WADAU WA MSD WAHIMIZWA KUSIMAMIA MATUMIZI SAHIHI YA TAKWIMU BIDHAA ZA AFYA
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauteri Kanoni, akifungua kikao cha wadau na wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mtwara Machi 22, 2024. ........................... Na Mwandishi Wetu , Mtwara WADAU wa Afya wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Mtwara wamehimizwa kusimamia matumizi sahihi ya takwimu za mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya, ili ziwawezeshe kufanya maamuzi sahihi juu ya bidhaa hizo katika maeneo yao. Akifungua kikao cha wadau na wateja wa MSD kanda ya Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauteri Kanoni amesema uwepo wa takwimu sahihi unaiwezesha MSD kuagiza kwa usahihi bidhaa za afya na kuboresha upatikanaji wa bidhaa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Aidha, amewashauri MSD kuhakikisha utaratibu wa vikao vya mwaka vya wadau ni muhimu kwa pande zote mbili, yaani Bohari ya Dawa (MSD) yenyewe na wadau ili kwa pamoja kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya, kwa kujadili changamoto na kuzitafutia utatuzi. Kwa upande wake Meneja wa MSD Kanda ya Mtwar...