Posts

Showing posts from August, 2023

BENKI YA CRDB YAJA NA HATIFUNGANI YA KIJANI

Image
Na Selemani Msuya  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo ametoa rai kwa wananchi, kampuni za sekta binafsi na umma, taasisi za serikali kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza katika hatifungani ya kijani au “Green Bond” ya Benki ya CRDB. Profesa Kitila ametoa raia hiyo leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Hatifungani ya Kijani uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu wa kada mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Amesema uamuzi wa Benki ya CRDB kuja na hatifungani hiyo ya kijani na kutoa fursa kwa wananchi na taasisi mbalimbali kununua hisa na fedha zitakazopatikana kuelekezwa kwenye miradi ya mazingira ni wa kuigwa na taasisi nyingine kwani unaenda kusaidia serikali kutekeleza miradi mingi. Kitila amesema serikali ina mipango mingi ya kuhakikisha miradi ya kuzuia uharibifu wa mazingira unaosababishwa mabadiliko ya tabianchi kutokea, hivyo ujio wa Kijani Bond ni wazi kuwa lengo hilo litaweza kutumia. "Kijani Bond i...

MSD KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa  (MSD), Mavere Tukai ......................................................... Na Mwandishi wetu- Dodoma     BOHARI ya Dawa (MSD) imewahakikishia wananchi huduma bora    zinazokidhi   viwango vya Kimataifa kutokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha utendaji wake. Akieleza hatua hizo   Agosti 24, 2023 jijini Dodoma wakati wa mahojiano maalum na Idara ya Habari (MAELEZO), Mkurugenzi Mkuu wa Bohari hiyo Bw. Mavere Tukai amesema, MSD inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa maghala   ya kisasa ya kuhifadhi bidhaa za afya katika mikoa   mitano ikiwemo   Dodoma na Mtwara ambapo mkandarasi ameanza kazi ya ujenzi. “Mradi huu hapa jijini Dodoma na kule mkoani Mtwara inagharimu shilingi Bilioni 39 ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa maghala matano tuliyopanga kujenga katika Ofisi za Kanda katika mikoa ya Mwanza, Kagera na Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha huduma ze...

LATRA YAIAHIDI KAMATI YA BUNGE KUBORESHA SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI, YATOZA FAINI MABASI SH. MIL.1, 250,000/-

Image
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), CPA Habib Suluo. ........................................................................ Na Dotto Mwaibale, Singida   MKURUGENZI Mkuu  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), CPA Habib Suluo, ameihakikishia Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuwa mamlaka hiyo itaendelea kutekeleza majukumu yake kikamilifu kwa kuboresha shughuli za usafirishaji nchini na kuwapima madereva ili waendeshe vyombo vya moto kwa usalama zaidi. Suluo aliyasema hayo baada ya Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge, Miraji Mtaturu, kuipongeza LATRA kwa kusimamia mfumo utoaji wa tiketi kwa mtandao ambao umeanza kupunguza kero kwa abiria. '' Tutaendelea kutekeleza majukumu yetu kwa ukamilifu na kuufanyia kazi ushauri uliotolewa na Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa lengo la kuboresha shughuli za usafirishaji ikiwemo kuendelea kuwatahini madereva ili kuhakikisha abiria wanasafiri kwa usalama,''. alisema Suluo wakati akiwasilisha taarifa...

KAMPUNI YA JOSTANO TRANS KINARA SEKTA YA USAFIRISHAJI NCHINI

Image
Mabasi ya Kampuni ya Jostano and General Supplises Limited yakiwa Stendi ya Mabasi ya Mkoa wa Singida Misuna tayari kwa safari zake. .................................................................................. Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam KAMPUNI ya Jostano and General Supplises Limited licha ya kuanza kufanya kazi  hivi karibuni imekuwa kinara katika sekta ya usafirishaji hapa nchini hususani katika Mikoa ya Singida, Manyara, Morogoro, Dar es Salaam, Dodoma na Mbeya. Licha ya kuwa na miaka miwili katika sekta hiyo tangu ianze kufanya kazi zake mwaka 2021 kampuni hiyo imejizolea umaarufu mkubwa kutokana na utoaji wa huduma zake kwa viwango vya hali ya  juu na kuwa kimbilio la abiria wengi. Mfanyabiashara Margaret Ntandu ambaye anasafirisha mchele kati ya Mkoa wa Tabora kupitia Singida anasema amekuwa akisafirisha bidhaa hiyo kupitia mabasi ya kampuni hiyo na haja wahi kupata changamoto yoyote. '' Nimekuwa nikisafirisha mizigo yangu kutoka Singida kwenda Dodoma ...

RAIS DK.SAMIA SULUHU HASSAN AIPA TANO MSD KWA UFANISI WA KAZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Dk.Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023. ..................................................  Na Mwandishi Wetu, Arusha RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ameridhishwa na mabadiliko yanayoendelea Bohari ya Dawa ( MSD) na kuwataka waendeleee kuchapa kazi. Rais Samia amesema hayo  Jumamosi Agosti 19, 2023 jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na taasisi za umma. Rais Dk.Samia akiwa amemsimamisha Mkurugenzi wa MSD, Mavere Tukai alisema taasisi hiyo ni kati ya mashirika yaliyo badilika na matumaini yake itakwenda kufanya vizuri hasa katika mfumo wa  uuzaji wa Dawa Afrika kwa kuwa na soko kubwa hususani kwa nchi za Kusini mwa Jangw...

