Posts

Showing posts from January, 2024

TAKUKURU SINGIDA YAOKOA ZAIDI YA SH.MILIONI 156 ZA MIRADI YA MAENDELEO

Image
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Singida, Sipha Mwanjala akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Januari 31, 2024 ya utendaji kazi kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2023. ............................................................ Na Dotto Mwaibale, Singida   TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imeokoa zaidi ya Sh.Milioni 156 baada ya kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Sipha Mwanjala akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Januari 31, 2024 ya utendaji kazi kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2023 alisema miradi iliyofuatiliwa ilikuwa ni 11 yenye thamani ya zaidi ya Sh.B ilioni 5 katika sekta za Elimu na Afya. Mwanjala alisema miradi hiyo inajumuisha ujenzi wa Shule za Sekondari za Kutwa na za Kata iliyotekelezwa kupitia mradi wa kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambao unahusisha ujenzi na ukarabati wa Shule za Sekondari...

KIKAO KAZI CHA KUJADILI RASIMU YA TAARIFA YA TATHMINI YA USHIRIKI WA WATANZANIA KATIKA MIRADI YA KIMKAKATI NCHINI CHAANZA SINGIDA

Image
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Anderson Mutatembwa akifungua kikao kazi cha wataalam cha kujadili Rasimu ya Taarifa ya Tathmini ya Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati Uwekezaji inayotekelezwa nchini kilichofanyika Mkoani Singida, tarehe 29 Januari, 2024.   ..................................................... Na Mwandishi Wetu, Singida   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Anderson Mutatembwa, ameongoza kikao kazi cha wataalam kujadili Rasimu ya Taarifa ya Tathmini ya Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati Uwekezaji inayotekelezwa nchini kilichofanyika Mkoani Singida Januari 29, 2024.   Bw. Mutatembwa, alisema  dhana ya Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati yaani (Local content) ni dhana inayolenga katika kuhakikisha kuwa thamani ya ziada inayopatikana kwenye uchumi kutokana na utekelezaji wa miradi ya kimkakati na uwekezaji inabaki nchini na kuchangia ukuaji wa u...