Posts

Showing posts from June, 2023

MADEREVA MSD WAJENGEWA UWEZO ILI KUTOA HUDUMA KWA UFANISI KATIKA UTENDAJI KAZI WAO

Image
Watumishi wa Kada ya Udereva wa Bohari ya Dawa (MSD) kutoka Makao Makuu na Kanda zote 10 wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo yalioandaliwa na MSD yaliyofanyika mkoani Morogoro. Na Mwandishi Wetu, Morogoro WATUMISHI wa Kada ya Udereva wa Bohari ya Dawa (MSD)  wamepewa mafunzo ya kuwajengea uwezo iliwaweze kutoa huduma bora kwa wateja wakati wa usambazi wa bidhaa za afya. Mafunzo hayo yanayofanyika mkoani Morogoro yamewahusisha madereva wote wa MSD kutoka Makao Makuu na Kanda zote 10 ambazo ni Dodoma, Mtwara, Kilimanjaro, Kagera, Dar es Salaam, Iringa, Tanga, Tabora, Mbeya na Mwanza. Mkufunzi wa mafunzo hayo Kaimu Meneja wa Rasilimali Watu , Adolar Duwe, amesema kuwa mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa Wataalamu wa usambazaji bidhaa za afya kwani yatawawezesha kuongeza uelewa juu ya huduma kwa wateja na namna ya kuhudumia wateja wa MSD. Akizumgumza kwa niaba ya Maderava wa MSD Bw. Erick Kaaya, amesema mafunzo hayo yamewaongezea ujuzi, kujiamini na uelewa wa masuala mbalimbali...

MADINI CHUMVI YALIYOPATIKANA WILAYA YA MANYONI KUWA CHANZO KIPYA CHA MAPATO

Image
 Mkuu  wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota akizungumzia  Madini Chumvi yaliyopatikana Kata ya Majiri Kijiji cha Mpandagani  wilayani humo katika kikao kilichofanyika ofisini kwake jana Juni 23,2023 kuwa ni chanzo kipya cha mapato katika Halmashauri ya wilaya hiyo.  Na Dotto Mwaibale, Manyoni MKUU wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota amesema kuwa Madini Chumvi katika Kata ya Majiri Kijiji cha Mpandagani  yatakuwa chanzo cha mapato katika Halmashauri ya Wilaya hiyo. DC Kemirembe ameyasema haya leo Juni 23,2023 katika kikao cha Kuwasilisha ripoti ya Utafti wa madini hayo uliofanywa na Wataalam kutoka Wizara ya Madini. "Tunawashukuru sana kwa utafiti wenu mliofanya na kutuhakikishia kuwa madini chumvi yanayopatikana ni mazuri na yanafaa kwa kiwango kikubwa kwa matumizi ya binadamu, sisi kama wawakilishi wa Serikali tutahakikisha tunakitumia vizuri chanzo hiki cha mapato kwa manufaa ya jamii lakini pia ili kukuza mapato ya halmashauri YETU”. alisema Kem...

SERIKALI YATAKA WASHAURI WA WANAFUNZI KUWAJENGA WANAFUNZI KATIKA MAADILI MEMA NA UZALENDO

Image
Mkuu waWilaya ya Ikungi,  Mhe. Thomas Apson (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Ushauri na Uelekezi kwa Washauri wa Wanafunzi Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TACOGA 1984), baada ya kufunga mafunzo yaliyohusu namna bora ya kukuza utendaji katika kuwapa ushauri wanafunzi yalioanza Juni, 21, 2023 na kufikia tamati Juni 23,2023 katika Ukumbi wa TIA Kampasi ya Singida. ..................................................  Na Dotto Mwaibale, Singida SERIKALI imewataka washauri wa wanafunzi na viongozi wa serikali za wanafunzi kuendelea kuwajenga wanafunzi katika maadili mema na uzalendo, umoja wa kitaifa ili wawe wabunifu ndani ya mazingira ya maendeleo ya sayansi na teknolojia. Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amesema hayo Juni 23, 2023 wakati wa kufunga mafunzo ya washauri wa wanafunzi na viongozi wa serikali za wanafuzi yaliyoandaliwa na Chama cha Ushauri na Uelekezi kwa Washauri wa Wanafunzi Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania ( TACOGA 1984...

TPHPA KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU NA HUDUMA KWA WANANCHI

Image
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka  ya Afya ya Mimea  na Viuatilifu  Tanzania  (TPHPA)  Prof Joseph Ndunguru (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mamlaka hiyo Mkoa wa Shinyanga baada ya kuzungumza  na Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo mkoani humo. Wa kwanza kutoka kushoto ni  M simamizi wa Kituo cha TPHPA Mkoa wa Shinyanga, Jesca Ndomba,  na wa tatu ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo Na Mwandishi, Wetu , Shinyanga MAMLAKA  ya Afya ya Mimea  na Viuatilifu  Tanzania  (TPHPA)  imesema itaendela kuboresha miundombinu yake na huduma kwa wananchi hili waweze kupata tija katika sekta ya kilimo kama ilivyo dira na dhima ya Wizara ya Kilimo.  Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Prof Joseph Ndunguru wakati  akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo Mkoa wa  Shinyanga na kuwataka kufanya kazi kwa weledi na kufuata maadili ya kazi...

