Posts

Showing posts from July, 2023

DC SINGIDA : WAFANYABIASHARA VIPODOZI SHIRIKIANENI NA SERIKALI KATIKA KUDHIBITHI VIPODOZI VYENYE SUMU

Image
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili, akizungumza na Wafanyabiashara wa Vipodozi Mkoa wa Singida Julai 27, 2023, wakati akifungua kikao cha TBS na wafanyabiashara hao cha kutoa elimu juu ya uelewa kuhusu vipodozi vyenye viambata sumu. ....................................................... Na Dotto Mwaibale, Singida MKUU wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mragili amewataka wafanyabiashara wa vipodozi mkoani hapa kushirikiana na Serikali pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kudhibiti bidhaa zenye viambata vyenye sumu. Mragili alitoa ombi hilo wakati akifungua kikao cha TBS na wafanyabiashara cha kutoa elimu juu ya uelewa kuhusu vipodozi vyenye viambata sumu Mkoa wa Singida. Hatua ya TBS kutoe elimu hiyo ilifuatia maombi yaliyotolewa na wafanyabiashara hao kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mwezi Mei, 2023 wakati maafisa wa TBS walipoanzisha operesheni ya kupita katika maduka ya vipodozi kwa lengo ya kuondoa bidhaa hizo katika soko ambazo zinaathari kwa binadamu....

RC SINGIDA: NIT- KIFANYENI CHUO CHENU KUWA MAHALI SAHIHI PA KUPATIA MAFUNZO STAHIKI

Image
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Mhandisi Profesa Zacharia Mganilwa, akimkabidhi zawadi Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida, Goodluck Mwangomango kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa  kozi ya Maafisa Usafirishaji na Madereva Wakuu wa Taasisi za Umma na Halmashauri zote hapa nchini uliofanyika Julai 26, 2023 katika Ukumbi wa RC Misheni mjini hapa.  Kulia ni  Mkuu wa Kituo cha Mafunzo Endelevu cha NIT, Bahati Mabina. ........................................................ Na Dotto Mwaibale, Singida   MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ametoa wito kwa Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuendelea kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili kukifanya chuo hicho kuwa mahali sahihi pa kupatia mafunzo stahiki.  Wito huo umetolewa na Serukamba kwa niaba yake na Katibu Tawala Wilaya ya Singida, Goodluck Mwangomango wakati akizindua kozi ya Maafisa Usafirishaji na Madere...

MBUNGE GEKUL: WANANCHI KUWENI WATULIVU SERIKALI IPO KWENYE MCHAKATOTO WA KUANDAA FIDIA ZENU

Image
Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul, akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi katika ziara yake aliyoianza hivi karibuni jimboni humo. ...................................................... Na Mwandishi Wetu, Babati MBUNGE wa Jimbo la Babati Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul amewataka wananchi ambao nyumba zao zitapitiwa na ujenzi wa njia ya ‘Bypass’ kuwa watulivu kwani Serikali ipo kwenye mchakato wa kuandaa fidia zao. Gekul ameyataja  maeneo yatakayo athirika na ujenzi huo ni pamoja na Mitaa ya Hangoni,Kwere,Mrara na Wang'waray. Akizungumza wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ambayo ameianza baada ya vikao vya bunge la bajeti kumalizika hivi karibuni Gekul amesema kuanzia mwezi wa Septemba waathiriwa wa kupisha ujenzi huo ambao tayari wamekwisha tambuliwa baada ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kufanya t...

WATAALAM SEKTA YA AFYA BABATI WATOA CHANGAMOTO ZAO KWA MBUNGE GEKUL, WANUFAIKA WA TASAF NAO WAIBUKA

Image
Mmoja wa Wataalam wa Sekta ya Afya Hospitali ya Mji Babati mkoani Manyara akielezea changamoto walizonazo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi. ............................................... Na Mwandishi Wetu, Babati WATAALAM wa Afya wa Hospital ya Mji Babati mkoani Manyara wametoa malalamiko yao kwa Mbunge wa Jimbo la Babati Mji Pauline Gekul kutokana na changamoto wanazozipitia kwenye masuala  ya kiutumishi. Wataalam hao wametoa malalamiko hayo baada ya kukutana na mbunge huyo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi, ziara ambayo anaifanya jimbo jimbo lote baada ya kumalizika kwa vikao vya bunge la bajeti hivi karibuni. Baadhi ya malalamiko waliolalamikia ni ufinyu wa kikokoteo baada ya kustaafu, kutopandishiwa mishahara baada ya kumaliza masomo Yao pindi wakiwa Kazini pamoja na kucheleweshewa kwa pindi wanapohamishwa vituo vya...

