na ufugaji wa mazoea kwenda ufugaji wenye tija utakaowakwamue kiuchumi. Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati, John Mwanja akizungumza leo Februari 14,2023 wakati wa mafunzo hayo kwa wajasiriamali wa kata za Ikungi na Unyahati wilayani Ikungi mkoani Singida ili kuwawezesha wananchi  kufanya ufugaji wenye tija utakaowaongezea kipato. "Mafunzo haya ambayo ni ya kwanza kutolewa katika Chuo cha VETA Ikun...

MWENYEKITI MPYA BODI YA REA AANZA KAZI RASMI NA KUSISITIZA UCHAPAKAZI, UADILIFU

Image
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Nishati Vijijini, Janet Mbene akizungumza na Wajumbe wa Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), juzi Februari 11, 2023 jijini Dar es Salaam. Na Veronica Simba, REA   MWENYEKITI mpya wa Bodi ya Nishati Vijijini, Janet Mbene ameanza kazi rasmi kwa kukutana na kuzungumza na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ambapo amesisitiza uchapakazi, weledi, uadilifu na ushirikiano katika kazi. Katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo, Februari 11, 2023 na kuhudhuriwa pia na Wajumbe wa Bodi, Mwenyekiti amehamasisha kufanya kazi kwa ufanisi ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa katika kuwasaidia wananchi hususan wa vijijini kupata maendeleo. “Tujitahidi sana kufanya kazi vizuri, kwa weledi na kwa wakati huku tukisimamia maeneo ambayo tunapaswa kuyasimamia kwa karibu sana hasa wakandarasi wanaotekeleza miradi mbalimbali,” amesisitiza Mwenyekiti. Akizungumza zaidi, Mbene ameeleza kuwa maendeleo ya kiuchumi yanategemea s...

KAMISAA WA SENSA ANNE MAKINDA: REDIO ZINA UMUHIMU MKUBWA WA KUTOA TAARIFA SAHII ZA MATOKEO YA SENSA

Image
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Tanzania Bara, Anne Makinda, ambaye alikuwa mgeni rasmi akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wahariri wa habari wa redio jamii yanyayohusu matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yanayofanyika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali mkoani hapa ambayo  yameanza leo Februari 10, 2023 na yatafikia tamati kesho. Na Dotto Mwaibale ,  Singida KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Tanzania Bara, Anne Makinda amesema redio zinategemewa sana na wananchi kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali zinazotolewa na Serikali na taasisi zingine zikiwemo za idara ya takwimu. Makinda ambaye alikuwa mgeni rasmi ameyasema hayo leo Februari 10, 2023 wakati akifungua mafunzo ya wahariri wa habari wa redio jamii yanyayohusu matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yanayofanyika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali mkoani hapa ambayo yatafikia tamati kesho.. Alisema redio j...

SUA, TAASISI ZOTE ZA WIZARA YA KILIMO WASAINI MKATABA WA KUINUA KILIMO NCHINI

Image
Wakuu wa Taasisi  zote zilizo chini ya Wizara ya Kilimo zinazojishughulisha na undelezaji wa pembejeo za Kilimo Utafiti na uzalishaji  na wawakilishi wao wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya Taasisi hizo na  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) katikaafla iliyofanyika Februari 9, 2023 mkoani Morogoro. Na Calvin Gwabara,   Morogoro. CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Kilimo zinazojishughulisha na undelezaji wa pembejeo za Kilimo Utafiti na uzalishaji zimesaini mkataba wa mashirikiano ujulikano 'MoU. ambao utasaidia kuongeza ushirikiano katika utendaji wa Taasisi hizo na kuongeza ufanisi na tija katika kilimo nchini. Akizungumza kwenye hafla hiyo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo upande wa Taaluma Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof.  Maulid  Mwatawala kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda alisema awali SUA ilikuwa iing...