BOHARI YA DAWA (MSD) YATWAA TUZO YA MLIPA KODI BORA 2023
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai (kushoto) akipokea tuzo ya mlipa kodi bora. MSD Yatwaa Tuzo Ya Mlipakodi Bora 2023 .............................................. Na Mwandishi Wetu BOHARI ya Dawa (MSD), imetwaa tuzo ya Mlipakodi Bora kwa mwaka 2023 ya Mamlaka ya Kodi Tanzania. Tuzo hizo zimetolewa usiku wa Novemba 24, 2023 katika hafla maalum ya wiki ya Mlipakodi zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijiini Dar es Salaam ambako Bohari hiyo imeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha WalipakodiWalipakodi wa Kati kwa Mkoa wa Kikodi wa Temeke. Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai amesema ushindi huo una maana kubwa kwa Bohari hiyo na Watanzania. Amesema MSD ambayo ni moja ya Taasisi za kimkakati za Serikali inayohusika na kuzalisha, kununua, kutunza na kusambaza bidhaa za afya kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali nchini inafuata taratibu, sheria na miongozose ikiwa ni pamoja na kulipa kodi stahiki. "Maendeleo yoyo...