BOHARI YA DAWA (MSD) MFANO WA KUIGWA JUMUIYA YA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA (SADC)

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)  Mavere Tukai, akizungumza na wakuu   wa Taasisi za Bohari ya Dawa pamoja na viongozi wanaosimamia manunuzi ya bidhaa za afya katika  Jumuia ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya kufanyika kwa mkutano wa siku mbili kwa viongozi hao uliofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 10, 2023 na kufikia tamati Julai 12, 2023 kwa wakuu hao kutembelea MSD kujionea shughuli mbalimbali zinavyofanyika zikiwamo za kuhifadhi Dawa na Vifaa Tiba.   ................................................. Na Mwandishi Wetu   WAKUU wa Taasisi za Bohari ya Dawa pamoja na viongozi wanaosimamia manunuzi ya bidhaa za afya katika  Jumuia ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wameeleza kuwa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) imekuwa mfano wa kuigwa katika nchi za jumuiya hiyo. Aidha wamesema MSD itakuwa chachu ya kuunganisha maendeleo na kukuza uchumi wa Afrika kutokana na ufanisi wake katika  upatikanaji wa uhakika wa dawa na...

AFISA VIJANA SINGIDA AWAPONGEZA WAZAZI KWA UTOAJI WA CHAKULA SHULENI

Image
Afisa Vijana Mkoa wa Singida  Frederick Ndahani (wa pili kushoto) akiwa na wajumbe wa Kamati ya Lishe wa Shule ya Msingi Nkalankala na Shule ya Sekondari ya Set Benjamin wakati akikagua chakula kilichopatikana kwa ajili ya wanafunzi wa shule hizo.  Na Mwandishi Wetu, Singida   AFISA Vijana Mkoa wa Singida  Frederick Ndahani ameupongeza Uongozi wa Shule ya Msingi Nkalankala na Shule ya Sekondari ya Set Benjamin pamoja na wazazi  wa Kata ya Nkalankala kwa kuamua kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni. Ndahani ameyasema hayo wakati akifuatilia Ufundishaji na hali ya utoaji wa chakula shuleni katika Shule za Msingi na Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida. Ndahani amewapongeza wazazi waliounda kamati ya Lishe ya shule na kusimamia ,utoaji wa elimu ya umuhumu wa chakula,ukusanyaji,utunzaji na upishi ambapo hadi sasa Shule ya Msingi Nkalankala imekusanya jumla ya magunia 90 ya Mahindi, maharage gunia 20 na mafuta ya chakula lita 350 na Shule ya Sekon...

MBUNGE NGASSA: WANANCHI MSITETELEKE MPO SALAMA KWENYE MIKONO YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Image
Wakina mama wakimlaki Mbunge wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora, Nicholaus Ngassa wakati wa ziara yake aliyoifanya jimboni humo mara baada ya vikao vya Bunge la Bajeti kumalizika hivi karibuni, ambayo ilikwenda sanjari na mikutano ya hadhara.  Na Mwandishi Wetu, Igunga   MBUNGE wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora Mhe. Nicholaus Ngassa amewaomba wananchi wa jimbo hilo kutoteteleka  kwa kauli mbalimbali za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu, kuhusu maendeleo na kuwahakikishia kuwa chini ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samoa Suluhu Hassan  wapo kwenye mikono salama na waendele kupokea miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kupitia Ilani ya Chaka hicho.  Ngassa ametoa kauli  hiyo wakati akizungumza na Wananchi kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara aliyofanya katika Vijiji na Vitongoji vya Kata ya Kinungu. "Kinungu tumeleta umeme, barabara, maji ya visima  ujenzi wa miundombinu ya madarasa kwa shule zote za sekondari na msingi ...

WAKUU WA TAASISI ZINAZOSIMAMIA MANUNUZI BIDHAA ZA AFYA NCHI ZA SADC WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM, KESHO KUTEMBELEA MSD

Image
Wakuu wa Taasisi zinazosimamia Manunuzi ya Bidhaa za Afya kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana jijini Dar es Salaam jana Julai 10, 2023 katika mkutano wa siku tatu. Na Mwandishi Wetu WAKUU wa Taasisi zinazosimamia Manunuzi ya Bidhaa za Afya kwa nchi za SADC wamekutana jana Julai 10, 2023 jijini Dar es Salaam, kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha mpango wa manunuzi ya pamoja ya bidhaa za afya kwa nchi za ukanda wa Kusini mwa Africa-SADC (SPPS). Washiriki hao pamoja na mambo mengine watajadili namna bora ya kutekeleza mpango wa manunuzi ya pamoja ili kuweza kutekeleza mpango huo kwa ufanisi zaidi na kujadili mapendekezo yaliyotolewa na mshauri mwelekezi. Nchi 16 Wanachama  wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambazo  ni wanachama wa mpango huo wa manunuzi ya bidhaa hizo za afya ni   Angola , Boswana, Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo , Lesotho, Madagascar,...