WANAFUNZI WAPYA TAASISI YA UHASIBU MKOA SINGIDA WATAHADHARISHWA KUTOJIHUSISHA MAPENZI NA WALIMU
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, ambaye pia ni Mratibu wa taaluma, Flora Lemnge, akizungumza na wanafunzi wapya wa kampasi hiyo katika semina elekezi kwa wanafunzi hao iliyofanyika Oktoba 30, 2023. Kutoka kushoto ni Mlezi wa Wanafunzi, Asia Hansy, Mshauri wa wanafunzi, Ambwene Kajula, Mratibu wa Mipango na Dawati la Malalamiko wa taasisi hiyo, Magreth Emmanuel. .................................................................... NA DOTTO MWAIBALE, SINGIDA WANAFUNZI wapya waliochaguliwa kujiunga na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida kwa msimu wa masomo wa 2023/2024 wametakiwa kutojihusisha na uhusiano wa kimapenzi na walimu. Kaimu Mkurugenzi wa kampasi hiyo ambaye pia ni Mratibu wa taaluma, Flora Lemnge, ameyasema hayo jana Oktoba 30, 2023 katika semina elekezi kwa wanafunzi hao na kueleza kuwa mwanafunzi atakayejihusisha na uhusiano wa kimapenzi ...