Posts

Showing posts from May, 2023

DC IRAMBA AGUSWA NA ADHA YA WANANCHI KIJIJI CHA MSAI KUKOSA ZAHANATI

Image
Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda (katikati) akishiriki kufyatua matofali wakati wa mfululizo wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya Kata ya Shelui na Mtoa wilayani humo jana May 29, 2023 akiwa ameongoza na wataalam, watendaji wa Kata na Tarafa pamoja  na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama. ......................................................  Na Mwandishi Wetu, Iramba MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amesema atafanya mawasiliano na wahusika wa sekta ya afya ili ziweze kupatika fedha za kumalizia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Msai Kupatikana kwa fedha hizo na kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo kutawaondolea adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kwenda kupata huduma za matibabu maemo mengine. Mwenda ameyasema hayo  wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Kata yaMtoa na Shelui pamojana kusikiliza kero za wananchi ili kuzitafutia u...

RC SINGIDA :UKAMILISHAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NI JAMBO LA KUFA NA KUPONA

Image
 Mkuuwa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkhandi kilichopo wilayani humo leo May 30, 2023. Kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Muragili na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Omari Mande. ........................................................   Na Dotto Mwaibale, Singida MKUU wa Mkoa wa Singida,Peter Serukamba amesema kazi ya kumalizia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya zote mkoani hapa ni la kufa na kupona na kuwa kazi hiyo ifanyike usiku na mchana kutokana na umuhimu wake. Serukamba ameyasema hayo leo May 30, 2023 wakati alipokuwa katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua ukamilishaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na kuhimiza miradi yote iwe imekamilika kabla ya Julai 1, 2023 kwa viwango vinavyotakiwa na kulingana na thamani halisi ya fedha zilizotole...

WACHIMBA MADINI KUANZISHA BENKI KWA LENGO LA KUKOPESHANA

Image
Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wachimbaji Madini Tanzania ( FEMATA) John Bina (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa shirikisho hilo katika kikao cha siku mbili kilicho anza leo May 27, 2023, Ukumbi wa Hotel ya Aqua Mjini Singida ambacho kitafikia tamati kesho. Kulia ni mgeni rasmi wa kikao hicho Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida, Chone Malembo na kushoto ni Mwenyekiti wa Wanawake wachimbaji madini Taifa, Martha Kayaga. ........................................................... Na Dotto Mwaibale, Singida SHIRIKISHO la Vyama vya Wachimba Madini Tanzania (FEMATA) linatarajia kuanzisha benki yao ambayo itatumika kuwakopesha wachimbaji kwa lengo la kuinua sekta hiyo muhimu kiuchumi nchini. Hayo yamesemwa na Rais wa FEMATA,  John Bina wakati akizungumza katika kikao cha siku mbili cha Kamati Tendaji ya shirikisho hilo  ambacho kimeanza leo May 27, 2023 na kufikia tamati kesho May 28, 2023 chenye lengo la kukamilisha mchakato wa kuandika katiba mpya ambayo ita...

DC MWENDA AZINDUA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MASAGI ILIYOJENGWA KWA MIL.99/-

Image
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda  akikoroga uji wa Lishe ulikuwa unagawiwa kwa Watoto waliofika kwenye uzinduzi wa Zahanati ya Kijiji cha Masagi iliyopo Kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui wilayani hapa iliyojenga kwa zaidi ya Sh.Milioni 99 katika hafla iliyofanyika juzi. Na Mwandishi Wetu, Iramba MKUU wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Suleimani Yusuph Mwenda,  amezindua rasmi Zahanati ya Kijiji cha Masagi Kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui wilayani hapa iliyojenga kwa zaidi ya Sh.Milioni 99 ambayo  itahudumia wananchi  3,117 wa  kijiji hicho..  Akizungumza baada ya kuzindua zahanati hiyo,  Mwenda, amewataka wananchi hao kuhudhuria kikamilifu na kupata matibabu katika zahanati hiyo kwani kwa sasa changamoto ya kufuata matibabu kwa mwendo mrefu umeisha. Alisema  kuzinduliwa kwa Zahanati hiyo kutaondoa  kabisa vifo vya akina Mama na watoto  ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata  matibabu Shelui au Mtoa  na katika Hospit...