WAKULIMA WA VIAZI IKUNGI WALIA NA MADALALI, DC ATOA NENO
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro akizungumza na Wananchi wa wilaya hiyo katika moja ya mikutano yake iliyofanyika hivi karibuni. Na Thobias Mwanakatwe, Ikungi WAKULIMA wa kata saba zinazolima viazi vitamu wilayani Ikungi mkoani Singida wamelalamikia kukithiri kwa vitendo vya wafanyabiashara na madalali kununua mazao yao kwa kutumia vipimo vya lumbesa visivyokubalika kisheria. Malalamiko hayo yalitolewa juzi na viongozi wa kata ya Puma wakati Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro, alipofanya mkutano na madiwani, wenyeviti wa vijiji, vitongoji, watendaji na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi kwenye maeneo yao. Kata zinazolima viazi katika Wilaya ya Ikungi ni Puma, Kituntu, Ihanja, Isyeke,Makiungo, Dung'unyi na Ikungi. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) kata ya Puma, Hangida Ramadhani, alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakienda katika maeneo ya vijiji vya kata hizo na kutaka k...