BOHARI YA DAWA (MSD) YAANZA RASMI ZOEZI LA KUHESABU MALI

Image
Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) wakiendelea na zoezi la kuhesabu malikatika maghara yao.   Na Dotto Mwaibale,    BOHARI  ya Dawa (MSD) imeanza rasmi zoezi la kuhesabu mali kwa mujibu wa sheria. Zoezi hilo la kuhesabu mali  linategemewa kukamilika  mwishoni  mwa mwezi Juni 2023 ili kuanza mwaka mpya wa fedha.   Katika kipindi hiki maghala yote ya MSD Makao Makuu pamoja na Kanda zote  yatakuwa yamefungwa kupisha zoezi hilo.   Awali kabla ya kuanza kwa zoezi hilo Bohari ya Dawa (MSD) iliwaarifu wateja wake wote wa Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kuwa  kuanzia Juni 15, 2023 mpaka Juni 30, 2023 litafanyika zoezi la kuhesabu mali kwa mujibu wa sheria na kuwa kutokana na zoezi hilo la kuhesabu mali, maghala yote ya MSD yatafungwa kwa kipindi cha wiki mbili kuanzia Juni, 15, 2023. Maombi yote ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara yawasilishwe MSD kabla ya Juni 7, 2023, ili kukidhi mahitaji wakati wote m...

MEJA JENERALI MBUGE “TUIMARISHE USHIRIKIANO KUKABILI MAJANGA”

Image
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja  Jenerali  Charles Mbuge  akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Watalam waliokutana kwa lengo la Kuhuisha na Kutafsiri Mwongozo wa Utekelezaji wa Dhana ya Afya Moja mkoani Singida.  Na Mwandishi Wetu - Singida   Serikali  kupitia  Ofisi  ya Waziri Mkuu imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano na sekta mbalimbali katika kukabiliana na maafa ili kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira salama. Kauli hiyo imetolewa   mkoani Singida na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja  Jenerali  Charles Mbuge  wakati akifungua kikao kazi cha Watalam waliokutana kwa lengo la Kuhuisha na Kutafsiri Mwongozo wa Utekelezaji wa Dhana ya Afya Moja. Meja Jenerali Mbuge amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la mwingiliano wa binadamu, wanyama na mazingira ambao  husababisha  kutokea kwa magonjwa mbalimbali yanayo...

TMDA KANDA YA KATI YATOA ELIMU YA UTOAJI TAARIFA YA MADHARA YA DAWA MKOANI SINGIDA

Image
Zoezi la Uelimishaji na uhamasishaji wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa ukifanyika Hospitali ya Kiomboi wilayani Iramba mkoani Singida. Na Dotto Mwaibale, Singida MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Kati imefanya uelimishaji na uhamasishaji wa utoaji wa taarifa za madhara yanayohisiwa kusababishwa na dawa katika Halmashauri za Wilaya ya Iramba na Manyoni mkoani Singida. Akizungumza wakati wa zoezi la uelimishaji lililofanyika kwa nyakati tofauti wiki hii, Mkaguzi wa Dawa kutoka TMDA, Seraphina Omolo alisema lengo kubwa ilikuwa ni kutoa uelimishaji na uhamasishaji wa utoaji wa taarifa za madhara yanayohisiwa kusababishwa na dawa,chanjo na vifaa tiba katika maeneo ya kutolea huduma za afya ikiwemo hospitali, vituo vya afya na zahanati. ‘”Zoezi hili liliwalenga watoa huduma za afya kuhusu utoaji wa  taarifa za madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya dawa, chanjo na vifaa tiba ili kuendelea kulinda afya ya jamii,” alisema Omolo. Omolo alisema katika mafunzo hayo,...

DIWANI ITIGI ADAIWA KUZUIA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, akipokea taarifa ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Isanjandugu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya Juni 7, 2023. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ilimbato Japhet,  aliotoa taarifa hiyo na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota.  Na Dotto Mwaibale, Itigi UONGOZI wa Wilaya ya Itigi mkoani Singida, umemlalamikia Diwani wa Kata ya Mitundu, Patrick Masanja  kwa madai ya kukwamisha utekelezwaji wa miradi ya maendeleo katika kata hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota alisema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba katika mfululizo wa ziara yake ya kukagua na kuhamasisha ukamilishaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali wilayani humo Juni 7, 2023. Kemirembe alisema kuwa diwani huyo Patrick Masanja amekuwa akiwazuia wananchi kutokushiriki shughuli za maendeleo mbalimbali zinapofanyika katika kata hiyo. "...