Posts

Showing posts from April, 2024

MSD YAFAFANUA SINTOFAHAMU ILIYOSAMBAA KATIKA VYOMBO VYA HABARI

Image

MSD YAKUTANA NA WADAU WAKE KANDA YA IRINGA, RC RUVUMA ATAKA WELEDI SEKTA YA AFYA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Ahmed Abbas Ahmed (kushoto) akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji wa Bohari ya Dawa (MSD), Victor Sungusia wakati wa mkutano mkuu wa MSD na  wadau wake wa Mkoa wa Ruvuma uliofanyika Aprili 8, 2024,  Na Mwandishi Wetu, Ruvuma MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Ahmed Abbas Ahmed, amewataka watumishi wa sekta ya afya Mkoani Ruvuma, kuzingatia weledi na kutoa huduma bora kwa wananchi, ili kuakisi maboresho na uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye sekta ya afya, chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita. Kanali Ahmed amesisitiza kuwa, serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi kwa ajili ya maboresho na ujenzi wa miundombinu ya afya mathalani majengo, ununuzi wa bidhaa za afya  na kuwezesha ajira za kutosha,  lengo likiwa kuinua hadhi ya huduma zinazotolewa nchini, hasa zinazomgusa mtanzania wa kawaida. Kanali Ahmed ametoa rai hiyo hii leo, wakati wa akifungua kikao kazi baina ya MSD Kanda ya Iringa na ...

WANANCHI ITIGI WAMSHUKURU RAIS , KITUO CHA AFYA KUANZA UPASUAJI

Image
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida, Hussein Simba, akizungumza wakati akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Aprili 3, 2024. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ayubu Kambi na na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Jonathan Hemed. .................................. Na Mwandishi Wetu, Itigi WANANCHI wa Kata ya Rungwa iliyopo wilayani Itigi mkoani Singida wamemshuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea Kituo cha Afya ambapo sasa wajawazito wameanza kupata huduma ya upasuaji na kuondokana na changamoto waliokuwa nayo ya kufuata huduma hiyo Hospitali ya St. Gasper iliyopo Itigi. Diwani wa Kata hiyo Said Sudi akitoa shukurani hizo kwa niaba ya wananchi wake wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichoketi Aprili 3, 2024 alisema hawana cha kumlipa Rais Samia zaidi ya kumpa kura zote katika uchanguzi mkuuu utakaofanyika mwakani. "Kata yetu tutampa kura asilimia 100 mama yetu kwa kazi kubwa aliyotufanyia si kwa kituo cha afya ...