BOHARI YA DAWA (MSD) KANDA YA KATI YAKUTANA NA WADAU WAKE KATIKA KIKAO KAZI
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Kati, John Sipendi, akizungumza na wadau wa MSD katika kikao kazi kilichofanyika wilayani Kondoa mkoani humo Aprili, 29, 2023. ............................................................. Na Mwandishi Wetu, Dodoma BOHARI ya Dawa (MSD) Kanda ya Kati Dodoma imekutana na wadau na wateja wake wakiwemo waganga wakuu, wafamasia na watendaji wa halmshauri kuhakikisha wanajadili uboreshaji wa huduma za afya na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa uhakika ili kupunguza kero kwa wananchi. Katika mkutano huo wadau hao wamekubaliana kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan za maboresho sekta ya afya kwa vitendo kwa kutumia taaluma zao kutoa huduma stahiki. Akizungumza jana wilayani Kondoa mkoani Dodoma Meneja wa MSD Kanda ya Kati, John Sipendi alisema, lengo la MSD kurejesha mikutano hiyo ya pamoja na wadau ni kukubali kukoselewa, kujenga mazingira ya kupunguza changamoto za pande zote mbili, kubadilisha uzoefu na ...