MSD YATAKIWA KUONGEZA SPIDI YA USAMBAZAJI WA BIDHAA ZA DAWA

Image
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu  akijibu maswali ya Wajumbe wa Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI  wakati kamati hiyo ilipokuwa ikipokea taarifa ya usambazaji wa bidhaa za Afya kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai katika kikao cha Kamati kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma. jana. ..................................................... Na WAF, Dodoma   KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI imeitaka Bohari ya Dawa (MSD) nchini kuongeza kasi ya usambazaji wa bidhaa za Dawa pamoja na kuwa na maghala ya dawa katika kila Halmashauri. Wito huo umetolewa leo Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI, Mhe. Stanslaus Nyongo baada ya kupokea taarifa ya usambazaji wa bidhaa za Afya kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bw. Mavere Tukai katika kikao cha Kamati kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma. “Kwanza naipongeza sana Wizara kwa hatua mnazoendelea kuchukua za kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa z...

SHILINGI BILIONI 5 ZATENGWA NA MFUKO WA KUWAWEZESHA WASANII NA WAIGIZAJI MKOANI MBEYA

Image
  Afisa Utamaduni Mkoa wa Mbeya Victoria Shao akizungumza katika kikao maalumu kilichowahusisha Wasanii, Waigizaji na waimbaji kilicho andaliwa na Wizara ya Utamadunim Sanaa na Michezo. ............................................................ Na M wandishi Wetu Mbeya   KIASI cha Shilingi Bilioni 5 kimetengwa na mfuko wa wizara ya sanaa na utamaduni ili kuwawezesha wasanii na waigizaji wa "Bongo Movie" wa mkoa wa Mbeya. Akizungumza katika kikao maalumu kilichowahusisha Wasanii, Waigizaji na waimbaji wa mkoa wa Mbeya na Songwe Afisa Mtendaji Mkuu [CEO] wa mfuko huo Nyakaho Mahemba amesema Wizara imeanza kutoa fedha hizo kwa wasanii kuanzia Desemba 2022 ambapo  imelenga kukuza na kuendeleza kazi za wasanii kujiendesha kibiashara badala ya burudani pekee. Mahemba amesema katika mpango wa serikali ni kuongeza ajira na kuongeza mitaji kwa wasanii kupitia mafunzo na kuongeza ubora  wenye lengo la kukidhi soko la ndani na nje ya nchi. Amefafanua kuwa wasanii wana uwezo ...

WANANCHI WAFURIKA BANDA LA TARI, KUJIFUNZA TEKNOLOJIA ZA KILIMO MAONYESHO YA NANENANE NGONGO LINDI

Image
 Wananchi wakiwa wamefurika katika Banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo kwenye Maonyesho ya Nanenane 2023 yanayofikia tamati leo Agosti 8, 2023 viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. ...........................................................   Na Dotto Mwaibale, Lindi   WANANCHI kutoka Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma wakiwa wamefurika katika Banda la Taasisi ya Utafiti kwa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele mkoani Mtwara kwenye Maonyesho ya Nanenane 2023 Kanda ya Kusini yanayofanyika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi kujionea na kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo. Katika Maonesho hayo watafiti wa kilimo wa TARI wanaonesha na kutoa elimu za teknolojia za kilimo za kuvutia jambo lililosababisha banda hilo kufurika wakulima na wananchi kwa lengo la kujifunza. Akizungumza na waandishi wa habari katika banda hilo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo hicho Dk. Fortunus Kapinga kuhusu maonesho hayo Mtafiti wa Kili...

DC LINDI AWATAKA WASANII KUCHANGAMKIA BILIONI 20 ZA MFUKO WA UTAMADUNI ZILIZOTOLEWA NA RAIS

Image
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shahibu Ndemanga akizungumza wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo  wadau wa utamaduni na sanaa Mkoa wa Lindi iliyoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo mkoani humo jana. ............................................ Na Dotto Mwaibale, Lindi   WASANII mkoani Lindi wametakiwa kuchangamkia fedha Sh.Bilioni 20 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kama ruzuku za kuwawezesha kukopa ili kuwasaidia kuinua vipato vyao kupitia kazi zao za sanaa. Ombi hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shahibu Ndemanga wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo  wadau wa utamaduni na sanaa Mkoa wa Lindi iliyoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. "Hizi fedha zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili yenu hivyo changamkieni fursa hiyo kwa kuboreha shughuli zenu ili muweze kujikwamua kiuchumi," alisema Ndemanga. Alisema wadau wa Sanaa watakaokidhi vigezo vilivyoweka ndio watakaokopeshwa fedha hizo kupitia mfuko ulioanzis...