SINGIDA YAJIDHATITI KUTUMIA MFUMO WA MSHITIRI KUPATA BIDHAA ZA AFYA
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza na wadau wa Sekta ya Afya wakati akifungua mafunzo ya wawezeshaji wa Mfumo Mshitiri kutoka Halmashauri Saba za mkoa huo katika mkutano uliofanyika mjini hapa Machi 30, 2023. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick na kulia ni Mwezeshaji wa kitaifa wa mfumo huo kutoka Wizara ya TAMISEMI, Emmanuel Mayunga, Na Dotto Mwaibale, Singida MKOA wa Singida umeendelea kujidhatiti na kuongeza ufanisi katika upatikanaji wa huduma bora za afya kwa kutekeleza afua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia mfumo wa Mshitiri kwa bidhaa za afya zinazokosekana Bohari ya Dawa (MSD). Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba wakati akifungua mafunzo ya wawezeshaji wa Mfumo Mshitiri kutoka Halmashauri Saba za mkoa huo ambazo ni Itigi, Iramba, Singida Manispaa, Ikungi, Manyoni, Singida DC na Mkalama. “Kutokana na changamoto na kuibuka kwa hoja mbalimbali za ununuzi wa bidhaa za afya vituoni, Ofisi ya ...