Posts

Showing posts from February, 2024

KUNA UMUHIMU WA MIFUKO YA KUHIFADHIA DAMU KUDUMU KWA MUDA WA MIEZI 5 MPAKA 9

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai ........................ Na Mwandishi Wetu.   BOHARI ya Dawa (Msd), imesema kuna haja ya kuwa na akiba ya mifuko ya kuhifadhia damu itakayodumu kwa kipindi cha kuanzia miezi mitano hadi tisa, kuepuka kuadimika kwa bidhaa hizo.   Kauli hiyo ya MSD inakuja katika kipindi ambacho, akiba ya mifuko hiyo kwa sasa ni miezi mitatu, jambo linalopaswa kuongezeka kutokana na ongezeko la mahitaji ya damu linalosababishwa na ajali.   Akizungumza jana Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai  wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wataalamu wa Maabara, alisema MSD inaona kuna haja ya kutafuta mbinu thabiti itakayowezesha kuwa na akiba kubwa ya mifuko na hivyo kuwa na uhakika wa upatikanaji wa damu salama kwa wananchi.   Alisisitiza kuwa, damu ni suala linaloamua maisha ya watu na mahitaji yake ni muhimu hasa kwa wajawazito, hivyo kuna haja ya kuhakikisha inapatikana kwa uhakika.   Katika kufanikisha hilo, alisema kuna h...

KAMPUNI YA BIVAC YAHIMIZA WAKULIMA SINGIDA KUCHANGAMKIA KILIMO CHA MAHARAGE LISHE

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bivac Company Ltd Lishe yenye makao makuu yake Arusha, Beatrice Alban akionesha maharage Lishe yanayouzwa na kampuni hiyo. .................................................. Na Dotto Mwaibale, Singida KAMPUNI ya Bivac Company Ltd Lishe yenye makao makuu yake Arusha imewaomba wakulima Mkoa wa Singida kuchangamkia fursa ya kuanzisha kilimo cha maharage lishe na kuwa itawasaidia kuwatafutia soko. Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo , Beatrice Alban hivi karibuni mjini Singida wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kilimo cha maharage hayo ambayo ni muhimu kwa masuala ya lishe. Alban alisema wamefika Mkoa wa Singida kupeleka   fursa yenye faida zaidi ya tatu ya kwanza ikiwa inahusu masuala ya lishe ambayo imekuwa ni changamoto kubwa kuanzia ngazi ya familia hadi jamii ambapo Seikali imeiona na ya pili ni uchumi hasa kwa mkulima ambaye kila siku amekuwa hapigi hatua na badala yake amekuwa akirudi n...

MSD MBEYA YATAMBUA USHIRIKIANO WA WADAU

Image
    Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa (katikati) akimkabidhi cheti Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Enock Mwambalaswa (kulia) kwa niaba ya  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera iliyotunukiwa halmashauri hiyo baada ya kuwa ya kwanza kufuatia vituo vyake vya afya kutokuwa na madeni inayodaiwa na MSD pamoja na  kutumia vyanzo vingine vya fedha mbali ya zile zinazo tolewa na Serikali kama ruzuku kwa ajili ya kununua bidhaa za afya. Hafla ya makabidhiano ya tuzo na vyeti hivyo ilifanyika Februari 9, 2024 sanjari na mkutano wa wadau na MSD. Kusshoto ni Meneja wa MSD Kanda ya Mbeya Marco Masala. ........................................................          Na Dotto Mwaibale, Mbeya BOHARI ya Dawa (MSD)  imewatambua na kuwapongeza wadau wake wa Kanda ya Mbeya kwa ushirikiano na umahiri wao kwenye suala zima la kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya kwenye maeneo yao. Akizungumza Februri 9, 2024 katika mkutano huo wa wadau n...

KITUO CHA AFYA MSANGE CHAKUMBUKWA, MSD YAPELEKA VIFAA TIBA VYA SH.MIL- 150

Image
Afisa Mauzo  wa MSD Kanda ya Dodoma, Omari Mosi akizungumza kwa niaba Meneja wa MSD wa kanda hiyo,  Mwanashehe Jumaa wakati akikabidhi jenereta la dharura litakalotumika katika Kituo cha Afya Msange kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida Februari 7, 2024  ................................................. Na Dotto Mwaibale , Singida SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imekikumbuka Kituo cha Afya cha Msange kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida kwa kutoa fedha jumla ya Sh.Milioni 150 kwa ajili ya kununua vifaa tiba. Afisa Mauzo  wa MSD Kanda ya Dodoma, Omari Mosi akizungumza kwa niaba Meneja wa MSD wa kanda hiyo,  Mwanashehe Jumaa wakati wa kukabidhi jenereta la dharura litakalotumika katika kituo hicho lenye thamani ya Sh.Milioni 65.7 alisema kati ya fedha hizo zilizotolewa tayari wamekwisha peleka vifaa vyenye thamani ya Sh.Milioni 98.3. "Vifaa vingine vilivyobaki vitaendelea kupelekwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu MSD itahakikisha vin...

KAMATI YA KUDUMU YA AFYA YA BUNGE YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA MSD

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavere Tukai, akitoa taarifa   ya hali ya utendaji na majukumu ya MSD kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI jijini Dodoma.,  .............................................. Na Mwandishi Wetu, Dodoma KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI imesema imeridhishwa na hali ya utendaji wa Bohari ya Dawa(MSD) na mipango ya utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo uzalishaji wa dawa ili kupunguza kununua dawa nje ya nchi. Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI, Mhe. Stansilaus Nyongo baada ya kupokea taarifa ya hali ya utendaji na majukumu ya Bohari ya Dawa (MSD), ambapo ameichagiza MSD kuongeza ufanisi, ubunifu wa hali ya juu kwa kuhakikisha bidhaa za afya zinakuwa toshelevu na kusambazwa. Kwa upande mwingine Mwenyekiti ameshauri MSD kufuatilia na kukusanya madeni ili kuhakikisha inajiendesha vizuri bila kuathiri mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya na kuon...