Posts

Showing posts from September, 2023

WILAYA YA MKALAMA WAPOKEA MWENGE WA UHURU 2023 KUTOKA IRAMBA, WAPONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI

Image
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali (kulia) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda baada ya kumaliza mbio zake wilayani humo Septemba 23, 20223 katika makabidhiano yaliyofanyika Viwanja vya Chuo cha Ufundi cha FDC kilichopo Kata ya Msingi wilayani humo. .............................................................................. Na Dotto Mwaibale, Mkalama WILAYA ya Mkalama mkoani Singida imepokea Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 kutoka Wilaya ya Iramba  mapokezi yaliyofanyika Septemba 23, 2023 Kata ya Msingi wilayani humo na kupongezwa kwa utekelezaji wa miradi ambapo kesho alfajiri Septemba 24, 2023 utakabidhi mbio hizo Wilaya ya Singida DC. Akizungumza wakati akiupokea Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali  alisema ukiwa wilayani humo utatembelea, utakukagua, kufungua, kuzindua na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi mbalimbali yenye thamani ya Sh. Bilioni 1.7. " Mwenge wa Uhuru ukiwa katika wilaya yetu uta...

SATF YAIPIGA JEKI WILAYA YA IKUNGI KUUNDA KAMATI ZA MTAKUWWA KATIKA KATA KUMI

Image
Meneja Miradi wa Taasisi ya Social Action Trust Fund (SATF) Nelson Rutabanzibwa (kulia) akizungumza na wajumbe wa kamati za Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne yaliyoanza Septemba 12, 2023 Wilaya ya Ikungi mkoani Singida na kufikia tamati Septemba 15, 2023.  .................................................. Na Dotto Mwaibale, Singida   TAASISI ya Social Action Trust Fund (SATF) iliyoanzishwa kwa udhamini wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Serikali ya Marekani (USAID) na kuratibiwa na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kusaidia juhudi za Serikali katika kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu waweze kuzifikia ndoto zao limeiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida kuunda kamati za Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) katika kata kumi.. Uundwaji wa kamati hizo katika kata hizo ulienda sanjari na wajumbe waliot...

VETA KANDA YA KATI YATOA MAFUNZO YA UFUGAJI WA MBUZI, KONDOO WILAYA YA IKUNGI BAADA YA KUBAINI SOKO LA UHAKIKA

Image
Afisa Masoko na Utafiti Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Kanda ya Kati, Sadan Komungoma (katikati) akizungumza na wajasiriamali wakati wa mafunzo ya ufugaji wa mbuzi na kondoo yaliyoandaliwa na VETA kwa wananchi wa Kata ya Unyahati wilayani Ikungi yaliyofanyika Septemba 13, 2023 Chuo cha VETA Ikungi mkoani Singida. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Eva Myula na kushoto ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Ladslous William Mwalimu kutoka VETA Singida. ..........................................................................  Na Dotto Mwaibale, Ikungi   MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Kanda ya Kati inaendelea kutoa mafunzo ya ufugaji wenye tija wa mbuzi na kondoo kwa wajasiriamali wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ili waondokane na ufugaji wa mazoea kwenda kwenye ufugaji wa kibiashara ambao utawakwamua kiuchumi.  Afisa Masoko na Utafiti VETA Kanda ya Kati, Sadan Komungoma, akizungumza leo Septemba 13, 2023  ...